Sunday, 12 February 2023

Rais Samia afunguka “akikupa Stress achana nae, maisha yako ni zawadi pekee Mungu amekupa




Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu amewasihi Wanafunzi wa Vyuo kuweka mkazo kwenye masomo na maisha yao na kujiepusha na mambo ambayo yatawarudisha nyuma na kusema hata kama Mtu ana Mpenzi ambaye anampa mawazo ni bora kuachana nae kwasababu kupigania maisha ni muhimu kuliko kupigania upendo wa kuharibiana maisha.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akizungumza na Wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (TAHLIFE) leo February 11,2023 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma “Nimuombe Mungu awashushie wote baraka mfanikiwe na yale mnayofanya, mnaosoma msome vema ile kurudia mwaka isiwepo, uki-disco usirudishwe nyumbani lakini kwanini udisco Mwanangu kwanini udisco kama kuna Mtu anakutia mawazo sio ebu achana nae angalia maisha yako kwanza”

“yapo tumetoka huko, inawezekana kuna lijitu huko kila ukigeuka lipo ukigeuka lipo linakusumbua achana nae, your life is yours ni zawadi pekee Mungu amekupa, chunga maisha yako haya mambo mtakutana nayo mbele, pale utatafuta unayeweza kuishi nae
vizuri”

“Kwa sasa chunga maisha yako usimpe Mtu mwingine nafasi ya kukuharibia maisha yako hapana, hakuna upendo wa kuharibiana maisha, akisema ‘nitakufa juu yako’ akafe umuone, nitakufa juu yako chozi linamtoka unamwambia kajinyonge haendi asikuharibie maisha, someni kwa bidii lakini msiacha kumtegemea Mungu”.


Habari picha na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment