Naibu Waziri wa Ardhi ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa pikipiki kwa watendaji wa kata 6 za Halmashauri ya Chalinze, pamoja na kutembelea kiwanda cha Uzalishaji wa marumaru cha Keda.
Pia, amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Vituo Vya Afya kwa ajili ya Vituo Vya Afya Viwili Kata za Kibindu na Msata na Zahanati vijiji 11.
Akigawa Pikipiki hizo, Ridhiwani amewakumbusha Watendaji kutumia vifaa hivyo kwa kuzingatia makusudio ya kutolewa kwa vyombo hivyo vya moto ikiwemo kwenda kusikiliza wananchi na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao.
Vilevile akikabidhi vifaa tiba wamehimizwa kuvitunza na kuvitumia kwa makusudio vifaa hivyo.
"Kazi kubwa inaelekezwa kituo cha Afya Miono ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa kipaumbele";: Kwa upande wa kiwanda tumewashukuru wawekezaji kwa kutambua mchango wa Raisi Dkt. Samia Suluhu #KaziInaendelea
Habari Picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment