(CUF- Chama Cha Wananchi)
Office of the National Chairman
P.O. BOX 10979 Dar es Salaam,
Tanzania
E-mail:
lipumba@yahoo.com
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI, 08 FEBRUARI 2023
SAKATA
LA FEDHA ZA PLEA BARGAINING ZILIZOKUSANYWA NA AFISI YA MWENDESHA MASHTAKA (DPP) NA UCHUNGUZI WA KILE
KILITOCHOKEA MPAKA BAADHI YA FEDHA HIZO KUTOJULIKANA ZILIPO
Sambamba na
uzinduzi wa Tume hiyo, Chama cha Wanaanchi-CUF tunafahamu juu ya uwepo wa
uchunguzi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni50 unaofanywa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG. Fedha hizizilipatikana kutokana na
utaifishwaji wa mali za Watanzania waliotuhumiwa kwa makosa ya jinai mbalimbali
na kupelekea makubaliano na serikali kupitia ofisi ya DPP yaani “Plea
Bargaining” ambao utahusisha kuhojiwa
kwa watu mbali mbali waliohusika katika jambo hilo.
Ndugu wanahabari,
kama mtakumbuka “Plea bargaining” ililetwa na mabadiliko ya sheria ya mwenendo
wa makosa ya jinai yaliyofanyika mwaka 2019 na kuendeshwa na ofisi ya Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP) kwa kuingia makubaliano na Watuhumiwa wa makosa ya jinai
ambao wengi wao hawakuwa wamepewa dhamana kutokana na makosa yao kutokuwa na
dhamana. Hata hivyo sheria hii ilitekelezwa na DPP hata kabla ya Mhe. Jaji Mkuu
kutunga kanuni za namna bora ya kutekeleza utaratibu wa “Plea bargaining” ambao
ungeainisha mambo muhimu kama akaunti ipi ambayo fedha hizi zipelekwe na kuweka
wazi namna ya matumizi ya fedha hizi.Jambo la kusikitisha zaidi, sehemu ya
fedha hizi zilipokelewa na DPP mwenyewe kwa njia ya fedha taslimu kinyume cha
sheria za nchi na zingine kuwekwa katika akaunti nchini Chinakama alivyoeleza
Mhe. Rais.
Ndugu wanahabari, Sisi
CUF-Chama Cha Wananchi tunaamini kwamba, kazi ya kuchnuguzana kutazama nini
kimetokea na nini kiliharibu ofisi hii ya DPP na kupelekeasehemu ya fedha hizo
za umma kutojulikana zilikowekwa haitoweza kufanikiwa kutekelezwa kwa uhuru na
TUME hii iliyoundwa na Mhe. Rais iwapo aliyekuwa Mkurugenzi wa Ofisi hiyo
kipindi cha Plea Bargaining; Jaji Biswalo bado anashikilia nafasi ya juu katika
moja ya ofisi ya utoaji haki, yaani Mahakama Kuu.
Na kama alivyosema
Mheshimiwa Rais kuwa kubadilisha Mkurugenzi wa ofisi hizi peke yake hakutotosha kumaliza mizizi inayopelekea kujitokeza
kwa mapungufu haya ya kiofisi, Sisi CUF -Chama Cha Wananchi tunaamini ili
kuhakikisha ofisi hizi zinabadilika kabisa na kutekeleza majukumu yake kwa
Muktadha wa Misingi ya Kikatiba, Demokrasia,
Haki sawa kwa wote na Utawala bora kwa mujibu wa sheria, basi hata wale
watumishi waliokuwa wakimsaidia Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kipindi hicho cha
“Plea Bargaining” wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi huru wa TUME hiyo na uchunguzi
wake utakuwa wenye tija na kufuata Utawala wa Sheria pamoja na kurejesha imani
ya Watanzania katika ofisi husika.
Tume pia ichunguze
na kubainisha kama kuna viongozi na taasisi nyingine zilizohusika katika sakata
hili.
Pamoja na uchunguzi
wa fedha zilizopokelewa taslimu na zilizowekwa kwenye akaunti za benki, pia
Tume ichunguze mali zisizohamishika zilizowekwa kama dhamana kwa wale
walioshindwa kulipa fedha taslimu, kama bado ziko mikononi mwa Serikali au
zimerejeshwa kinyemela.
Na mwisho, wale
watakaobainika wamehusika katika sakata hili ama la upotevu wa fedha au
matumizi mabaya ya ofisi husika basi wachukuliwe hatua za kisheria ili kuzuia
matukio kama haya kujirudia tena.
Tuna matumaini Tume
itafanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu, bila woga wala upendeleo na tunaitakia
utekelezaji mwema wa majukumu yake.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF - Taifa
Habari kamili na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment