Sunday, 12 February 2023

Picha: Ajali yaua mmoja, majeruhi 7 “Basi lilifeli breki na kutumbukia korongoni

 

Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine Saba kumjeruhiwa katika Kata ya Sigino Wilayani Babati Mkoani Manyara baada ya gari la abiria aina ya Costa kufeli breki na kutumbukia katika korongo.

Akizungumza na Ayo TV kwa njia ya simu kuthibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Acp George Katabazi amesema gari hilo lilikuwa likitokea Mkoani Singida kuelekea Arusha na baada ya kufika eneo la 

Kona ya Logia ndipo likafeli breki na kumshinda dereva.

“Ajali imetokea asubuhi gari lilikuwa na watu 29 abiria ni 27 dereva mmoja pamoja na utingo wake, dereva amefariki huku majeruhi wakiwa 7 ambapo kati yao watatu hali zao ni mbaya ila abiria wengine walipata mshtuko tu, chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa breki wa gari hali iliyopelekea kumshinda dereva kulimudu gari hilo na kuingia kwenye korongo”-RPC Katabazi

Habari picha na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment