Sunday, 12 February 2023

RC Makalla afunguka kuhusu Machinga na Bodaboda kwenda Afrika Kusini

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla ametoa tamko rasmi kwa Viongozi wa machinga na bodaboda kwenda ziara ya mafunzo Afrika ya Kusini, ameyasema hayo leo Februari 11,2023 katika Ukumbi wa DMDP Ilala wakati akipokea taarifa kwa Viongozi hao baada ya kurejea kutoka ziara ya mafunzo nchini Rwanda.

CPA Makalla amesema amefurahishwa na matokeo ya ziara ya mafunzo waliyoifanya 

nchini Rwanda kufuatia taarifa waliyoiwasilisha kwake.

Aidha CPA Makalla amefafanua kuwa miji ya Cape Town na Johanesburg Afrika ya Kusini ni miji katika tano bora kwa usafi Afrika hivyo ziara ya mafunzo nchini humo itapelekea kuleta mapinduzi makubwa zaidi ya Kampeni ya Usafi Jijini Dar es Salaam.

CPA Makalla amewataka Viongozi wa Machinga na Bodaboda kuitisha makongamano kushirikisha elimu waliyoipata nchini Rwanda kwa wanachama wao ili kuwa na uelewa wa pamoja ambao utalifanya Jiji la DSM kusonga mbele katika mikakati yake.

Hata hivyo CPA Amos Makalla amesema “Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuyalea makundi haya kufanya Kazi vizuri anachokifanya yeye katika Mkoa ni utekelezaji kwa vitendo maelekezo na maono ya Mhe Rais”- RC Makalla

CPA Makalla amewahakikishia Viongozi wa Machinga na Bodaboda kuendelea kuwapatia ziara za mafunzo kwa kadri inavyo wezekana kwa kuwa kuelimishana ni njia pekee na bora ya kuleta mabadiliko chanya.


Habari picha Ally Thabit

No comments:

Post a Comment