Sunday, 30 June 2024

MBUNGE WA CHALINZE ANUSULU VIFO VYA MAMA NA MTOTO


 Riziwani Kikwete Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri amesema wameamuwa kuleta Msoga Marathon Lengo kupata fedha kwaajili ya kununua vifaa vya kuwaifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya kutimiza miezi tisa (NJITI) .

amewashukuru watu,makampuni,taasisi, viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa kiserikali na wadau mbalimbali kwa kushiriki kwenye Msoga Marathon na kutoa michango yao mbalimbali . Kwani yeye mbunge wa Chalinze ameahidi fedha zilizopatikana zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Na amesisitiza kuwa Msoga Marathon itafanyika kila mwaka amesema haya mkoani Pwani wilaya ya Chalinze kata ya Msoga kijiji cha Msoga  kwenye mbio za Msoga Marathon .

Habari picha na Ally Thabit 

Wednesday, 26 June 2024

RAIS KIKWETE KUNOGESHA MSOGA MARATHON

 Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 wa Tanzania Dr Kikwete amepongeza waandaaji wa Msoga Marathon kwani mbio hizi zinampango wa kukusanya kiasi cha fedha milioni Mia tatu therasini ambako zitaenda kutumika kwenye kununua vifaa kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda na ujenzi wa vyumba vya kujifungulia mamawajawazito haya ni malengo mazuri ndio maana yeye anaunga mkono mbio za msoga marathon kushiriki kwenye mbio hizi na kutoa pesa na anatoa wito kwa taaasisi, makampuni,viwanda na watu binaus kushiriki na kuchangia zoezi hili amesema haya wakati akihojiwa na wasafi TV na redio.

Habari na Ally Thabit 

WAFANYA BIASHARA WAPEWA MATUMAINI

 Mwenyekiti  wa Wafanyabiashara  Martini Mbwana anawataka wafanyabiashara kufungua maduka yao kwani changamoto walizoolozesha kamati ya waziri mkuu baadhi washazifanyia kazi na vikao vinaendelea kati ya kamati ya waziri mkuu na Wafanyabiashara lengo wafanya biashara wasitishe kufunga maduka yao.

Mpaka sasa mikoa ambayo wafanyabiashara wamefunga maduka yao .Arusha,Mbeya,Mwanza,Tanga,Mtwara na dar es salaam.  Mwenyekiti wa wafanyabiashara  Martini Mbwana  amesema hii inaleta athari kwa uchumi wa tanzania na uchumi wa mtu mmojammoja ivyo anatoa rai kwa wafanyabiashara  kufungua maduka yao kwani hata mkuu wa mkoa wa dar es salaam CHALAMILA ameimiza hekima na busara itumike na si kufunga maduka kwani kitendo cha kufunga maduka ni kukiuka maagizo na maelekezo ya waziri mkuu Amesema haya jijini 

Habari na Ally Thabit 

Tuesday, 25 June 2024

PROF LADSLAUS MNYENE ATOASIRI NZITO ELIMU KIDIGITALI


 Mkurugenzi wa  Idara ya Sayansi na Teknolojia Wizara ya Elimu Prof Ladslaus Mnyane  amesema Utoaji elimu kwanjia ya kidigitali kuanzia elimu ya Awali ,msingi ,secondary na vyuo vikuu itasidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufundishwa masomo kwa muda mfupi wakiwa wengi,walimu watafundisha wanafunzi kwa uchache wao,itapunguza gharama kwa serikali kwa kutoajili walimu wengi.

Katika mabadiliko ya kiteknolojia duniani tanzania tukiwafundisha wanafunzi kwa njia za kidigitali itawawezesha wanafunzi baada ya kumaliza shule na vyuo vikuu watakuwa wameshabobea katika matumizi ya kidigitali . Hivyo ufanisi utaongezeka kwa kiasi kikubwa katika utendaji kazi kwenye sekta mbalimbali mfano kwenye sekta ya madini,sekita ya kilimo,sekta za maji na sekta zinginezo.

Prof Ladslaus Mnyane amesema lengo la kutoa elimu kwa njia ya kidigitali kuwezesha watanzania kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ya sasa na ya baadae,pia wanatarajia serikali na watu binaus kutekeleza mpango huu kwa vitendo  ifikapo mwezi7/2025  .Swala la kujumuisha na kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu ili wapate elimu kwa nia ya kidigitali ni jambo muhimu na linatija kwa tanzania amesema haya jijini dar es salaam kwenye mjadala wa kupokea maoni kwa wadau wa elimu  kwa namna gani ya kukamilisha mpango wa kutoa elimu kwa njia ya kidigitali.

Habari picha na Ally Thabit 

ROJERS FUNGO WA TARSIWAKUTANA NA WAANDISI WA BARABARA

 Meneja wa taasisi ya TARSI  Rojers Fungo Taasisi yao imeamuwa kufanya semina ya siku tano5 na Waandisi wa barabara pamoja na Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu  na watu wa serikalini lengo kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kudhibiti ajali za barabarani . Semina hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho ya seranq maboresho yakutumia teknolojia za kisasa katika utengenezaji wa barabara.

Rojers Fungo ametoa wito kwa washiriki wa semina hii wazingatie mafunzo na watendee kazi watakayoyapata kwenye semina .

Habari na Ally Thabit 

Monday, 24 June 2024

KATIBU WA MAY SALA AJA NA MUAROBAINI WA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA

 Amadi Sefu Katibu wa May Sala Mbio za Pole ili watu waepuke kupata magonjwa yasiyoambukiza ni vyema wakajiunga na vikundi vya mbio za pole .pia vikundi vya pole vinajenga umoja,mshikamano,kudumisha amani na kuchochea ukuaji wa uchumi amesema haya kwenye viwanja vya barafu jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

WATU WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU

 Mratibu wa Damu Salama Wilaya ya Kinondoni anawataka watu wawewanachangia damu mara kwa mara kwani damuinasaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto amesema haya kwenye viwanja vya barafu kaika bonanza lililoandaliwa na kikundi cha barafu wilaya ya kinondoni .

Kwenye bonanza ili watu wamechangia uniti 22 za damu .

Habari na Ally Thabit