Hajati Shamimu Kani Mwenyekiti wa Wanawake kutoka Baraza la Kiislam Tanzania (BAKWATA) amewataka wanawake viongozi kushirikiana na Wanawake wengine katika kuwajengea uwezo wa Uongozi.
Pia wasikubali kukandamizwa na kunyonywa na mifumo dume na wapige vita ndoa za utotoni,mimba za utotoni na aina zote za ukatili zinazojitokeza katika familia,Jamii,maofisini,masokoni na mahara popote
Tukifanya hivi tutapata Wanawake wengi na bora katika nafasi za Uongozi. ametoa rai kwa wanaume kuwaunga mkono wake zao wanapowania nafasi za kazi na Uongozi .ameipongeza TGNP Mtandao kwa kuja na proglam ya kuwajengea uwezo Wanawake katika Uongozi
Habari na Ally Thabiti