Wednesday, 17 March 2021

ANA MAKINDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA TGNP

 Spika wa Bunge Mstaafu Ana Makinda ameutaka Mtandao wa kijinsia (TGNP Mtandao ) kuweka mifumo ya kanzi data ya Wanawake  viongozi.  Pia wawajengee uwezo watoto wa kike kuanzia shule ya msingi .

 Ametoa wito kwa wanawake viongozi kuwa nafasi walizozipata wazitumie vizuri na wazitendee haki waepuke na maswala ya Ufisadi wawe wahadirifu ,Uaminifu na waweze kutatua changamoto za kijamii.

Uku akiwataka watunga  sera na wapanga bajeti wazingatie usawa wa kijinsia na ameipongeza TGNP Mtandao kwa kuwajengea uwezo Wanawake viongozi 

Habari na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment