Wednesday, 28 April 2021

MUFUTI WA TANZANIA KUWAINUA WENYE ULEMAVU


Mufuti Mkuu wa Tanzania  Abubakari bin Zuberi  amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye Ulemavu wawapeleke wakasome maswala ya Dini  ,kwani baraza kuu la waislam Tanzania  (BAKWATA)  litatoa  mafunzo ya kwa wasio Ona kwa kutumia maandishi ya nukta nundu ambako kutakuwa na mwalimu kutoka Morogoro .

Mufuti ametoa wito kwa waislam na watanzania kipindi hili cha mwezi mtukufu wa ramadhani kuwaombea viongozi wetu wa nchi  na kuiombea Amani iendelelee kuwepo Tanzania . amesema haya nyumbani kwake Magomeni Mikumi jijini Dsm wakati akiongea na Wanahabari .

Habari picha na Ally Thabiti


No comments:

Post a Comment