Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA ) kwa kudhirikiana na Friedrich Ebert Stiftung (FES) Kutokana na mabadiliko ya Tekinolojia wameamua kuja na kampeni maalum ya kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa mitandaoni(ZIMICA )
Kampeni hii ya mwezi 1 kuanzia mwezi 4 hadi 6 mwaka 2021 ,Inalenga kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na watoto wa kike.
Ataivyo Roes Reuben Mkurigenzi wa Tamwa amesema ukatili wa kijinsia unaofanywa katika hali ya kudhuru mwili,vipigo,ubakaji,ulawiti,ukeketaji,ndoa za utotoni ,mimba za mapema,rushwa ya ngono na matusi .
Ukatili huu unafanyika kwa njia ya intranet kama fece book,whatsapp,instagram, you tubu na twitter
Ambako Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha ongezeko kubwa la watumiaji wa intanet .ambako mwaka 2017 waliongezeka kwa asilimia 16 na kufikia 23 milioni na asilimia82 kati yao walitumia mitandao hivyo kwa njia ya simu .
Mala kadhaa tunaona video za utupu za Wanawake,watoto wa kike zinasambazwa kwa makusudi na video za ngono huu ni uzalilishaji unaofanywa mitandaoni ,udhalilishaji huu una madhara kisaikolojia na hata kupelekea kujiua na kupoteza mwelekeo wa maisha.
Roes Reuben Mkurigenzi wa Tamwa amesema nia ya TAMWA na FE S ni kuzuia ukatili na kuongeza uelewa kwa jamii na kujua madhara ya ukatili hasa kwa Wanawake na kujua mbinu za kuepuka udhalilishaji.
Zipo sheria zinazozuia ukatili mfano sheria ya maudhui ya mitandaoni (online content Regulation) inakataza kutoa na kurusha maudhui ya udhalilishaji unaokwenda kinyume na Tamaduni ya Mtanzania.
Kuendelea kwa ukatili huu pengine kwa waasirika kutofahamu sheria na au kuona aibu katika kuitafuta haki na hofu ya kuzalilika zaidi pindi kesi inapopelekwa mahakanani .
Tamwa wamesema ni vyema kujua kuwa udhalilishaji huu haukubaliki, ni muhimu kutambua kuwa zipo sheria zinazotulinda na muhimu kujua wapo wadau wanao weza kutusaidia.
Aidha kuna hadhabu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii vibaya ikiwemo faini ya sh milioni 5 au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwapamoja . Tamwa wametoa wito kwa selikari na asasi za kiraia kuzungumzia madhara ya vitendo vya ukatili wa mitandaoni ,na kutoa elimu kwa jamiii na kwa kizazi cha sasa , kuusiana na madhara ya kuitumia mitandao ya kijamii kama njia ya kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Pia Tamwa wametoa wito kwa jamii kuwa maswala ya ukatili wa kijinsia ni jukumu la kila mmoja wetu ,asasi za kiraia,madawati ya kijinsia,selikari,jeshi la polisi wasaidizi wa sheria na wasanii kukemea na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia
Habari na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment