Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Limewapata na Kuwahoji wasichana wawili ambao ambapo mmoja wa miaka16 Mwanafunzi wa kidato cha pili na mwingine wa miaka 12 Mwanafunzi wa Darasa la saba wakazi wa vijibweni kigamboni kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na watekwaji wanataka pesa.
Ufuatiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubainiwatoto hawa walipokuwa na baada ya mahojiano ya kina walikiri kutengeneza tukio hili la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka tarehe 26/01/2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi tarehe 27/01/2025 asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipo kamatwa wakiwa wanazunguka. Jeshi linalaani vitendo vya hivi vya watu wenye lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda ya Maalum Dar es salaam katika kipindi cha Desemba hadi Januari 2025 katika kusimamia mifumo ya haki jinai mahakamani baadhi ya watuhumiwa mbalimbali walipatikana na hatia ikiwa ni pamoja na Idrisa Rasshid miaka [35] Mkazi wa Kwembe Kimara alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Paul Elisha miaka (37) mkazi wa Mbezi Beach kwe nye Mahakama ya Kinondoni alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka na Jackson Mgeta (34) mkazi wa Kawe alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Jeshi la Polisi lina wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana ili kuimarisha mifumo ya ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kutekeleza falsafa ya ulinzi shirikishi ili kuzuia vitendo vya kihalifu. Imetolewa na Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam.
Habari na Ally Thabit Mbungo.