Friday, 7 February 2025

ASCP MULIRO J. AELEZEA WATOTO WALIOJITEKA

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam  Limewapata na Kuwahoji wasichana wawili ambao ambapo mmoja wa miaka16  Mwanafunzi wa kidato cha pili na mwingine  wa miaka 12 Mwanafunzi wa Darasa la saba  wakazi wa vijibweni kigamboni kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa  na watekwaji wanataka pesa.

Ufuatiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubainiwatoto hawa walipokuwa na baada ya mahojiano ya kina  walikiri kutengeneza tukio hili la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka  tarehe 26/01/2025 na kuelekea  Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi tarehe 27/01/2025 asubuhi na  baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipo kamatwa  wakiwa wanazunguka. Jeshi linalaani vitendo vya hivi vya watu wenye lengo la kujipatia  pesa kwa njia za udanganyifu.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda ya  Maalum Dar es salaam  katika kipindi cha Desemba hadi Januari 2025 katika kusimamia mifumo ya haki jinai mahakamani baadhi ya watuhumiwa mbalimbali walipatikana na hatia  ikiwa ni pamoja na Idrisa  Rasshid miaka [35]  Mkazi wa Kwembe  Kimara alihukumiwa  miaka 30 jela kwa kosa la kubaka kwenye Mahakama ya Wilaya ya  Kinondoni.  Paul Elisha miaka (37) mkazi wa Mbezi  Beach kwe nye Mahakama ya Kinondoni alihukumiwa kifungo cha maisha  jela kwa kosa la kubaka na Jackson Mgeta (34) mkazi wa Kawe alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

Jeshi la Polisi lina wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana ili kuimarisha mifumo ya ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kutekeleza falsafa ya ulinzi shirikishi ili kuzuia  vitendo vya kihalifu. Imetolewa na Kamanda  Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit Mbungo. 


No comments:

Post a Comment