Saturday, 22 February 2025

KATIBU MKUU NA MSEMAJI WA SERIKALI ABAINISHA MIKAKATI YA WAKULIMA WA KAHAWA


 Greyson Msigwa Katibu Mkuu na Msemaji wa Serikali amesema kuwa serikali ya tanzania imeweka mazingira rafiki na wezeshi kwenye zao la kahawa kwa kuwapa wakulima wa kahawa pembejeo zenye ubora na za kisasa ,Mbegu zenye ubora,Mafunzo kwa wakulima wa kahawa,Teknolojia za kisasa na zenye ubora na kufanya tafiti pamoja na kuwatafutia masoko wakulima wa kahawa ndani ya nchi na nje ya nchi.

Lengo la kufanya haya yote ni kuwainuwa wakulima wa kahawa kiuchumi na kuongeza uzalishaji wenye tija katika kahawa . Baada ya serikali kuyafanya haya yote chini ya rais Dr samia hatimae kahawa ya tanzania imepanda thamani kubwa na kupelekea kahaya ya tanzania kuuzika katika masoko ya kitaifa na kimataifa .

Katibu Mkuu na Msemaji wa Serikali amesisitiza kuwa watu wenye ulemavu katika zao la kahawa wanashirikishwa kikamilifu Pia kupitia mradi wa BBT watu wenye ulemavu  wapo na kupitia mikopo ya halmashauri watu wenye ulemavu wanapewa pesa kwaajili ya kufanya biashara mbalimbali amesema haya kwenye mkutano 3RD G25 AFRICAN SUMMIT 2025 uliofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit Mbungo 


No comments:

Post a Comment