Friday, 12 March 2021

MENEJA WA KODI MKOA WA TEMEKE AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

 Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke Poo Wararaze amesema kuanzia tarehe 10mwezi3 2021 wameanza kutoa elimu kwa mlipa kodi kwenye Wilaya ya Temeke.  Lengo kujenga mazingira rafiki kwa wafanya biashara wadogo, wakati na wakubwa waweze kulipa kodi kwa kiwango kikubwa.

Hii itasaidia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali Meneja  wa TRA amesema kampeni ya Mlango kwa Mlango si kwaajili ya kuwakamata wafanya biashara na wawekezaji ndani ya Wilaya ya Temeke .

 Hivyo amewataka wajitokeze kwa wingi na watoe ushirikiano kwa elimu inayotolewa ambako mwisho tarehe 26 mwezi3 2021 elimu hii itawafikia watu wenye Ulemavu  Pia wameandaa vipeperushi vya Nukta Nundu am kwaajili ya wasio Ona . amesema haya kwenye Ofisi ya Wilaya ya Temeke jijini Dsm 

Habari Victoria Stanslaus

TCRA YATEMA CHECHE KWA MATAPERI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mwandisi John Kiraba  amesema  makampuni yote ya Simu yenye tabia yakuweka vifurushi pasipo utaratibu hatua kali zitachukuliwa dhidi yao 

Habari na  Ally Thabiti

WAZIRI WA ARDHI ABAINI UFISADI

 William Lukuvi Waziri wa Nyumba Maendeleo na Makazi amesema  Watumishi wa Chuo cha Marogoni wakamatwe mara moja kwakuiba milioni500 kwa wakazi wa Kata ya Kivule wakati wa kurasimisha Ardhi ya wana Kivule 

Habari na Victoria Stanslaus

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SEKTA YA NISHATI NA MADINI ASIKITISHWA

 Nikodemius Kajungu amesema  kwanafasi yake ya Katibu Mkuu  anasikitishwa na kuuzinishwa kiwango cha pesa wanacholipwa Wachimbaji Madini  kwani ni kidogo na hakikidhi mahitaji yao.

Hivyo ameitaka TEITI kuandika ripoti za kutatua changamoto hii amesema haya kwenye Ofisi za Bunge posta jijini Dsm  

Habari na Victoria Stanslaus











WACHIMBAJI MADINI WADOGO WATOA NENO KWA TEITI

 Katibu wa Wachimbaji Madini Wadogo Tariki amesema wachimbaji wadogo wameweza kutoa bilioni 128 hivyo ameitaka TEITI washirikishe wachimbaji wadogo  kikamilifu wanapoandaa ripoti zao ili wawasirishe keto na changamoto zinazo wakabili amesema haya kwenye Ofisi za Bunge posta jijini Dsm 

Habari na Victoria Stanslaus

WAZIRI WA MADINI ATOA CHOZI ZITO

 Doto Biteku Waziri wa  Madini ameitaka TEITI kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogo wa Madini kwa kutoa ripoti za kuwakwamuwa wachimbaji wadogo kuwa wakati na wakubwa

Waziri Doto Biteku ameitaka TEITI kuweza kujitangaza zaidi na kujenga mahusiano mazuri na taasisi zingine amesema haya kwenye Ofisi za Bunge posta jijini Dsm 

Habari na Victoria Stanslaus


Thursday, 11 March 2021

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AIPONGEZA TRA

 Mkuu wa Wilaya yaTemeke Godwini Gondwe amesema kampeni ya TRA ya Mlango kwa Mlango kwaajili ya kutoa elimu ya kuamasisha watu kulipa kodi ni mzuri  kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa mazingira wezeshi na rafiki  kwa wawekezaji na wafanya biashara wadogo,wakati na wakubwa kuenddelea kufanya shughuri zao ndani ya Temeke na wengine kuvutiwa kuja  kuwekeza Temeke . Pia kampeni hii ya TRA itasaidia katika ujenzi wa huduma za msingi ndani ya Temeke kutokana na pesa za walipa kodi  mfano barabara,hospitali na miundombinu mingineyo . Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwini Gondwe ametoa wito kuwa TINI namba ni bure na wananchi waTemeke wawape ushirikiano Maafsa wa TRA 


Habari na Victoria Stanslaus