Tuesday, 24 August 2021

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AWAITA WAWEKEZAJI

 Prof Kitlo Mkumbo Waziri wa Viwanda na Biashara amewataka watu kujitokeza Kwa wingi katika kuwekeza kwenye Viwanda 20. Pia amewataka  SIDO na NDC kuendeleza Viwanda walivyokabidhiwa na wizara ya Viwanda na Biashara .

Nae Mkurugenzi wa TEMLO prof Frederick  Kaimba amesema wameamuwa kutengeneza mashine za kutengeneza Sukari . Lengo kuwafikia Wajasilia mali wadogo na Kuwainua wakulima wa miwa na kuondoa uhaba wa upatikanaji wasukari Tanzania. 

Ujenzi wa Mashine hizi umefikia asilimia 40. Kiasi chabilioni 19 zitakuwa zimeokolewa kutokana na upatikanaji wa Mashine hizi. Mashine zitauzwa Kwa shilingi milioni Mia mbili hamsini.amesema haya jijini Dsm 

Habari na Ally Thabiti

Thursday, 5 August 2021

MO ATOA MABILIONI KWA SIMBA

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mo Deuji ametoa kiasi cha bilioni 20 kwaajili ya Uwekezaji Simba na amewataka wanasimba waendelee kumuunga mkono na watasajili wachezaji wa kimataifa .

Habari na Ally Thabiti 

CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI CHAWAKWAMUWA WANANCHI NA UMASIKINI

 Prof Mwabless Malila  amewataka watu kujiunga na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinatoa elimu bora ambako mtu  akimaliza kusoma anapata Ajira .

Pia Chuo hiki kupitia mradi wa UNDP kimewakwamuwa kiuchumi wakazi wa kanda ya Ziwa Kwa kuwapa elimu ya Viazi Lishe na Wavuvi WA kanda ya Ziwa wameweza kufundishia namna ya kutengeneza mabarafu .

Ambako Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinatoa elimu Kwa gharama nafuu Kwa ngazi ya Cheti,Diploma,Shahada ya Kwanza na zinginezo .

Chuo kinapatikana Mwanza eneo la Kisesa na Bwilu na Kwa Dodoma eneo la Miuji mjini ambako Hosteri zipo za kutosha  .prof Mwabless Malila ametoa wito kwa watu kukitumia Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kwa elimu,utafiti na ushauli amesema haya kwenye Maonyesho ya 16 ya Vyuo Vikuu yalioandaliwa na TCU ambako yamefanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dsm.

Habari na Ally Thabiti 


HAJI MANALA AMKALIA KOONI MO NA KUMSHIKA PABAYA


Aliye kuwa Msemaji wa Simba Haji Manala amemtaka Mwekezaji wa Simba amlipe pesa zake na  aache kuwaongopea Wana Simba kuwa ametoa pesa za Uwekezaji ndani ya Simba  si  kweli .

Amemtaka C.o wa Simba Barbra Hassani Aache kumfuatilia na kumpaka matope .

Habari picha na Ally Thabiti 

GLOBAL LINK EDUCATION YAJA KIVINGINE KIELIM


 Neema Mabula Meneja wa Tawi la Dsm Kutoka Global link Education amesema wanatoa mkopo wa  fedha wa asilimia 50 mpaka asilimia 70 kwaajili ya elimu .

Na wanawatafutia Wanafunzi fursa ya kwenda kusoma nchi za China ,Indiana nchi zinginezo Kwa gharama nafuu .Pia wanawatafutia Wanafunzi Vyuo vya hapa Tanzania  .

Global link Education wanapatikana Arusha,Mwanza,Mbeya eneo la Mwanjelwa, Dodoma,Zanzibar na Dsm  amesema haya kwenye Maonyesho ya Vyuo Vikuu viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dsm .

Habari picha na Alloy Thabiti 

TAWA YAWATA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA


 Mwenyekiti wa Bodi ya Tawa Jenelali  Mstaafu Hamisi Semfuko amewataka watanzania kujitokeza kwenye Uwekezaji wa Wanyama Poli ambako mwaka 2018 Tawa ilianzisha mchakato wa Uwekezaji .

Ametoa wito kwa watanzania waishio kwenye vijiji kutunza ,kulinda na kuhifadhi maeneo ya Hifadhi ya Wanyama Pol . Kwani watanufaika kiuchumi .

Amewataka makampuni ya kitanzania kujitokeza kwenye Uwekezaji wa Wanyama Poli kwani kwenye Kampuni 10 zilizojitokeza Kampuni 1 ya watanzania.

Habari picha na Ally Thabiti

MSANII WA KIMAREKANI AMWAGA MAMILIONI TANZANIA


 Msanii Kameko Tarnez Kutoka Marekani amekuja nchini Tanzania kwaajili ya kutafuta vipaji vya waimbaji ambako tarehe11 mwezi wa 10 mwaka 2021 shindano litaanza.

Huku Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 11 fedha ya kitanzania pia Kwa sasa atazinduwa I. P . Yake  na atarekodi nyimbo na Daimondi na Ally kiba pamoja na Amonaizi .

Amewataka watanzania kulinda na kudumisha Amani iliyopo na waendelee kuwa na umoja na amewataka wamuunge mkono Kwa ujio wake hapa Tanzania .

Habari picha na Ally Thabiti