Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dawasa Mkama Bwile amesema moja ya mipango mikakati yao ni kudhibiti uvujqji wa maji kutoka asilimia 40% mpaka ifike asilimia 30% ingawaje inatakiwa upoteaji wa maji iwe asilimia 20%.
Wednesday, 7 August 2024
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA DAWASA ABAINISHA MIKAKATI KABAMBE
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dawasa Mkama Bwile amesema moja ya mipango mikakati yao ni kudhibiti uvujqji wa maji kutoka asilimia 40% mpaka ifike asilimia 30% ingawaje inatakiwa upoteaji wa maji iwe asilimia 20%.
WANAHABARI WAWAPONGEZA DAWASA
Mwanahabari Mkongwe wa Tbc Anuali Mkama amesema kitendo cha Dawasa kukutana na wanahabari pamoja na waariri wa habari ni muhimu kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto za ujujaji wa maji ambako zaidi ya asilimia 40% maji ya dawasa yanapotea kwa kuvuja .
Hivyo kupitia wanahabari na waariri wa vyombo vya habari watatumia vyombo vyao vya habari katika kuelimisha jamii kutoa taarifa ya uvujaji wa maji ya dawasa na changamoto zingine zinazowakabili wateja wa dawasa.
Mwanahabari Anuali Mkama amesema semina hii imekuwa kiunganishi kati ya dawasa ,waariri wa vyombo vya habari na wanahabari amesema haya kwenye semina kati ya dawasa ,waariri wa vyombo vya habari na wanahabari jijini dar es salaam ukumbi wa mwalimu nyerere.
Habari picha na Ally Thabit
Tuesday, 6 August 2024
RAISI WA WAKANDARASI WANAWAKE WAIPONGEZA BANKI YA NMB
Raisi wa Wakandarasi Wannawake Mwandisi Judith Odongo amesema Nmb kuwaongezea kiwango cha fedha imewasaidia katika swala la mtaji kwani wataweza kufanya miradi mikubwa nchini tanzania .
Raisi wa wakandarasi wazawa mwandisi Judith Odongo amesema faida wanazozipata kuongezeka kwa uchumi kwa mtu mmojammoja na nchi kwa jumla 'kuongezeka kwa kodi,kukuwa kwa ajira ambako vijana wengi watapata ajira ya vibaruwa au za kudumu.
Judith Odongo amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwa wakandarasi ambako kwa sasa wanawake 350 ni wakandarasi na wenye ulemavu wawili 2akiwemo mwandisi mkongwe mama Esta amesema haya wakandarasi wakiwa na nmb banki jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
NMB YAWATAKA WAKANDARASI WAZAWA KUCHANGAMKIA FURSA
Nmb benki imeongeza kiwango cha mkopo kwa wakandarasi wazawa kutoka bilioni mbili nukta tano 2.5 mpaka bilioni tatu na kuweka kiwango kidogo cha riba .amesisitiza kuwa nmb benki itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wakandarasi wa kitanzania amesema haya nmb benki walipokutana na wakandarasi wazawa.
Habari picha na Ally Thabit
NAIBU WAZIRI WA UJENZI AMEWAPONGEZA NMB BENKI
Naibu Waziri wa Ujenzi Mwandisi Godfrey Kasekenya aipongeza Banki ya NMB kwa kuwapa fursa Wakandarasi wa ndani kwa kuwaongezea kiwango cha fedha ambako akina riba kubwa hii itawawezesha na kusaidia wakandarasi wazawa kufanya miradi mikubwa na kukamilisha kwa wakati .
Ambako mwanzo wakandarasi wazawa walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya mitaji,Naibu Waziri wa Ujenzi amesema raisi dkt Samia kafanya maboresho ya sheria kwa wakandarasi wazawa kufanya miradi ya bilioni hamsini 50 ambako hapo mwanzo walikuwa wakifanya miradi ya bilioni kumi 10
Amesema haya jijini dar es salaam kwenye mkutano wa wakandarasi na benki ya nmb.
Habari picha na Ally Thabit
SHULE YA ST.MARKS INATOA ELIMU YA VIWANGO VYA JUU
Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Mkuranga Juma Saidi Maghahira anawata wazazi na walezi wawapeleke watoto wao kwe ye shule ya St. Marks kwani elimu wanayotoa inaubora na viwango vya kimataifa pia inazingatia elimu bora ,maadili, Ulinzi na usalama amesema haya kwenye mahafari ya tatu kwa wanafunzi wa Awali na mahafari ya pili kwa darasa la saba shule ya St Marks.
Habari na Ally Thabit.
Monday, 5 August 2024
ASKOFU FROLIANI KATINZI AWAPA NENO WAZAZI
Askofu Froliani Katunzi Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za St Marks,St Methinks,Ujenzi,Victoria na Magnet anawataka wazazi na walezi watanzania na wasio watanzania wawapeleke watoto wao kwenye shule hizi kwani bei ni nafuu ,ulinzi na usalama unazingatiwa kwa kiasi kikubwa kwa watoto .
Mabweni kwaajili ya kulala watoto yapo ya kutosha, katika elimu inayotolewa kwenye shule hizi ni kiwango cha kimataifa ambako mtoto akiitimu anauwezo wa kujiali na kuajiliwa .Askofu Katunzi amesema shule zao zina miundombinu rafiki na wezeshi kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu pia ina wataalam wa rugha za alama kwa wenye uziwi na uono afifu.
Mwenyekiti wa bodi Askofu Katunzi amesema katika kumuunga mkono rais dkt Samia elimu wanazozitoa kwenye shule zao kuanzia elimu ya Awali,Msingi na Secondary wanamafunzo ya vitendo na wana kompyuta zipatazo Mia nne kwaajili ya kufundishia wanafunzi kwa njia ya kidigitali .
Swala la Elimu Bora ,Maadili ,Malezi na Usalama na Ulinzi kwa Watoto pamoja na nidhamu katika shule zao ndio falsafa yao kwa siku zote.ametoa wito kwa nawafunzi watakao maliza darasa la ssaba wawe na nidhamu njema pindi watakapoenda makwao na amewataka wazazi na walezi ifikapo tarehe 19/9/2024 wawalete kwenye shule hizi ili wapate kusoma preform one wapate elimu bora kwa gharama nafuu.
Amesema haya kwenye mahafari ya tatu kwa wanafunzi wa elimu ya awali shule ya St Marks na mahafari ya pili kwa darasa la saba shule ya St Marks wilayani mkuranga mkoa pwani eneo la mwandege.
Habari picha na Victoria Stanslaus.





