Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dawasa Mkama Bwile amesema moja ya mipango mikakati yao ni kudhibiti uvujqji wa maji kutoka asilimia 40% mpaka ifike asilimia 30% ingawaje inatakiwa upoteaji wa maji iwe asilimia 20%.
Mkama Bwile amesma dawasa inadai kiasi cha fedha bilioni 40 kutoka kwenye taasisi mbalimbali na watu binausi ivyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake wanampango wa kukusanya kiasi kikubwa cha madeni haya ili dawasa iweze kujitegemea na kutatuwa changamoto zilizopo ndani ya dawasa.
Mkama Bwile ameongeza kwa kusema dawasa itafunga dira za maji pamoja na mita za kisasa amewaakikishia waariri wa vyombo vya habari na wanahabari dawasa itakuza na kuhimarisha ushirikiano kati yao ,kwani dawasa inaamini kuwa wanahabari pamoja na waariri wa vyombo vya habari ni daraja kubwa na kiungo muhimu kati ya dawasa na wananchi katika kufikisha taarifa kwa wananchi wote.
Amesema haya kwenye semina kati ya dawasa pamoja na wanahabari na waariri wa vyombo vya habari semina hii imefanyika jijini dar es salaam ukumbi wa mwalimu nyerere.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment