Hamza Chilo Naibu Waziri Wizara ya Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa rais anawataka watanzania wote nchini na wasio watanzania watunze mazingira kwa kupanda miti,kutokata miti,kutunza vyanzo vya maji Lengo kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Pia anawapongeza Umoja wa mbio za pole wa Vingunguti (VIJOVI) kwa kuunga mkono serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti eneo la vingunguti kama inavyoonekana pichani naibu waziri akipanda mti wa aina ya mpera kwenye hospitali ya kata vingunguti akiwa amesmbatana na mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na mstahiki mea Kumbila Moto pamoja na viongozi wa VIJOVI.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment