Askofu Froliani Katunzi Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za St Marks,St Methinks,Ujenzi,Victoria na Magnet anawataka wazazi na walezi watanzania na wasio watanzania wawapeleke watoto wao kwenye shule hizi kwani bei ni nafuu ,ulinzi na usalama unazingatiwa kwa kiasi kikubwa kwa watoto .
Mabweni kwaajili ya kulala watoto yapo ya kutosha, katika elimu inayotolewa kwenye shule hizi ni kiwango cha kimataifa ambako mtoto akiitimu anauwezo wa kujiali na kuajiliwa .Askofu Katunzi amesema shule zao zina miundombinu rafiki na wezeshi kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu pia ina wataalam wa rugha za alama kwa wenye uziwi na uono afifu.
Mwenyekiti wa bodi Askofu Katunzi amesema katika kumuunga mkono rais dkt Samia elimu wanazozitoa kwenye shule zao kuanzia elimu ya Awali,Msingi na Secondary wanamafunzo ya vitendo na wana kompyuta zipatazo Mia nne kwaajili ya kufundishia wanafunzi kwa njia ya kidigitali .
Swala la Elimu Bora ,Maadili ,Malezi na Usalama na Ulinzi kwa Watoto pamoja na nidhamu katika shule zao ndio falsafa yao kwa siku zote.ametoa wito kwa nawafunzi watakao maliza darasa la ssaba wawe na nidhamu njema pindi watakapoenda makwao na amewataka wazazi na walezi ifikapo tarehe 19/9/2024 wawalete kwenye shule hizi ili wapate kusoma preform one wapate elimu bora kwa gharama nafuu.
Amesema haya kwenye mahafari ya tatu kwa wanafunzi wa elimu ya awali shule ya St Marks na mahafari ya pili kwa darasa la saba shule ya St Marks wilayani mkuranga mkoa pwani eneo la mwandege.
Habari picha na Victoria Stanslaus.
No comments:
Post a Comment