Wednesday, 7 August 2024

WANAHABARI WAWAPONGEZA DAWASA


 Mwanahabari Mkongwe wa Tbc Anuali Mkama amesema kitendo cha Dawasa kukutana na wanahabari pamoja na waariri wa habari ni muhimu kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto za ujujaji wa maji ambako zaidi ya asilimia 40% maji ya dawasa yanapotea kwa kuvuja .

Hivyo kupitia wanahabari na waariri wa vyombo vya  habari watatumia vyombo vyao vya habari katika kuelimisha jamii  kutoa taarifa ya uvujaji wa maji ya dawasa na changamoto zingine zinazowakabili wateja wa dawasa.

Mwanahabari Anuali Mkama amesema semina hii imekuwa kiunganishi kati ya dawasa ,waariri wa vyombo vya habari na wanahabari amesema haya kwenye semina kati ya dawasa ,waariri wa vyombo vya habari na wanahabari jijini dar es salaam  ukumbi wa mwalimu nyerere.

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment