Sunday, 11 August 2024

MKURUGENZI WA BUDEO ATOA KILIO KWA WADAU WA MAZINGIRA


 Khamsini  ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Budeo inayoshuhurikia utunzaji wa mazingira amempongeza na kumshukuru rais dkt Samia,waziri mkuu Kasimu Majaliwa na Makamu wa rais kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia . 

 kwani watu wakiwa na matumizi ya nishati safi ya kupikia tanzania itaondokana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji wa miti oviyo ndio maana taasisi ya Budeo inaamasisha wanafunzi kupanda miti,ujenzi wa vizimba vya taka na namna ya kutenganisha taka kwenye madampo yetu.

Wamepanda miti elfu  nne na mia mbili 4200 katika shule 11 zilizopo wilaya ya Ilala jijini dar es salaam  na tarehe 30 mwezi 8 2024 wanaenda kufanya uzinduzi wa kizimba cha taka kwenye shule ya secondary ya Zanaki.

Ametoa wito kwa jamii,wadau,makampuni na serikali kuisaidia taasisi ya Budeo kifedha ili waweze kufanya kazi vizuri amema haya kwenye zoezi la upandaji miti eneo la vingunguti wilaya ya Ilala jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment