Teresio Cosmas Mzerere wa Afritanza Attorneys ameipongeza Thrdc kwa kuwakutanisha Watetezi wa haki za Watoto na Wadau kwaajili ya kuwapa mafunzo juu ya sheria ,Sera,Miongozo Kanuni na Miongozo namna ya kutetea na kulinda haki za watoto amesema mafunzo haya ambao yamejumuisha watetezi wa haki za watoto kutoka mikoa ya Dar es salaam,Tanga,Dodoma, na mikoa mingine ya tanzania . Kwani itasaidia kudhibiti na kuzuia ukatili dhidi ya watoto mfano utekwaji wa watoto,ubakwaji kwa watoto na vitendo vya ulawiti dhidi ya watoto.
Ametoa wito kwa washiriki wenzake kutumia mafunzo haya katika kutokomeza vitendo viovu dhidi ya watoto amesema haya kwenye mafunzo ya siku mbili yalioratibiwa Thrdc yaliofanyika kwenye Shule ya Sheria jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment