Mratibu na Muandaaji wa Kongamo Lililowaunganisha Wasanii na Taasisi mbalimbali Ebehard Oswad amesema lengo la kuandaa kongamano la Sanaa Pesa ni kuwatafutoa masoko wasanii na kuwaunganisha na fursa mbalimbali
Wakiwemo Wenye Mabank ili waweze kutambulika na kupata mikopo na kampuni za bima kwani wasanii wengi nchini tanzania awajajiunga na bima za afya ambako usababisha kuwa ombaomba pindi wanapokuwa wanaumwa au kupata ajari .
Nae kwa upande wake Steve Nyerere amewataka wasanii wenzake kutokubali kudharirishwa pindi wanapofanya matamasha kwani sikuhizi kuna mtindo wa waandanji wa matamasha wanatangaza kiingilio bia kwaajili ya kwenda kuona tamasha la msanii na badala yake wawe na bei elekezi.
Kwaupande wake Naibu Waziri wa Sanaa,Michezo na Utamaduni Amiss Mwijuma amempongeza muandaaji wa Sanaa Pesa EBEHARD OSWAD kwa kuweka mipango mikakati kwa lengo la kuwakwamuwa wasanii kiuchumi.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment