Sunday, 11 August 2024

MKURUGENZI WA BUDEO ATOA KILIO KWA WADAU WA MAZINGIRA


 Khamsini  ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Budeo inayoshuhurikia utunzaji wa mazingira amempongeza na kumshukuru rais dkt Samia,waziri mkuu Kasimu Majaliwa na Makamu wa rais kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia . 

 kwani watu wakiwa na matumizi ya nishati safi ya kupikia tanzania itaondokana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji wa miti oviyo ndio maana taasisi ya Budeo inaamasisha wanafunzi kupanda miti,ujenzi wa vizimba vya taka na namna ya kutenganisha taka kwenye madampo yetu.

Wamepanda miti elfu  nne na mia mbili 4200 katika shule 11 zilizopo wilaya ya Ilala jijini dar es salaam  na tarehe 30 mwezi 8 2024 wanaenda kufanya uzinduzi wa kizimba cha taka kwenye shule ya secondary ya Zanaki.

Ametoa wito kwa jamii,wadau,makampuni na serikali kuisaidia taasisi ya Budeo kifedha ili waweze kufanya kazi vizuri amema haya kwenye zoezi la upandaji miti eneo la vingunguti wilaya ya Ilala jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

VIJOVI WAJA KIVINGINE KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 

Katibu wa Mbio za Pole Kata ya Vingunguti (VIJOVI) amesema wameamuwa kupanda miti lengo kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,Amempongeza Naibu Waziri wa  Wizara ya Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa rais kwa kushirikiana  nae katika upandaji wa miti kata ya vingunguti na kukimbia nae pamoja kwenye mbio za pole.

Ametoa wito kwa wanasiasa kutowatumia wakimbiaji wa mbio za pole kipindi cha uchaguzi na badala yake ni vyema wawatumie  na kushirikiana  nao muda wote amesema haya eneo la vingunguti  wilaya ya Ilala jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

BALOZI WA MAZINGIRA ABAINISHA MIKAKATI MIZITO YA KUKABILIANA NA MABADIRIKO YA TABIA YA NCHI


 Grit Godfrey Mwimanzi  Balozi wa Mazingira kutoka Wizara ya Mazingira chini ya Ofisi ya makamu wa rais  ,Katika kukabiliana na madiliko ya tabia ya nchi serikali imeweka sera,sheria,kanuni,taratibu na miongozo .Pia serikali inatoa elimu kwa jamii na mashuleni ya namna ya kupanda miti na kuitunza. 

Akiwa balozi wa mazingira anafanya kazi kubwa ya kuamasisha kupanda miti na kupiga vita matumizi ya nishati chafu ya kupikia ambako wanawake laki tatu hufariki kila mwaka kwa matumizi ya nishati chafu ya kupikia na watu zaidi ya asilimia 80% nchini tanzania wanatumia nishati chafu ya kupikia .

Yeye ni balozi wa mazingira anaunga mkono juhudi na jitihada za rais dkt Samia ifikapo mwaka 2030 watanzania asilimia 80% waondokane na matumizi ya nishati chafu ya kupikia yaani wasitumie kuni na mkaa amesema haya kwenye zoezi la upandaji miti kwenye hospitali ya kata ya vingunguti wilaya ya Ilala jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

NAIBU WAZIRI WA MAZINGIRA OFISI YA MAKAMU WA RAIS AIMIZA WATANZANIA KUTUNZA MAZINGIRA


 Hamza Chilo Naibu Waziri Wizara ya Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa rais anawataka watanzania wote nchini na wasio watanzania watunze mazingira kwa kupanda miti,kutokata miti,kutunza vyanzo vya maji Lengo kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Pia anawapongeza Umoja wa mbio za pole wa Vingunguti (VIJOVI) kwa kuunga mkono serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti eneo la vingunguti kama inavyoonekana pichani naibu waziri akipanda mti wa aina ya mpera kwenye hospitali ya kata vingunguti akiwa amesmbatana na mkuu wa wilaya ya Ilala Edward  Mpogolo na mstahiki mea Kumbila  Moto pamoja na viongozi wa VIJOVI.

Habari picha na Ally Thabit 


Saturday, 10 August 2024

MKUU WA SHULE YA UJENZI AAIDI MAKUBWA KWA WAZAZI NA MALEZI


 Mkuu wa Shule ya Ujenzi amesma Wataendelea Kutoa Elimu bora kwa wanafunzi kuanzia elimu ya Awali ,Msingi na Secondary .Swala la nidhamu na maadili pamoja na ulinzi na usalama kwa wanafunzi kwenye shule ya ujenzi ndio kipaumbele Chao.

Amesema shule ya ujenzi katika mitihani ya taifa kuanzia Msingi na Secondary wanafanya vizuri kila mwaka hivyo anawataka wazazi na walezi wawafikishe watoto wao kwenye shule  ya Ujenzi iliyopo wilaya ya mkoa wa pwani eneo la mkuranga mjini.

Amesisitiza kuwa shule ya ujenzi inazingatia ulinzi na usalama kwa wanafunzi wote pia inatoa elimu bila kujali dini,rangi,kabila na hitikadi yoyote shule ya ujenzi inatoa elimu kwa gharama nafuu tena mzazi au mlezi analipa kwa awamu nne amesema haya kwenye mahafari ya elimu ya Awali na darasa la saba .

Habari picha na Ally Thabit 

DR TINDWA AUPONGEZA UONGOZI WA SHULE YA UJENZI

Mgeni Rasimi Kwenye Mahafari ya ya Wanafunzi wa elimu ya Awali na shule ya msingi kwenye shule ya Ujenzi iliopo wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani eneo la Mkuranga Mjini Dr Tindwa amewapongeza Walimu,Wafanya kazi na Viongozi wa shule hii kwa ka'i kubwa na mzuri wanayoifanya ya kufundisha watoto kwani shule ya Ujenzi  inaufahuru mzuri kuanzia shule ya Awali ,Msingi na Secondary .

Pia inawaandaa watoto ili waweze kujiajili na kujitegemea kimaisha pindi wanapomaliza shule  amesema swala la shule ya ujenzi kuwasomesha bule watoto wasiojiweza ni jambo jema na zuri, ametoa wito kwa wazazi na walezi wawapeleke watoto wao shule ya ujenzi kwani watapata elimu bora,Malezi,watafundishwa maadili mema,nidhamu na pamoja na namna ya kumjua mungu.

Mgeni rasimi Dr Tindwa amesema ada ya shule ya ujeni ni nafuu amesema haya kwenye mahafari ya wanafunzi wa elimu ya Awali na Darasa la saba .

Habari na Ally Thabit 

Wednesday, 7 August 2024

DIWANI WA MWANDEGE ATOA NENO SHULE YA ST.MARKS

Diwani wa Kata ya Mwandege Osmani amewapongeza walimu na viongozi wa shule ya St.Marks kwa kutoa elimu bora na yenye ushindani hivyo amewataka wazazi na walezi wawapeleke watoto wao kwenye shule ya St Marks  kwani bei zao ni nafuu,elimu wanatoitoa inaubora na ushindani.

Swala la ulinzi na usalama kwa watoto ni mkubwa na umeimarika pia wawapeleke katika shule ya Ujenzi iliopo mkuranga mjini pamoja na shule ya St Marks iliopo kata ya  mwandege mkoa wa pwani au piga simu 0789 131388 kwa amesema haya kwenye mahafari ya tatu kwa elimu ya awali na mahafari ya pili ya darasa la saba .

Habari na Ally Thabit