Friday, 7 February 2025
MASHUJAA WA SARATANI PAMOJA NA WADAU WANAOPIGA VITA SARATANI ZA AINA ZOTE WAPO KWENYE MATEMBEZI
FAITH GUGU MKUU WA GSM FOUNDATION AAHIDI MAKUBWA KWENYE HOSPITALI YA OCEANROAD CENCER INSTITUTE
Mkurugenzi Mkuu wa GSM FOUNDATION Faith Gugu amesema wataendelea kushirikiana na hospital ya Ocean road Cancer Institute katika mapambano ya saratani za aina zote lengo kutokomeza au kupunguza uogonjwa wa saratani na vifo vinavyotokana na saratani za aina zote kwani GSM FOUNDATION inatoa elimu kwa jamii ya kujilinda dhidi ya magonjwa ya saratani. Elimu hii inawafikia watu wenye ulemavu wa aina zote.
Amesema haya kwenye kilele cha maazimisho ya saratani yalio fanyika kwenye Hospitali ya Ocean road cancer Institute ambako uazimishwa kila tarehe 4 ya mwezi wa 2 duniani kote kila mwaka .
Habari na Ally Thabit
GLORIA KIDA MKURUGENZI WA ASASI YA SHUJAA WA SARATANI AIMIZA WATU KUPIMA SARATANI
Mkurugenzi wa Asasi ya Shujaa wa Saratani Gloria Kida anawataka watu kujitokeza kwa wingi kupima saratani za aina zote Pia anawahimiza wanajamii kuchanja chanjo ya HPV wao na watoto wao kwani ni kinga dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi .
Asasi yao Imetoa Elimu ya Saratani Katika Mkoa wa Mwanza na Wilaya zote za Dar es salaam amesema haya kwenye kilele cha week ya saratani iliyo fanyika kwenye Hospitali ya Oceanroad Cancer Institute ambako kila mwaka uazimishwa tarehe 4 ya mwezi 2 duniani kote .
Habari na Ally Thabit.
ASCP MULIRO J. AELEZEA WATOTO WALIOJITEKA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Limewapata na Kuwahoji wasichana wawili ambao ambapo mmoja wa miaka16 Mwanafunzi wa kidato cha pili na mwingine wa miaka 12 Mwanafunzi wa Darasa la saba wakazi wa vijibweni kigamboni kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na watekwaji wanataka pesa.
Ufuatiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubainiwatoto hawa walipokuwa na baada ya mahojiano ya kina walikiri kutengeneza tukio hili la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka tarehe 26/01/2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi tarehe 27/01/2025 asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipo kamatwa wakiwa wanazunguka. Jeshi linalaani vitendo vya hivi vya watu wenye lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda ya Maalum Dar es salaam katika kipindi cha Desemba hadi Januari 2025 katika kusimamia mifumo ya haki jinai mahakamani baadhi ya watuhumiwa mbalimbali walipatikana na hatia ikiwa ni pamoja na Idrisa Rasshid miaka [35] Mkazi wa Kwembe Kimara alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Paul Elisha miaka (37) mkazi wa Mbezi Beach kwe nye Mahakama ya Kinondoni alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka na Jackson Mgeta (34) mkazi wa Kawe alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Jeshi la Polisi lina wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana ili kuimarisha mifumo ya ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kutekeleza falsafa ya ulinzi shirikishi ili kuzuia vitendo vya kihalifu. Imetolewa na Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam.
Habari na Ally Thabit Mbungo.
Monday, 25 November 2024
NMB BANK NA TAASISI YA TSA WASHILIKIANA KUWAFUNZA WAJISIRIAMALI
Kwaupande wake mtndaji mkuu wa Taasisi ya TSA ZAHORO PAULO MAKANGA amesema wameamua kuingia makubaliano na Bank ya NMB kwa ajili ya kuboresha na kukuza mifumo ya wabunifu na wajasilia mali kwani wajasiriamali watatengenezewa mazingira lafiki ya kuu na kutangaza bidhaa zao,
Taasii ya TSA na Bank ya NMB watawapa wajasiriamali na wabunifu elimu ya utunzaji fedha na usimamizi wa mitaji yao ya biashara TSA na NMB bank wataandaa program mbalimbali kwa wajasiriamali na wabunifu namna ya kukuza na kuimalisha biashara na uchumi wao,
ZAHORO PAULO amesema pia kutakuwa na mashindano kwani kutaleta chachu kwa wajasiriamali na wabunifu katika matumizi ya mtandao huku akiipongeza serikali kwa kuandaa sera ambayo itasaidia kukuza na kulasimisha wajasiriamali na wabunifu, Nchi zingine zinapata kiasi kikubwa cha fedha. amesema haya makao makuu ya NMB wakatika wakiingia makubaliano na Bank hiyo.
Habari Picha na Ally Thabiti.
CHADEMA WAISUTA SERIKALI
Mwenyekiti wa chama cha CHAEMA Mbowe na katibu mkuu John Mnyika wamekanusha na kukana waziwazi kuwa awajawahi kukubaliana na serikali juu ya TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa, Vitongoji na Vijiji na badala yake walitaka tume huruma ya uchaguzi ndiyo isimamie.
Habari na Ally Thabiti
MKUU WA CHUO KIKUU HURIA HAMIZA NDOTO ZA MWALIMU NYERERE KUKAMILIKA
Waziri Mkuu Mstaafu mizengo pinda na mkuu wa chuo huria amesema katika kuhazimisha miaka 30 ya chuo kikuu huria waweza kukamilisha na kufanikisha ndoto za mwalimu Nyerere kwa kutoa elimu yenye ujuzi.
Habari na Ally Thabiti
