Tuesday, 11 March 2025

TAASISI YA BI AISHA SURURU YAAHIDI MAKUBWA KWA VIJANA


 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya BI Aisha Sururu amesema wataendelea kuwawahifadhisha Quran vijana wote wa kitanzania na wasio watanzania lengo wamtambue mungu na wawe wenye maadili mama. 

BI Aisha Sururu ametoa wito kwa watanzania na wasio watanzania kutoa michango yao ya fedha na Mali ili taasisi yake ijenge madarasa na mabweni eneo la kiparang'anda mkoa wa pwani kiasi kinachoitajika ni zaidi ya bilioni mia nne.
Amesema haya jijini dar es salaam  kwenye mashindano  ya kuhifadhi Quran. 

Habari picha na Victoria Stanslaus 

Monday, 10 March 2025

AMANA BENK YAAIDI MAZITO


 Mkurugenzi wa Amana Benk Abubakari amesema watazidi kudhamini na kufadhiri mashindano ya Quran lengo kuwatia moyo wanaohifadhi na kusoma Quran  na kukikuza kitabu cha mungu amesema haya kwenye mashindano ya 25 ya kuifadhi Quran  yalioandaliwa na taasisi ya Bi Aisha Sururu foundation ambayo yamefany8ka jijini dar es salaam. 

Habari picha na Victoria Stanslaus 

BI ASHA DIWANI VITI MAALUM JIJI LA ILALA AIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUWAPELEKA WATOTO WAO KUSOMA QURAN


 Diwani wa Viti Maalum  na Mweka hazina kwenye taasisi ya Aisha Sururu Foundation anawataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kusoma Quran  kwani kuna faida zinapatikana  zikiwemo kuwa na imani,kuulumia binadamu mwenzako,kuwana ofu na kuwa mwadilifu na weredi katika kazi na jamii kwa ujumla .

Habari picha na Victoria Stanslaus

MJUMBE WA ALMASHAURI KUU YA CCM APONGEZA MASHINDANO YA QURAN

 

Amoll Abudi Juma Mjumbe wa Almashauri Kuu ya ccm taifa mkoa wa dar es salaam  amempongeza bi Aisha Sururu kwa kuendesha mashindano ya quran kwa miaka ishilini na tano pamoja na kuwahifazisha maneno ya mungu watoto yatima,wajane,wasiojiweza,watu wa makundi maalum kwani kufanya hivi kunasaidia kupata watu wenye maadili,wenye ofu ya mungu na hatimae nchi ya tanzania inapata amani ,upendo na utulivu.

Habari picha na Victoria Stanslaus 

SHEIKH PONDA AELEZA UMUHIMU WA FUNGA

 Sheikh Issa Ponda  amewataka Waislamu wote wale ambao awana matatizo ya kiafya waweze kutekeleza nguzo ya nne ya kiislam kati ya tano wafunge ramadhani ndani ya mwezi huu wa ramadhani kwani watakuwa waja wema  pia wasome Quran mara kwa mara.

Habari na  Victoria Stanslaus 

SHEIKH CHIZENGA AELEZA FAIDA ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

 Katibu Mkuu  wa Baraza Kuu la Ulamaa Bakwata amewataka waislamu nchini tanzania wafunge ramadhani kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhani kwani miongoni mwa faida watakazozipata ni kuimarika kwa afya zao .Pia mungu atawasamehe makosa yao na zambi zao pia anawasisitiza watanzania wote bila jujali dini,kabila,rangi na jinsia wazidi kumuombea afya njema rais Dr Samia  kwani amekalisha miradi yote na anatenda haki kwa kila mmoja hivyo ni vyema kumchagua kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu hakika mama samia mitano tena.

Habari picha na Ally Thabit. 

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI AWATOA OFU WATANZANIA















Eng. Felchesmi J.Mramba  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati amewatoa ofu watanzania  kuhusu uhamuzi uliofanywa na serikali yetu ya tanzania kwa kununua umeme megawati mia moja kutika nchi ya Ethiopia .

Kwani Umeme huu unanunuliwa kwa gharama ndogo  kwani umeme utasaidia mikoa ya kaskazini kupata umeme wa uhakika  kwenye viwanda na  maeneo wanayoishi wananchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi J. Mramba amesema tanzania itapata umeme huu kupitia kutoka Ethiopia kwa kutumia miundombinu ya Kenya kwani Kenya na Ethiopia zipo karibu . Serikali ya tanzania imefanya uhamuzi huu kwa sababu tunapoteza megawati kumi na saba za umeme kwa kutumia kupitisha umeme kwa njia za ndani ya nchi yetu Pia sera zetu zinaruhusu kununua umeme nchi za nje .

Mfano Mkoa wa Rukwa umeme unaotumika ni kutoka nchi ya Zambia ,Umeme unaotumika  mkoa wa Kagera unatoka nchi ya Uganda hata nchi ya Ethiopia amnayo inatuuzia tanzania  umeme licha ina megawati elfu sita lakini bado inanunua umeme nchi zinginezo na mpaka sasa nchi zipatazo tatu zimeleta maombi za kuuziwa umeme na tanzania  na wamekubaliana na wapo hatua za mwisho nchi hizi ni Burundi,Rwanda na Zambia .

Na sasa Tanzania kwa Kushirikiana na Zambia wanatekeleza mradi wa Taza ambao megawati sita za umeme zitauzwa nchini Zambia na mradi umefikia asilimia hamsini .Nakampu  ya Mifodi ya Zambia itanunua megawati mia moja tanzania  nchi zinginezo  zitazonunu umeme tanzania Msumbiji,Marawi,Dr kongo

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa bei tunayouziwa umeme na nchi ya Ethiopia  ni bei na fuu na rafiki kwani ni dora saba nukta saba sent .

Swala la Bwawa la Mwalimu Nyerere limeleta ukombozi katika kupatikana umeme wa kutosha nchini tanzania hivyo watanzania tuunge mkono uwamuzi uliofanywa na serikali yetu ya tanzania na tuendelee kumpongeza rais Dr Samia kwa kukamilisha bwawa la mwalimu nyerere na miradi mingineyo mpaka kuwezesha nchi kuondokana na tatizo la kukatikakatika umeme mara kwa mara.

Habari picha na Victoria Stanslaus