Monday, 5 August 2024

WATU WAIMIZWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE YA ST. MARKS


 Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Shule ya St. Marks Peter Tadeo amesema shule ya St Marks inafundisha watoto vizuri na inazingatia mahadili mema kwa wanafunzi na inapokea wanafunzi wa dini zote  kwa bei nafuu kuanzia elimu ya Awali ,Msingi na Secondary .

Tarehe16 / 9/2024 shule ya marks  inapokea wanafunzi wa PRIFORM ONE kwa ada  ya shilingi za kitanzania laki mbili na ishirini,shule ya St Marks ina mabweni kwaajili ya wanafunzi vilevile shule ya St Marks inapokea wanafunzi wanao amia amesema haya kwenye mahafari ya elimu ya awali ambako huu ni mwaka wa tatu na mahafari ya darasa la saba ambako huu ni mwaka wa pili .

Shule ya St Marks inapatikana Wilayani Mkuranga mkoa wa pwani eneo la mwandege .

Habari picha na Ally Thabit 

 

WILAYA YA KIBAHA YAIMARISHA ULINZI KWA WATU WENYE UALBINO

 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Niksoni Saimoni amesema katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa watu wenye Ualbino  Wilaya ya kibaha inatoa elimu kwa jamii ya namna ya kuwalinda watu hawa .Pia mkuu wa wilaya ya kibaha  amempongeza rais dkt Samia kwa kuweza kujenga barabara wilayani kibaha kwani imekuwa kichocheo kikubwa kwa kukuwa kwa uchumi wa mtu mmojammoja na kibaha  yenyewe.

Ujenzi wa madarasa rais dkt Samia amejenga madarasa kuanzia elimu ya Awali,Msingi na Secondary ambako imewezesha wanafunzi kutokwenda kusoma umbali mrefu na upatikanaji wa maji safi na sarama ..amesema haya jijini Dsm  wilayani ubungo kwenye kongamano la Sanaa pesa lililowakutanisha wasanii mbalimbali.

Habari picha na Ally Thabit 

EBEHARD OSWAD AWATAFUTIA FURSA WASANII


 Mratibu na Muandaaji wa Kongamo Lililowaunganisha Wasanii na Taasisi mbalimbali Ebehard Oswad amesema lengo la kuandaa kongamano la Sanaa Pesa ni kuwatafutoa masoko wasanii na kuwaunganisha na fursa mbalimbali 

 Wakiwemo Wenye Mabank ili waweze kutambulika na kupata mikopo na kampuni za bima kwani wasanii wengi nchini tanzania awajajiunga na bima za afya ambako usababisha kuwa ombaomba pindi wanapokuwa wanaumwa au kupata ajari .

Nae kwa upande wake Steve  Nyerere amewataka wasanii wenzake kutokubali kudharirishwa pindi wanapofanya matamasha kwani sikuhizi kuna mtindo wa waandanji wa matamasha wanatangaza kiingilio bia kwaajili ya kwenda kuona tamasha la msanii na badala yake wawe na bei elekezi.

Kwaupande wake Naibu Waziri wa Sanaa,Michezo na Utamaduni Amiss Mwijuma amempongeza muandaaji wa Sanaa Pesa EBEHARD OSWAD kwa kuweka mipango mikakati  kwa lengo la kuwakwamuwa wasanii kiuchumi.

Habari picha na Ally Thabit 

Thursday, 1 August 2024

WATETEZI WA HAKI ZA WATOTO WAIBUA MAMBO MAZITO

 

Mama Gradnes Mtetezi wa haki za Watoto amebainisha mambo yanayosabasha watoto kufanyiwa ukatili .Ugumu wa maisha
 unaofanya wazazi kushindwa kufuatilia watoto wao,Uchu wa maharakani kwani watu wanaamini kufa kupeleka kiungo cha mtoto kutapelekea yeye kukaa madarani miaka mitano 5 ,Waganga wa kienyeji ambao wanapiga ramli chonganishi, tamaa ya kutaka Mali nyingi na utajili , kuwatelekeza watoto kwani wazazi wengi na walezi wamewatelekeza watoto wao na watoto kujiteka wenyewe.

Mama Gradnes ametoa rai kwa wanaharakati kutoa elimu ya mara kwa mara kwa jamii lengo jamii itambue wajibu wa kulinda na kutetea watoto amesema haya kwenye mafunzo  ya siku mbili yalioanza tarehe 31 /7/2024  na kumalizika  tarehe 1/8/2024 yalio andaliwa na THRDC  ambayo yamejumuishwa na watetezi wa haki za watoto lengo watetezi wakatoe elimu na kupaza sauti juu ya haki za watoto amesema haya jijijini dar es salaam  wilaya ya Ubungo kwenye Shule ya  sheria .

Habari picha na Victoria  Stanslaus

DR FRANCIS MAGARE AWAPONGEZA THRDC

 

Mkurungezi Mkuu Mtendaji  wa Taasisi ya East Africa and Human Rights Institute amesema Thrdc wamefanya jambo zuri na jema katika kuweka nguvu za pamoja juu ya kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto .

Pia amewataka watetezi wa haki za watoto kutumia vyema mafunzo yalioanza tarehe 31 /7/2024 na kumalizika tarehe 1/8/2024 wayatumie vizuri katika kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na ukandamizwaji wa haki za watoto.

Mafunzo haya yamejumuishwa watetezi  wa haki za watoto tanzania nzima  ambako yamefanyika jijini dar es salaam  wilaya ya ubungo kwenye shule ya sheria.

Habari picha na  Victoria Stanslaus

WATETEZI WA HAKI ZA WATOTO WAIPONGEZA THRDC


 Teresio Cosmas Mzerere wa  Afritanza Attorneys  ameipongeza Thrdc  kwa kuwakutanisha Watetezi wa haki za Watoto na Wadau kwaajili ya kuwapa mafunzo juu ya sheria ,Sera,Miongozo Kanuni na Miongozo namna ya kutetea na kulinda haki za watoto amesema mafunzo haya ambao yamejumuisha watetezi wa haki za watoto kutoka mikoa ya Dar es salaam,Tanga,Dodoma, na mikoa mingine ya tanzania  . Kwani itasaidia kudhibiti na kuzuia  ukatili dhidi ya watoto mfano utekwaji wa watoto,ubakwaji kwa watoto na vitendo vya ulawiti dhidi ya watoto.

Ametoa wito kwa washiriki wenzake kutumia mafunzo haya katika kutokomeza vitendo viovu dhidi ya watoto amesema haya kwenye mafunzo ya siku mbili yalioratibiwa Thrdc yaliofanyika kwenye Shule ya Sheria jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

 OLENGURUMWA AWAHASA WATETEZI WA HAKI ZA WATOTO KUWA MSATARI WA MBELE KUKEMEA UKATILI 


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (TRDC), kwa kushirikiana na wadau wanaendesha mafunzo kwa Watetezi wa haki za Watoto kutoka mikoa mbalimbali nchini.


Simina hiyo ya siku mbili inalenga kuwajengea uwezo Watetezi hao kwenye masuala mbalimbali ikiwemo ya kisera na kisheria, wanavyoweza kuyaoanisha kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya utetezi kwenye ngazi mbalimbali.


Akizungumza leo Julai 31, 2024 katika semina hiyo , Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema kuwa Watetezi wa haki za Watoto wanayo nafasi ya kubwa ya kusaidia katika jitihada za kukabiliana na matukio mbalimbali ya ukatili kwa watoto, hususani kipindi hiki ambacho kuwepo na matukio ya utekaji na vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto.


"Tunafahamu hali ya ulinzi wa Mtoto Nchi hii imekuwa na changamoto nyingi sana Ripoti ya Jeshi la Polisi juzi ilionesha utekaji umekuwa mkubwa, kwa mfano mwaka jana tu watoto zaidi ya 73 kwa mujibu wa ripoti hiyo, tumeona masuala ya ulawiti na ubakaji yote yamekuwa matatizo makubwa ambayo hawa Watetezi wa haki za binadamu wanapaswa kwenye kukemea, kufuatilia na hata kuwajibisha zile taasisi ambazo zinahusika na ulinzi wa haki za Kiraia."amesema Olengurumwa 


Amesema wana jukumu la kukemea pale wanapoona kuna dalili au vitendo vya ukiukwaji wa haki za Watoto kwa sababu sehemu ya majukumu yao


Aidha Mratibu Kitaifa wa Tanzania Children Rights Forum, Ombeni Kimaro, amesema kuwa uelewa mdogo uliopo katika jamii juu ya masuala yanayohusu haki za Watoto ni sababu inayopelekea vikwazo katika ulinzi wa haki za Watoto.


Amewahasa wazazi ,walezi na jamii kwa ujumla kuwa mfano bora katika kuhakikisha wanasimamia na kulinda haki za Watoto, ambapo amesema kwa upande wao wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa, ikiwemo kushirikiana na Serikali.


Washiriki wa semina hiyo wametokea kwenye Mikoa nane ikiwemo mkaoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Singida, ambapo yatahitimishwa kesho August 2024.

Habari picha na Ally Thabit