Sunday, 30 June 2024

RAIS DR KIKWETE AWAPONGEZA WAANDAAJI WA MSOGA MARATHON


 Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya nne 4 Dr Kikwete anawapongoza waandaaji wa mbio  za Msoga Marathon  kwani ubunifu huu ni mzuri na unatija kubwa kwenye sekta ya Afya ambako fedha zilizopatikana zitawezesha kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo kwa kinamama wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua Na kununua  vifaa vya kuwawezesha watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa kutimia .

Rais Dr Kikwete anawatia moyo waandaaji na kuwataka kutokata tamaa na mbio hizi za Msoga Marathon  ziwe endelevu ma zifanyike kila mwaka ''amempongeza mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete na wenzake kuamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Msoga  Marathon. 

Ametoa wito kwa watu wote wawe namoyo wa kuwasaidia watu wenye uhitaji amesema haya wilayani Chalinze kata ya Msoga kijiji cha Msoga  mkoani pwani  kwenye mbio za Msoga Marathon. 

Habari picha na Ally Thabit 

TOYOTA YAJA NA BIDHAA YA KIBABE MSOGA MARATHON


 Jamal Chembera Meneja Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania LTD amewapongeza waandaaji wa Mbio za Msoga  Marathon kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia kuokoa na kunusuru vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa .Jamal Chembera amesema kampuni ya Toyota inamuunga mkono rais Dr Samia  katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ndio maana kampuni ya Toyota wameamuwa kuja na magari ambayo yanatumia nishati ya umeme .

Ivyo amewataka watanzania na wasio watanzania kununua magari kutoka Toyota  kwani bei ni mafuu,ayachafui mazingira  na ukiitaji unapata kwa muda mfupi .ametoa wito watu wasiogope teknolojia na badala yake waitumie teknolojia kama Toyota walivyoleta magari ya kisasa yanayotumia nishati ya umeme.

Habari picha na Ally Thabit 

ADERA IZENGO AFARIJIKA KUWEPO KWA MSOGA MARATHON


 Mwananchi wa Wilaya ya Chalinze Kata ya Msoga kijiji cha Msoga Mkoa wa Pwani Adera Izengo amesema msoga marathon itawakomboa wanawake wakati wa kujifungua  na itanusuru vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa aijafika .

ametoa rai kwa waandaji wa msoga marathon mbio hizi ziwezinafanyika kila mwaka kwani licha ya kupatikana kwa fedha kwaajili ya ujenzi na kuboresha  hospitali ya Chalinze pamoja na ununuzi wa vifaatiba pia mbio zinasaidia watu kufanya mazoezi ya mwili amemshukuru mhe mbunge na naibu waziri Riziwani Kikwete pamoja na waandaji wa msoga marathon  bila kuwasaau washiriki wote amesema haya wilaya ya  Chalinze  kata ya Msoga kijiji cha Msoga mkoani Pwani.

Habari picha na Ally Thabit 

MBUNGE WA CHALINZE ANUSULU VIFO VYA MAMA NA MTOTO


 Riziwani Kikwete Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri amesema wameamuwa kuleta Msoga Marathon Lengo kupata fedha kwaajili ya kununua vifaa vya kuwaifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya kutimiza miezi tisa (NJITI) .

amewashukuru watu,makampuni,taasisi, viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa kiserikali na wadau mbalimbali kwa kushiriki kwenye Msoga Marathon na kutoa michango yao mbalimbali . Kwani yeye mbunge wa Chalinze ameahidi fedha zilizopatikana zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Na amesisitiza kuwa Msoga Marathon itafanyika kila mwaka amesema haya mkoani Pwani wilaya ya Chalinze kata ya Msoga kijiji cha Msoga  kwenye mbio za Msoga Marathon .

Habari picha na Ally Thabit 

Wednesday, 26 June 2024

RAIS KIKWETE KUNOGESHA MSOGA MARATHON

 Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 wa Tanzania Dr Kikwete amepongeza waandaaji wa Msoga Marathon kwani mbio hizi zinampango wa kukusanya kiasi cha fedha milioni Mia tatu therasini ambako zitaenda kutumika kwenye kununua vifaa kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda na ujenzi wa vyumba vya kujifungulia mamawajawazito haya ni malengo mazuri ndio maana yeye anaunga mkono mbio za msoga marathon kushiriki kwenye mbio hizi na kutoa pesa na anatoa wito kwa taaasisi, makampuni,viwanda na watu binaus kushiriki na kuchangia zoezi hili amesema haya wakati akihojiwa na wasafi TV na redio.

Habari na Ally Thabit 

WAFANYA BIASHARA WAPEWA MATUMAINI

 Mwenyekiti  wa Wafanyabiashara  Martini Mbwana anawataka wafanyabiashara kufungua maduka yao kwani changamoto walizoolozesha kamati ya waziri mkuu baadhi washazifanyia kazi na vikao vinaendelea kati ya kamati ya waziri mkuu na Wafanyabiashara lengo wafanya biashara wasitishe kufunga maduka yao.

Mpaka sasa mikoa ambayo wafanyabiashara wamefunga maduka yao .Arusha,Mbeya,Mwanza,Tanga,Mtwara na dar es salaam.  Mwenyekiti wa wafanyabiashara  Martini Mbwana  amesema hii inaleta athari kwa uchumi wa tanzania na uchumi wa mtu mmojammoja ivyo anatoa rai kwa wafanyabiashara  kufungua maduka yao kwani hata mkuu wa mkoa wa dar es salaam CHALAMILA ameimiza hekima na busara itumike na si kufunga maduka kwani kitendo cha kufunga maduka ni kukiuka maagizo na maelekezo ya waziri mkuu Amesema haya jijini 

Habari na Ally Thabit 

Tuesday, 25 June 2024

PROF LADSLAUS MNYENE ATOASIRI NZITO ELIMU KIDIGITALI


 Mkurugenzi wa  Idara ya Sayansi na Teknolojia Wizara ya Elimu Prof Ladslaus Mnyane  amesema Utoaji elimu kwanjia ya kidigitali kuanzia elimu ya Awali ,msingi ,secondary na vyuo vikuu itasidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufundishwa masomo kwa muda mfupi wakiwa wengi,walimu watafundisha wanafunzi kwa uchache wao,itapunguza gharama kwa serikali kwa kutoajili walimu wengi.

Katika mabadiliko ya kiteknolojia duniani tanzania tukiwafundisha wanafunzi kwa njia za kidigitali itawawezesha wanafunzi baada ya kumaliza shule na vyuo vikuu watakuwa wameshabobea katika matumizi ya kidigitali . Hivyo ufanisi utaongezeka kwa kiasi kikubwa katika utendaji kazi kwenye sekta mbalimbali mfano kwenye sekta ya madini,sekita ya kilimo,sekta za maji na sekta zinginezo.

Prof Ladslaus Mnyane amesema lengo la kutoa elimu kwa njia ya kidigitali kuwezesha watanzania kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ya sasa na ya baadae,pia wanatarajia serikali na watu binaus kutekeleza mpango huu kwa vitendo  ifikapo mwezi7/2025  .Swala la kujumuisha na kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu ili wapate elimu kwa nia ya kidigitali ni jambo muhimu na linatija kwa tanzania amesema haya jijini dar es salaam kwenye mjadala wa kupokea maoni kwa wadau wa elimu  kwa namna gani ya kukamilisha mpango wa kutoa elimu kwa njia ya kidigitali.

Habari picha na Ally Thabit