Tuesday, 24 March 2020

WANASIASA WAIPA TANO TUME YA UCHAGUZI TANZANIA

John Shibuda Mwenyekiti wa Chama cha TADEA na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania kwakuwa wawazi na Kwa kuwashirikisha viongozi wa vyama vya Siasa katika maendeleo ya hatuwa ya uandikishaji wa wapiga Kura kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura John Shibuda ametoa wito Kwa watanzania kujitokeza Kwa wingi tarehe 17 mwezi 4 kwenye maboresho ya pili ya daftari la kudumu la wapiga Kura huku akiwataka wanasiasa kuamasisha watu wajitokeze Kwa wingi mpaka sasa watanzania milioni30 wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura

Habari picha na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment