Friday, 4 September 2020

CHUO KIKUU CHA SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE (SUA) KUIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

 

Mkurugenzi wa shahada za awali SUA, Nyambilila Amuli(kulia) 

Mkurugenzi ndg, Nyambilila ameipongeza sana serikali ya awamu ya tano kwa kuwawezeshea ujenzi wa maabara ya kisasa kabisa. Ujenzi wa maabara hiyo umeleta tija na manufaa makubwa katika kufanya tafiti zao. Pia ameongeza kua tafiti mbalimbali zikiwemo za kilimo,ufugaji na uvuvi ni eneo ambalo wamekua wakijikita zaidi. Hivyo vijana wote nchini ni fursa kwao kujiunga katika chuo chetu(SUA), kwani wataweza kujiajiri wenyewe pindi wamalizapo chuo bila ya kusubiria ajira serikalini.
Chuo kikuu cha SUA ni miongoni mwa vyuo bora kabisa ukanda ya Afrika mashariki na kati kwa kuwandaa wataalamu mbalimbali katika fani za kilimo na ufugaji. Chuo hicho kinajivunia vijana wengi nchini waliotoka chuoni hapo na kufanya mengi makubwa kwenye jamii yetu
Pia chuo cha SUA kimekua kikifanya tafiti mbalimbali kuangalia udongo unaofaa katika kilimo na utafiti wa mbolea sahihi.
Amemaliza kwa kuishukuru sana serikali kuwapatia trekta ambazo zimekua na mchango mkubwa sana. Serikali pia imewezesha kupatikana kwa tawi lingine la chuo hicho lililopo katavi na kua na uwezo wa kudahili vijana wengi zaidi
Kwa vijana wote wenye maono makubwa na kilimo wanakaribishwa sana kujiunga na chuo cha SUA kwani kina ubora mkubwa sana katika sekta hiyo
Habari picha na ally thabiti

No comments:

Post a Comment