Tuesday, 30 July 2024

MKURUGENZI WA TRS AWATOA OFU WATANZANIA


 Mkurugenzi  Mkuu  Mtendaji  wa Shirika la Reli tanzania (TRS) Mwandisi Masanja Kadogosa amesema usafiri wa treni ya umeme (SGR) imezingatia makundi yote wakiwemo watu wenye ulemavu  kwenye vituo vya kupandia treni ya mwendo kasi (SGR) kwani miundombinu ni rafiki na wezeshi na kwenye mabehewa kuna viti mwendo kwaajili ya watu wenye ulemavu wa viungo. Kwa upande wa watu wasioona mlangoni pindi anapoingia kwenye mabehewa mazingira rafiki na wezeshi. 

Mwandisi Masanja Kadogosa amempongeza rais Dr Samia  kwa kutoa fedha kwaajili ya kukamilisha mradi wa SGR anaamini kuwa tarehe 1 /8/2024 uzinduzi wa safari za dar es salaam mpaka Dodoma utasaidia kukuwa kwa uchumi wa tanzania na mtu mmoja mmoja .

Pia amempongeza Waziri wa Usafirishaji na Uchukuzi  Prof Makame Mbarawa kwa kazi kubwa anayoifanya katika kusimaia ujenzi wa SGR pamoja manunuzi ya vichwa vya treni na mabehewa yake . Mwandisi Kadogosa amewataka watanzania kuitumia treni yao ya umeme kwani bei nafuu usafiri wake wa haraka na yeye amewaakikishia watanzania safari zao zitakuwa za uwakika na usalama  amesema haya makao makuu ya trs jijini dar es salaam  wakati akizungumza na wanahabari.

Habari na Ally Thabit 


WAZIRI AIMIZA WATANZANIA KUTUMIA TREN YA MWENDO KASI

 Waziri wa Usafirishaji na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema tarehe 1 mwezi 8 mwaka 2024 rais Dr Samia  atazindua tren ya umeme (SGR) kutoka Dar es salaam  mpaka Dodoma .

Kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi wa reli mpya ya kisasa inayotumia umeme ni dora bilioni 3.18 ambako zaidi ya kilometa 722 na vichwa vya tren 19 na mabehewq kwaajili ya habiria 89 na mabehewa ya mizigo 1430 ambako kiasi cha fedha kilichotumika kununua ni tilioni 1.3.

Waziri wa Uchukuzi  na Usafirishaji  prof Makame Mbarawa amesema Tren hii 


itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuwa kwa sekta mbalimbaloi mfano kilimo,Uvuvi,Biashara na Viwanda . Pia Usafiri huu wa tren ya Umeme unauwezo wa kubeba mizigo tani 10000 kwa pamoja ambako sawa na malori 1000'' Usafiri huu wa Sgr ni wa gharama nafuu ambao kila mtanzania anaweza kutumia.

Hivyo Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji  Prof Makame Mbarawa anawataka watanzania kutumia tren ya umeme kwani ina faida kubwa kwao na kwa uchumi wa tanzania  amesema haya jijini dar es salaam  wakati akizungumza na wanahabari kuhusu uzinduzi wa safari za tren kutoka dar es salaam  mpaka Dodoma1/8/2024 ambako rais Dr Samia ndiye mgeni rasmi.


Thursday, 25 July 2024

WAZIRI WA UJENZI AWAPONGEZA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA)

Inosent  Bashungwa Waziri wa Ujenzi amesema Wakala wa Majengo Nchini Tanzania (TBA) wanatekeleza ujenzi wa miradi kwa vitendo na gharama nafuu . Huku akiwataka watumishi wa serikalini wanapopangishwa  nyumba na wakala wa majengo (TBA) wazilinde na kuzitunza pia walipe kodi kwa wakati.

Waziri Inosent  Bashungwa amewapongeza wakala wa majengo kwa kuweka vitasa janja kwenye nyumba walizo jenga n kuwepo kwa mifumo ya ulipaji wa umeme na maji rafiki na wezeshi amesema haya wakati wa uzinduzi wa nyumba ya ghorofa  yenye uwezo wa kukaa familia 16 na jumla ya gharama zilizotumika kujenga nyumba hii ni bilioni 5 fedha za kitanzania . 

 Na hapa pichani waziri wa ujenzi Inosent  Bashungwa akiwa ameambatana na mkurugenzi mkuu mtendaji wa TBA  Daudi Kandolo huku akiwemo mkui wa mkoa wa da es salaam  na mwenyekiti wa ccm kinondoni . 


Habari picha na Ally Thabit 

MAENDELEO BANK YATOA GAWIO KWA WANAHISA WAKE

 Ndugu waandishi wa Habari,Mtakumbuka  Kwamba Mnmo tarehe 17 Aprill 2024,uongozi wa maendeleo bank uliongea na uma kupitia waandishi wa habari na kutangaza kwamba bank yao ya maendeleo Bank Plc ikiwa ni bank ya kwanza  nchini kuorodhoshwa Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE) wakati wa kuanzishwa kwake  kupitia dirisha la dogo  la EGM, imewekwa historia ya kuwa bank yenye faida kwa miaka 9 mfululizo kuanzia mwaka  wake wa piliwa kuanzishwa kwake  yaani mwaka 2015.

Aidha umma ulitaarifiwa kwamba matokeo ya kifedha ya mwaka 2023 yanaonesha uimara na ukuaji thabiti wa Maendeleo Bank katika soko la mabenki hapa nchini. Katika mwaka huo,bank ilikuza faida kwa 66% baada ya kodi. Ambapofaidabaada ya kodiiliongezeka hadi shilingi za kitanzania bilioni2.3 kutoka shilingi bilioni1.4 mwaka 2022.

Ukuaji huo wa kuvutia  faida ulichangiwa zaidi na mikakati mizuri ambayo bank imejiwekea na inayosimamiwa vyema na uongozi wa bank pamoja na ushirikiano mzuri wa  wateja na wadau mbalimbali. Uongozi wa bank umeainisha baadhi ya vichocheo vya mafanikio haya makubwa ambavyo ni pamoja na 

;1 Ukuajiwa faida baada ya kodi kwa asilimia 66 kutoka shilingi za kutanzania bilioni1.4 mwaka 2022 hadi shilingi bilioni2.3 kwa mwaka 2023.

2. Kuongezeka kwa Amana  za wateja kwa asilimia 15 kutoka shilingi za kitanzania bilioni78.0 mwaka 2022 hadi shilingi za kitanzania  bilioni 90.0  mwaka 2023.

3. Kuimarika kwa ubora wa mikopo kutoka mikopo chechefu ya asilimia 5.2 mwaka wa 2022 hadi asilimia 4.95 mwaka wa 2023- hiiimechangiwa na kuimarika  kwa hali ya uchumi na kuwafanya wateja walipe mikopo kwa wakati.

4.Kuongezeka kwa mikopo kwa wateja kwa asilimia 21 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 61.0 hadi shilingi za kitanzania bilioni 74.0 mwaka 2023.

5.Kuongezeka kwa jumla ya Mali za bank kwa asilimia 17 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 107.0 mwaka 2022 hadishilingi bilioni 125.0 mwaka 2023.

6.Kuimarika kwa mtaji wa bank kwa asilimia 12 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 17.0 mwaka 2022 hadi shilingi za kitanzania bilioni 19.0 mwaka 2023.

Hivyo basi kutokana na sera ambayo bank imejiwekea  kuhusu ugawaji wa sehemu ya faida kwa wanahisa 'Gawio' ambapo bank  hutoa asilimia 50 ya faida yake kwa wanahisa wake . Hivyo kwafaida ya mwaka 2023 shilingi bilioni 2.35 jumla ya gawio ni shilingi  bilioni 1.17 . Hii ni sawa na  shilingi 44 kwa kila hisa. Mwaka jana gawio lilikuwa sawa na shilingi 26 kwa hisa. Sawa na ongezeko la asilimia 69.

Bank Kuu ya Tanzania  imeruhusu gawio hili kutokewa na pia  Mkutano wa wanahisa uluofanyika tarehe 22 Juni2024, ukumbi wa msasani tower ulipendekeza gawio hilo liwe kwa mfumo wa hisa badala ya fedha taslimu. Hivyo basi kila mwanahisa atapewa hisa za ziada kwa thamani halisi ya gawio analo stahili kupewa. Maamuzi haya yalifikiwa ili kuowezesha bank kuimarisha zaidi mtaji wake hasa kipindi hiki ambapo bank imepata kibali cha kutanuwa na kufanya kazi nchi nzima .

Nipende kutumia fursa hii kuwataarifu waandishi wa habari kwamba Maendeleo  Bank imepata kibali rasmicha kupanda hadhi na kuwa bank inayofanya kazi nchi nzima  ikiwa ni pamoja na kufunguwa matawi nje ya Der es salaam.  Mafanikio haya yalisubiriwa kwa hamu kubwa kwa miaka  mingi kutokana  na kigezo cha mtaji ambao bank ilikuwa na hadhi ya kikanda. Kwa sasa  Bank imefikisha mtaji wa bilioni 19 ambao unakidhi kuiwezesha  bank kufanya kazi nchini kote. Ili bank iruhusiwe kufanya kazi nchini kote ni lazima mtaji wake uwe zaidi ya shilingi bilioni 15.

Mwisho nipende kuwakumbusha ndugu waandishi wa habari na uma  mzima  wa watanzania kwamba bank inaendelea kuwekeza  kwenye teknolojia na sasa tuko hatua  za mwisho katika kuanzisha  huduma mpya  za kidigitali kama bank ya mtandao ( Internet banking), mfumo wa ukusanyaji wa malipo ikiwemo ada za shule (PCS) na mikopo kwa njia ya simu, hii itaeezesha  bank kuongeza faida  kwa fedha za wanahisa kwa mwaka 2024 na  kuboresha njia mbadala za upatikanaji wa huduma  kwa wateja  wetu.

Katika juhudi za kuboresha  huduma , mwaka huu 2024,tumefungua tawi jipya  Mbagala ambalo ni tawi letu la tano tukiwa na lengo la kuwasogezea huduma  wateja wao na wakazi wa Mbagala na maeneo jirani. Haya yamesemwa  na kiongozi wa Bank ya Maendeleo jijini dar es salaam  Ofisini kwao.

Habari na Ally Thabit 



Friday, 12 July 2024

MRADI WA KAIZEN WAFIKA KWA KISHINDO MIKOANI

 Richard  Pweleza Mratibu wa Kaizen amesema lengo la kuwa na mradi wa kaizen kuwakuza wajasilia Mali wadogowadogo pamoja na viwanda vidogovidogo ili watengeneze bidhaa zenye ubora  mpaka sasa mradi wa kaizen upo kwenye mikoa 19 ikiwemo mkoa ,,Morogoro,Pwani,Tanga,Dodoma ,Singida , Arusha,Ruvuma na mikoa mingineyo pia mradi umefika Zanzibar eneo la Pemba na Unguja .

Ametoa wito kwa watu kufika ofisi za Sido na chuo cha Cbe ili wapate fursa ya kujiunga na mradi wa kaizen amesema haya kwenye maonyesho ya 48 kwenye viwanja vya sabasaba  jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 


BOT YAWATOA OFU WATANZANIA

 Emanuel Tutuba Gavana wa Bank Kuu ya Tanzania amesema watu wasiwe na ofu sekta ya fedha nchini tanzania ni Imara  kwani amna mikopo chechefu kwenye mabenk ya tanzania na Bot wana akiba ya fedha za kutosha.

Pia ameupongeza uongozi wa Bank ya Tiob kwa kuwaunganisha vijana pamoja kuwatafutia fursa za ajira kwa kuanzisha shindano la TIOB Challenge kwani shindano ili linatija kubwa kwa vijana na taifa kwa ujumla.

Emanuel  Tutuba amewataka wafanyakazi wa mabenk wawe waadirifu,Wazalendo na waaminifu pia Bot imeandaa mitaala ya kutoa elimu ya fedha .huku kuna mipango ya kuwafikia makundi mbalimbali mfano wavuvi,wafanyabiashara wadogowadogo,wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wa aina zote lengo sekta ya fedha iwe jumuishi nchini tanzania  amesma haya kwenye utoaji wa tizo na zawadi kwenye shindano la Tiob Challenge lililoandaliwa na Bank ya Biob kwenye ukumbi wa kimataifa JNICC jijini Dar es salaam.

Habari na Ally Thabit 

MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA BANK YA TIOB AWEKA MIKAKATI MIZITO


 Patrick  Mususa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji  wa Bank ya Tiob amewapongeza na kuwashukuru washiriki wa shindano la Tiob Challenge wapatao 2462 kutoka vyuo vikuu nchini tanzania ambako malengo yalikuwa vijana wapatao 2000 ndio waliolengwa . Haya ivyo kuvuka lengo inaonyesha vijana wanautayari wa kuchangamkia fursa zinapojitokeza kwenye sekta ya fedha.

Ivyo bank ya Tiob imeamuwa kuweka mokakati madhubuti na imara ili kuwepo na muendelezo wa shindano la TIOB Challenge pia kwa kujua umuhimu wa wasichana ambao wapo vyuo vikuu wameweka mipango mikakati ya wao kushiriki kikamilifu.

Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji  wa Bank ya Tiob Patrick  Mususa ametoa rai kwa wadau nchini tanzania  kudhamini shindano la TIOB Challenge amesema haya wakati wa utoaji tuzo na zawadi kwenye shindano la  TIOB Challenge lililoandaliwa na Bank ya  Tiob lililofanyika jijini dar es  salaam  kwenye ukumbi wa kimataifa JNICC.

Habari picha na Ally Thabit 

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU IFM AIPONGEZA BANK YA TIOB

 

Eliki Mwanafunzi wa Chuo  Kikuu cha Ifm amesema Bank ya Tiob imefanya jambo Zurich kwa kuweka shindano la Tiob Challenge Lilojumuisha vijana wa vyuo vikuu wapatao 2462 ambako wamevuka lengo jumla ya washiriki 2000 .Eliki amesema shindano ili limeibua fursa mbalimbali kwa vijana waliopo vyuo vikuu kwani vijana watapata ajira za kutosha ,watapata ujuzi na maarifa kuhusu elimu ya fedha .

Eliki Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ifm amekuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano haya ambako amepata fursa ya kujitangaza,kuendelea kusoma bule kwa ngazi ya juu na pengine akapqta ajira kwa mabenk yaliyopo nchini tanzania. 
Ametoa rai kwa waandaaji waendelee kuandaa na waongeze kasi ya washiriki.

Ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuchangamkia fursa zinavyojitokeza amesema haya jijini dar es salaam  kwenye utolewaji wa tuzo na zawadi kupitia shundano la Tiob Challenge lililoandaliwa na Bank ya TIOB ilioyo fanyika kwenye ukumbi wa kimataifa JNICC jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Thursday, 11 July 2024

MUHADHIRI WA CHUO KIKUU MZUMBE APONGEZA KONGAMANO LA CEGA AFRICA EVIDENCE SUMMIT 2024

 

Dr Tukae Mbegalo Muhadhiri Chuo kikuu Mzumbe amesema Kongamano ili  la Africa Evidence Summit litasaidia kupata mbinu za kufanya tafiti na matumizi ya kisasa ya kiteknolojia ya kufanyia tafiti '' amesema tafiti zinawezesha kufanya mabadiliko ya kisera,sheria ,kanuni taratibu na miongozo.

Pia tafiti zinaongeza uelewa kwa makundi maalum  ususani  kwa watu wenye  usonji  na tafiti zinaonesha fursa mbalimbali katika jamii mfano kwenye kilimo na maeneo mengineyo. Tafiti zinakuza na kiboresha huduma za kijamii kama huduma za afya . 

Chuo Kikuu cha Mzumbe kinafanya tafiti kwenye sekta ya Afya,Kilimo, Elimu,Utawala, Biashara,Sayansi  na Teknolojia kwa upande wake muhadhiri Dr Tukae Mbegalo anafanya tafiti kuhusu elimu kwa watoto waliopo shule za awali lengo kuwaandaa watoto mapema ili kupata watu wenye uweredi na elimu pamoja na ujuzi wa kutosha ambao utasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na tanzania  kwa ujumla .

Muhadhiri Dr Tukae Mbegalo amewapongeza na kuwashukuru waandaaji wa kongamano lilowajumuisha watafiti na wadau mbalimbali kutoka ulimwenguni na bara la Africa amesema haya kwenye kongamano la siku mbili jijini dar es. salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Wednesday, 10 July 2024

CHAMA CHA CUF KUTIKISA DUNIA TAREHE 12 /7/2024

 Mwandisi Mohamed Ngurangwa wa Chama cha Cuf amesma tarehe 12/7/2024 Chama Chao cha Cuf kinamkabidhi kadi ya uanachama kama na gwisi wa siasa nchini tanzania  mkoani Singida eneo la Kondoa amesema haya wakati akizungumza na wasafi redio na wasafi TV.

Habari na Ally Thabit 

RATRA CC YAIMIZA MATUMIZI SALAMA YA BARABARA

 Emanuel Baraka Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam  na mjumbe wa baraza la usalama barabarani ratra cc anawataka wananchi kutambuwa wajibu na haki zao wanapokuwa barabarani pia watumiaji wa vyombo vya moto wazingatie sheria za usalama barabarani wakifanya ivyo ajali nchini tanzania zitapungua kwa kiasi kikubwa Pindi abilia anapoitaji kutoa taarifa apige simu bure 0800111080 au 0800110020.

Emanuel Baraka wa Ratra cc ameupongeza uongozi wa ratra cc kwa kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni na vyuoni na kutengeneza vipeperushi vya maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasiona amesema haya kwenye maonyesho ya 48 viwanja vya sabasaba jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

MWALIMU SALEHE AWAITA WATU WENYE ULEMAVU KUCHANGAMKIA FURSA VETA

 Mwalimu Salehe amesema Chuo cha Veta Kinatoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu  wa aina zote lengo watu hawa waweze kujitegemea kiuchumi na kimaisha ivyo ni vyema wazazi na walezi wasiwafungie ndani watu wenye ulemavu badala yake wawapeleke veta ili wapate ujuzi wa aina mbalimbali ''huku akiwataka watu wenye ulemavu  kutokata tamaa kwani wajiunge veta watapata fursa mbalimbali amesema haya kwenye maonyesho ya 48 kwenye viwanja vya sabasaba  jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

WATU WENYE ULEMAVU WAIPONGEZA VETA

 Bonifas  Kienze Muhitimu wa Veta AsieOna anaishukuru veta kwa kuwapa mafunzo watu wasio Ona kwa kujifunza Ufundi serenata na Ufundi wa Alminiam kwani unawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamuwa kiuchumi.

Bonifas Kienze ni Fundi Serema asiye Ona ambae anatengeneza Vitanda'makabati'meza na vitu vinginevyo vya mbao anawataka watu kutembelea maonyesho ya 48 viwanja vya sabasaba kwenye banda la veta . Ametoa wito kwa jamii wawapeleke watu wenye ulemavu  veta ili wapate ujuzi.

Amesema haya kwenye maonyesho  ya 48 kwenye  viwanja vya  sabasaba jijini dar es salaam 

Habari na Ally Thabit 

PROF EDWARD MIJUEL AIMIZA MATUMIZI YA TAFITI KWA AFRICA


 Prof Edward Mijuel amezitaka Nchi za Bara la Africa Kuzingatia Matumizi ya Tafiti kabla awajapanga mipango yao .Kwani tafiti zinaonesha matatizo ya watu na maitaji yao  mfano tafiti za afya zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa au kupunguza vifo vya wakina mama na watoto'' pia tafiti zinasaidia kufanya maboresho ya sera na sheria .

Prof Edward Mijuel  amesema wamekutana watafiti na wadau mbalimbali kwenye mkutano wa Africa Evidene Summit ambao mkutano huu unajumuisha nchi ya tanzania'kenya'uganda'ethiopia na nchi zinginezo kutoka mabara tofauti Lengo kuangalia  na kujadili changamoto wanazokutana nazo watafiti na kuweka nguvu za pamoja za kushawishi serikali za Africa karika kutumia tafiti kwenye mipango yao.

Swala la tafiti kujumuisha watu wenye ulemavu wa aina zote ni muhimu na zina tija amesema haya kwenye mkutanoa wa Africa Evidence Summit unaofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA ESRF AELEZA UMUHIMU WA TAFITI

 

Prof Fotunata  Songora Makene Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji  wa Taasisi ya Utafiti ESRF amesema tafiti ni muhimu  kwani zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo kwenye jamii kwenye sekta mbalimbali mfano Afya, Elimu na Kilimo .

Pia tafiti zinasaidia kwa kiasi kikubwa watu kuondokana na umasikini  ametoa wito kwa watunga sera kutumia tafiti zinazofanywa na watafiti ili serikali iweze kuboresha sheria, Kanuni taratibu na Miongozo ili kuwepo na mabadiliko na maendeleo katika jamii.

Mfano serikali ya tanzania itatoa mafunzo ya Amali kwenye secondary hapa nchini lengo wanafunzi wakimaliza shule ya secondary waweze kujiajili' kwani serikali imeweza kutumia mfumo huu baada ya watafiti kufanya  tafiti kwenye sekta ya elimu amesema haya kwenye mkutano wa Africa Evidence Summit jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Tuesday, 9 July 2024

MKURUGENZI WA RANJI YA NARCO AELEZA PUNGUZO LA BEI YA NG'OMBE


 Mkurugenzi  wa Ranji ya Narco Mohamed  Mbwana amesma serikali imetenga ardhi ekta 12 elfu lengo kufuga ng'ombe ambao nyama za  ng'ombe hawa zitauzwa nje ya nchi ambako kwa sasa tanzania  kupitia ranji Narko wanauza nyama ya ng'ombe falme za kiarabu.

Pia ranjit ya Narco inauza ng'ombe wenye ubora kwa bei ya punguzo milioni mbili na lakitano sawa na asilimia 29% ambako mwanzo ilikuwa milioni tatu na lakitano aina ya borani ng'ombe aina ya mitamba milioni moja na lakitano kati ya asilimia 40% ya bei punguzo apo awali ilikuwa inauzwa mitamba milioni mbili na laki tano .

Mkurugenzi  Mohamed Mbwana amesma mikoa ya ranjit ya narco too Rukwa,Karambo,Ruvuma,Morogoro,Mkata na Dodoma Kongwa. Pia amesema bajeti ilioandaliwa kupitia wizara ya mifugo itasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa chanjo,Uwepo wa ng'ombe na maitaji mengine.

Ametoa rai kwa wananchi waitumie ranjit ya narco ili waweze kujiajili kupitia sekta ya mifugo amesema haya kwenye maonyesho ya sabasaba ya 48 jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit. 

DR RAMADHAN AIOMBA SERIKALI KUWAUNGA MKONO WABUNIFU


 Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Udom Dr Ramadhan  Bakari amesema wanafunzi wa chuo cha Udom wamebuni Sateraiti pamoja na Loketi  lengo tanzania iwe na Sateraiti yake na Loketi yake yenyewe ili kuepuka gharama za vitu hivi kutoka nje ya nchi . 

Ametoa wito kwa serikali na wadau kuunga juhudi na jitihada  za wanafunzi wa chuo cha Udom waliobuni Sateraiti  na Loketi amesema haya kwenye maonyesho ya 48 kwenye viwanja vya Sabasaba. 

Habari picha na Ally Thabit 

SIDO YAWAFIKIA WAJASILIA MALI KIBABE


 Afisa Masoko wa SIDO amesema Kwenye Viwanja vya Sabasaba katika Maonyesho ya 48 Sido inawajasiliamali wadogo zaidi ya 135 ambako wajasiliamali hawa wametoka mikoa tofauti tofauti Wengine Zanzibar Lengo la Sido kulea wajasiliamali wadogo na viwanxa vidogo viogo kwa kuwapa elimu'kuwatafutia masoko na kuwaunganisha taasisi za ubora wa viwango.

Afisa Masoko wa Sido Linusi Lindu amesema Sido inaunda mashine za kukatoa mbao 'kutengeneza juis'na zinginezo ametoa wito kwa watu watembelee banda la Sido kwaajili ya kununua bidhaa mbalimbali kwenye maonyesho ya 48 na wajiunge na sido kwaajili ya kupata fursa mbalimbali za kujifunza nq masoko.

Habari picha na Ally Thabit 

MWENYEKITI MPYA WA CHAMA CHA ADC AWATULIZA WANACHAMA


 Shabani Itutu Mwenyekiti  Mpya wa chama cha Adcambae alipata kura 121 dhidi ya Doyo Hassan Doyo ambae alipata kura 70 kwenye uchagu'i uliofanyika hivi karibuni na kusababisha kuwepo kwa mgogoro ndani ya chama cha Adc mpaka kupelekea Doyo Hassan Doyo kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi.   ambako akafanya maamuzi ya kuwasilisha rufaa kwenye kamati ya uchaguzi ambako kamati ya uchaguzi wa chama cha Adc  Inawataka Shabani Itutu na Doyo Hassan Doyo wafanye maridhiano ili kusiwepo na mgogoro na Mwenyekiti  Shabani Itutu pamoja na Doyo wamekubali kufanya maridhiano amesema haya jijini dar es salaam  makao makuu ya chama cha Adc .

Habari na Ally Thabit 

CHAMA CHA ADC CHAINGIA KWENYE MARIDHIANO


Mwenyekiti  Mpya wa Chama cha ADC ambae kashinda kwa kishindo kwakura 121 dhidi ya mpinzani wake Doyo Hassan Doyo mwenye kura 70 ambae bwana Shabani Itutu amesema wamepokea rufaa kupitia kamati ya uchaguzi ilio wasilishwa na ndugu Doyo juu ya kupina maamuzi ya uchaguzi. Mwenyekiti  Shabani Itutu wa chama cha Adc amekubali na kupokea ushauli wa kamati namna ya kufanya maridhiano na ndugu Doyo amesema jambo ili ni zuri kwa masrai ya chama cha Adc.

Habari picha na Ally Thabit 

RICHARD PWELEZA MRATIBU WA KAIZEN AIMIZA WATANZANIA KUTUMIA MRADI WA KAIZEN KUKUZA BIASHARA ZAO




Habari Picha na Ally Thabiti
 

MOHAMED ZUBERI MBWANA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA RANCHI YA NARCO



 Habari Picha na Ally Thabiti

Friday, 5 July 2024

BODI YA SUKARI YATAKA KUWAPUUZA WAPOTOSHAJI


 Mkurugenzi  wa Bodi ya Sukari Prof Keneth Bengesi anawataka watu kuwapuuza wanao sambaza taarifa za uongo kuhusiana na vibali vinavyotolewa na bodi ya sukari Kwani kampuni zote zinazoingiza sukari nchini tanzania zina vibali na zimefuata kanuni'sheria' taratibu na miongozo ya uingizaji wa sukari.

Pia bodi ya sukari inatoa vibali kwa wakati na inazingatia usalama wa afya za binadamu katika matumizi ya sukari ametoa wito watu kuacha mara moja kupotosha jamii na wakiitaji taarifa waende bodi ya sukari haya akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Thursday, 4 July 2024

NAIBU WAZIRI MKUU AKIPONGEZA CHUO CHA BAHARIA DMI

 Dr Dotto Mashaka  Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa na chuo cha baharia (DMI) kwa kuandaa wataalam ambao watasaidia kukuza na kuomarisha uchumi wa bluu nchini tanzania pia amewataka wanafunzi wa chuo hichi kuzingatia wanayofundishwa na watafasiri kwa vitendo dhana ya uchumi wa bluu. 

Huku akiwataka washiriki wa kongamano la uchumi wa bluu watoe mawazo'ushauri'mipango na mikakati yakufikia uchumi wa bluu....amesema haya kwenye kongamano la siku mbili lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji wa Mazingira na Maendeleo  ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu  linalofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MKURUGENZI WA AZAM MALRINE APONGEZA UCHUMI WA BLUU


 Abubakari Azizi Mkurugenzi  wa Azam Marine amesema Uchumi wa Bluu utasaidia kwa kiasi kikubwa kukuwa kwa uchumi wa tanzania kwa mtu mmoja mmoja  na taifa kwa ujumla anawataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwenye bahari 'maziwa 'mito na mabwawa kwani wakifanya ivyo uchumi wao utaimarika .

Amekipongeza chuo cha  Mabaharia kwa kuunga mkono juhudi na jitihada za serikali katika kuelekea uchumi wa bluu kwa vitendo kwa kuandaa wataalamu kupitia chuo cha mabaharia (DMI) ....amesema haya kwenye kongamano la siku mbili  jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

ERASTO AIZAKI MWANAFUNZI CHUO CHA BAHARIA (DMI) AAHIIDI MAZITO TANZANIA KUELEKEA UCHUMI WA BLUU


 Mwanafunzi wa Chuo cha Baharia  cha (DMI) Erasto Aizaki Lamosai amesema Cheti na Zawadi alioipata kwaajili ya ubunifu alioufanya kwa kifaa cha kutambua matatizo yaliopo kwenye boti inavyokuwa inatembea ndani ya maji imemtia moyo na faraja kubwa  kwa kutambulika mchango wake kwenye Uchumi wa Bluu anaiomba serikali kifaa hiki kitumike pia ataakikisha anafanya bunifu zingine zenye tija na faida kwa nchi ya tanzania ili lengo na dhamira ya rais Dr Samia la uchumi wa bluu likamilike kwa vitendo .

Amesema haya kwenye kongamano la siku mbili linalojadili uchumi wa bluu  lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji  Utunzaji wa mazingira na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MASAKA JULIUS MASAKA MWANAFUNZI WA CHUO CHA BAHARIA (DMI) ABUNI TEKNOLOJIA


 Mwanafunzi wa Chuo cha Baharia (DMI) Masaka Julius Masaka amebuni kifaa cha kubeba mizigo bandarini ivyo anaiomba serikali wamuunge mkono kwa teknolojia alioibuni kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za kununua vifaa vya kubeba mizigo nje ya nchi kwani kifaa shake kinauwezo wa kubeba content zenye mizigo.

Masaka Julius Masaka ameupongeza uongozi wa chuo cha baharia DMI  kwa elimu wanayoitoa yenye Ubora  amesema haya kwenye kongamano la siku mbili jijini dar es salaam  lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji wa Mazingira  na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu. 

Habari picha na Ally Thabit 

MWANAFUNZI WA CHUO CHA BAHARIA (DMI) AUNGA MKONO UCHUMI WA BLUU


 Hamadi Mussa Hamadi Mwaanafunzi wa Chuo cha Baharia(DMI) amesema katika kuunga mkono juhudi na jitihada za serikali katika kuelekea uchumi wa bluu  yeye amefanya ubunifu wa limondi kwaajili ya kuwasha taa kwenye meli hii inasaidia kama kuna dhalura imetokea ndani ya meli unatumia limont kuwasha taa bila kufika eneo la tukio amesema haya kwenye kongamano la siku mbili  linalojadili uchumi wa bluu kwenye ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam. 

Ambako chuo cha baharia (DMI) kimeandaa kongamano ili la tatu lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji wa Mazingira na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili  ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu.

Habari picha na Ally Thabit 

TBS YAELEZA MIKAKATI YAO


 Emanuel wa Tbs  akiwa na Espekta  Maganga wa Ukaguzi wa Tbs  katika viwanja vya sabasaba  wamesema Tbs wanatoa elimu kwa jamii namna ya kutambua bidhaa feki na zilizoisha muda wakewa kutumika Tb imeimarisha mifumo na wametoa wito kwa jamii wafike kwenye viwanja vya sabasaba na watembelee banda la tbs ili wajifunze mambo mazuri kutoka Tbs  wamesema haya kwenye maonyesho ya 49 .

Habari  picha na Ally Thabit 

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LAWATOA OFU WATANZANIA

 LuteniKanali Gadetius Ilonda  amesema Jeshi la wananchi litaazimisha miaka 60 tangu lianzishwe mwaka 1964 katika maazimisho haya kutakuwa na shunguri mbalimbali za utoaji huduma za tibambalimbali kwa wananchi kwa magonjwa yote kwa wananchi ni bule ambako mikoa ya dar es salaam'Pwani'Tanga'Ruvuma'Mbeya 'Tabora'Zanzibar'Mwanza'Tabora pia kutakuwa na maonyesho ya tamad0uni lengo la maonyesho haya kuonesha mira na desturi  za watanzania .

Pia kutakuwa na Ujio wa Jeshi la Watu wa China ambako jeshi ili litatoa huduma za tiba kwenye meri yao ...lengo la ujio wachina kukuza demokrasia ya kijeshi nakukuza uchumi wa watanzania ametoa wito kwa wananchi kutokuwa na wasiwasi wala ofu watapokuwa wakiona vifaa vya kivita vya kijeshi kwenye maeneo  yao na miungurumo ya silaa nzito kwani maazimisho haya ya miaka60 ya jeshi la wananchi wa  tanzania litaendana na uchangiaji wa dam ivyo wanajeshi watachangia damu na wananchi wanaombwa kuchangia damu.

Lengo la uchangiaji wa dam ni kusambaza kwenye hospitali zote mchini kwaajili ya kuokoa maisha ya kinamama waojifungua na majerui.

Habari picha na Ally Thabit