Wednesday, 12 February 2020

CHUO CHA N.I.T CHABAINISHA MIKAKATI MIZITO

Mkuu wa chuo cha Usafirishaji na Uchukuzi(NIT) prof Zakaria Mganirwa amesema kiasi cha fedha zaidi ya bilioni50 zimetengwa kwaajili ya kuhimarisha miundombinu ya chuo cha NIT na ununuzi wa vifaa mbalimbali kwaajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa chuo cha Usafirishaji na Uchukuzi NIT ndege 5 zitanunuliwa na chuo cha NIT ambako ivi karibuni zitaanza kufika nchini Lengo wanafunzi watakao jifunza Urubani waweze kuzitumia kwenye mafunzo yao Mkuu wa chuo cha NIT amemshukuru rais Magufuli na serikali Kwa ujumla kwa kukiimariaha na kukijengea uwezo chuo cha NIT uku akipongeza jitihada za serikali Kwa kuwapeleka wakufunzi nje ya nchi zaidi ya 50 kwenda kuongeza ujuzi kwenye sekta ya Usafirishaji na Uchukuzi ambako itapunguza gharama Kwa watanzania kwenda kusomea mafunzo ya Usafirishaji na Uchukuzi nje ya nchi


Habari picha na Victoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment