Mgeni Rasmi kwenye Mahafari ya Shule ya Ujenzi iliopo mkuranga mjini Dr Tindwa amesema siri ambayo watu awaijui kuhusu shule ya Ujenzi . Wanafundisha watoto ambao watoto wao wamewakatia tamaa ya elimu na maisha kwani yeye mtoto wa dada yake aitwae Ashura shule nyingi za serikali na binausi zilimshindwa lakini shule ya ujenzi imeweza kumbadilisha mpaka kupelekea kufanya vizuri kidato cha 4 na hatimae kwa sasa anachukuwa Digrii chuo cha Uhasibi.
Pia shule ya ujenzi inaibuwa kulea na kukuza vipaji vya wanafunzi na inawafadhiri watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ni vyema wazazi na walezi wawapeleke watoto wao kusoma shule ya ujenzi ambayo ipo chini ya Dr Mtembei .
Dr Tindwa anawataka wadau,makampuni,taasisi na serikali kuunga mkono juhudi na jitihada zinazofanywa na shule ya ujenzi iliopo mkuranga mjini ndio maana leo hii katila mahafari ya wanafunzi wa Awali na daradara la saba yeye mgeni rasmi Dr Tindwa anakabidhi zawadi ya gari kwa uongozi wa shule ya ujenzi .Ambako mkuu wa shule anapokea kwa niaba yao kama inavyoonekana pichani.
Huku mkuu wa shule ndugu Saimoni akishukuru kwa kupewa zawadi ya gari amemuhakikishia mgeni rasmi Dr Tindwa kuwa zawadi ya gari itatumika kwa malengo yaliokusudiwa kwenye shule ya ujenzi iliopo mkuranga mjini.
Habari na Ally Thabit