Thursday, 23 February 2023
TAASISI YA AG GENERGIES YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA BIDHAA ZAO
RISHIT RADIA MKURUGENZI
Mkurugenzi Rishit Radia Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha kahawa amesema wanafanya kazi na wakulima zaidi ya 800 kiwanda cha kusaga na kusafisha alafu wanapaki kwenye paketi
ujazo milimita 250 wanaweka kwenye gunia kilo 60 kwaajili ya kahwa inaladha tamu, watu wanje wanafurahia pamoja na wakulima wameenea Tanzania nzima na kimataifa zaidi. kiwanda kipo talime
Haya yamesemwa na mkurugenzi wa kiwanda cha NORTHERN HIGHLANDS COFFEE COMPANY
Habri kamili na Victoria Stanslaus
Madaktari bingwa wa MOI wapewa mbinu za kisasa za upasuaji wa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) zimeanza kutoa mafunzo maalum ya upasuaji wa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo kwa mbinu za kisasa kwa madaktari bingwa waliohitimu katika chuo hicho ambapo wagonjwa 4 wamefanyiwa upasuaji huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema mafunzo hayo yanaongozwa na Mkufunzi maalum kutoka hospitali ya St. Luke`s, Ugiriki kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa matibabu ya kibobezi.
“Mafunzo haya ni endelevu ambapo wataalam wetu watafundishwa upasuaji wa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo kwa mbinu za kisasa ambapo mpaka sasa wagonjwa wanne kati ya saba waliopangwa wameshafanyiwa upasuaji huo” amesema Dkt. Boniface
Aidha, Dkt. Boniface ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kwani zaidi ya Millioni 50 zimeokolewa kama wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Dkt. Nicephorus Rutabasibwa amesema Madaktari bingwa watatu wa MOI waliohitimu Chuo cha MUHAS watafundishwa mbinu za kisasa za na za kibobezi zakutibu magonjwa ya mishipa ya damu kwenye ubongo.
“Mafunzo haya yamegawanyika katika sehemu nne ambapo tunalengo la kuwafanyia wagonjwa 40 katika kipindi cha mwaka mmoja kwa ajili ya kuwajengea uwezo wataalam wetu ili baadae wawafundishe wenzao waliopo katika hospitali mbalimbali nchini” amesema Dkt. Rutabasibwa
Naye, Mtaalamu Bingwa Mbobezi wa Mishipa ya damu kwenye Ubongo kutoka hospitali ya St. Luke`s kutoka Ugiriki Prof. Athanasios Petridis amesema anafuraha kubwa kuwa MOI na kutoa mafunzo ya kibobezi ya upasuaji wa kuzibua vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo na baada ya mafunzo hayo wataalam hao watakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji huo.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa Ubongo Dkt. John Michael Mtei ameushukuru uongozi wa Taasisi ya MOI kwa mafunzo hayo kwani yamewajengea uwezo wa kutibu magonjwa ya mishipa ya damu kwenye ubongo .
habari picha na Victoria Stanslaus
Friday, 17 February 2023
Picha: Rais Samia amewasili Addis Ababa nchini Ethiopia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AWATAKA TANROADS NA TARURA KUTEKELEZA MIRADI
Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka TANROADS na TARURA kutekeleza ujenzi wa Barabara zilizopo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam kwani mbunge wa Mbagala Chaurembo amesema katika jmbo lake la mbagala kwa kiwango kikubwa barabara bado hazijatengenezwa nae mbunge wa kibamba amelalamikia kutopewa kipaumbele barabara zake. Huku Mbunge Bona Kalua akiwataka TARURA waeleze lini watatengeneza barabara kwenye jimbo lake na wathibitishe kama pesa wanazo nae Mbunge Ndungulile wa Kigamboni akitoa kilio kuhusu ujenzi wa barabara wa mwendo kasi katika jimbo lake la kigamboni.
Meneja TARURA amesema barabara za DMDP zitajengwa katika jiji la Dar es Salaam kwani Benki ya Dunia iko Tayari kutoa hizo fedha na michakato imeanza hivyo ifikapo mwezi 11-2023 miradi ya barabara itatekelezwa kwa vitendo. Amewatoa hofu wabunge na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa TARURA itatekeleza kwa vitendo na sio kwa maneno.
Habari kamili na Ally Thabith
RIDHIWANI AGAWA PIKIPIKI KWA WATENDAJI WA KATA SITA NA KUPOKEA
Naibu Waziri wa Ardhi ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa pikipiki kwa watendaji wa kata 6 za Halmashauri ya Chalinze, pamoja na kutembelea kiwanda cha Uzalishaji wa marumaru cha Keda.
Pia, amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Vituo Vya Afya kwa ajili ya Vituo Vya Afya Viwili Kata za Kibindu na Msata na Zahanati vijiji 11.
Akigawa Pikipiki hizo, Ridhiwani amewakumbusha Watendaji kutumia vifaa hivyo kwa kuzingatia makusudio ya kutolewa kwa vyombo hivyo vya moto ikiwemo kwenda kusikiliza wananchi na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao.
Vilevile akikabidhi vifaa tiba wamehimizwa kuvitunza na kuvitumia kwa makusudio vifaa hivyo.
"Kazi kubwa inaelekezwa kituo cha Afya Miono ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa kipaumbele";: Kwa upande wa kiwanda tumewashukuru wawekezaji kwa kutambua mchango wa Raisi Dkt. Samia Suluhu #KaziInaendelea
Habari Picha na Ally Thabith
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM NA WASERIKALI
Amos Makala Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam tarehe 15/02/2023 amekutaka na viongozi wa ccm mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam wa ngazi zote pamoja na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali lengo kuweka mikakati ya maendeleo ya chama cha mapinduzi kwa kuitekeleza kwa vitendo, pia waweze kutambuana kwani ni wapya.
Habari kamili na Ally Thabith
Thursday, 16 February 2023
MBUNGE WA KAWE AWATAKA WATU WENYE ULEMAVU KUCHANGAMKIA FURSA
Askofu Gwajima Mbunge amewataka watu wenye ulemavu waende kwenye almashauri wapate mkopo wa asilimia mbili (2%).
Habari kamili na Ally Thabith
Sunday, 12 February 2023
RC Makalla afunguka kuhusu Machinga na Bodaboda kwenda Afrika Kusini
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla ametoa tamko rasmi kwa Viongozi wa machinga na bodaboda kwenda ziara ya mafunzo Afrika ya Kusini, ameyasema hayo leo Februari 11,2023 katika Ukumbi wa DMDP Ilala wakati akipokea taarifa kwa Viongozi hao baada ya kurejea kutoka ziara ya mafunzo nchini Rwanda.
CPA Makalla amesema amefurahishwa na matokeo ya ziara ya mafunzo waliyoifanya
nchini Rwanda kufuatia taarifa waliyoiwasilisha kwake.
Aidha CPA Makalla amefafanua kuwa miji ya Cape Town na Johanesburg Afrika ya Kusini ni miji katika tano bora kwa usafi Afrika hivyo ziara ya mafunzo nchini humo itapelekea kuleta mapinduzi makubwa zaidi ya Kampeni ya Usafi Jijini Dar es Salaam.
CPA Makalla amewataka Viongozi wa Machinga na Bodaboda kuitisha makongamano kushirikisha elimu waliyoipata nchini Rwanda kwa wanachama wao ili kuwa na uelewa wa pamoja ambao utalifanya Jiji la DSM kusonga mbele katika mikakati yake.
Hata hivyo CPA Amos Makalla amesema “Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuyalea makundi haya kufanya Kazi vizuri anachokifanya yeye katika Mkoa ni utekelezaji kwa vitendo maelekezo na maono ya Mhe Rais”- RC Makalla
CPA Makalla amewahakikishia Viongozi wa Machinga na Bodaboda kuendelea kuwapatia ziara za mafunzo kwa kadri inavyo wezekana kwa kuwa kuelimishana ni njia pekee na bora ya kuleta mabadiliko chanya.
Habari picha Ally Thabit
Picha: Ajali yaua mmoja, majeruhi 7 “Basi lilifeli breki na kutumbukia korongoni
Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine Saba kumjeruhiwa katika Kata ya Sigino Wilayani Babati Mkoani Manyara baada ya gari la abiria aina ya Costa kufeli breki na kutumbukia katika korongo.
Akizungumza na Ayo TV kwa njia ya simu kuthibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Acp George Katabazi amesema gari hilo lilikuwa likitokea Mkoani Singida kuelekea Arusha na baada ya kufika eneo la
Kona ya Logia ndipo likafeli breki na kumshinda dereva.
“Ajali imetokea asubuhi gari lilikuwa na watu 29 abiria ni 27 dereva mmoja pamoja na utingo wake, dereva amefariki huku majeruhi wakiwa 7 ambapo kati yao watatu hali zao ni mbaya ila abiria wengine walipata mshtuko tu, chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa breki wa gari hali iliyopelekea kumshinda dereva kulimudu gari hilo na kuingia kwenye korongo”-RPC Katabazi
Habari picha na Ally Thabit
Rais Samia afunguka “akikupa Stress achana nae, maisha yako ni zawadi pekee Mungu amekupa
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu amewasihi Wanafunzi wa Vyuo kuweka mkazo kwenye masomo na maisha yao na kujiepusha na mambo ambayo yatawarudisha nyuma na kusema hata kama Mtu ana Mpenzi ambaye anampa mawazo ni bora kuachana nae kwasababu kupigania maisha ni muhimu kuliko kupigania upendo wa kuharibiana maisha.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akizungumza na Wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (TAHLIFE) leo February 11,2023 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma “Nimuombe Mungu awashushie wote baraka mfanikiwe na yale mnayofanya, mnaosoma msome vema ile kurudia mwaka isiwepo, uki-disco usirudishwe nyumbani lakini kwanini udisco Mwanangu kwanini udisco kama kuna Mtu anakutia mawazo sio ebu achana nae angalia maisha yako kwanza”
“Kwa sasa chunga maisha yako usimpe Mtu mwingine nafasi ya kukuharibia maisha yako hapana, hakuna upendo wa kuharibiana maisha, akisema ‘nitakufa juu yako’ akafe umuone, nitakufa juu yako chozi linamtoka unamwambia kajinyonge haendi asikuharibie maisha, someni kwa bidii lakini msiacha kumtegemea Mungu”.
Habari picha na Ally Thabit
RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AONGOZA KAMATI YA UANGALIZI YA SADC NCHINI
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panelof Elders, POE) ameongoza Ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatilia Utekelezaji wa Makubaliano ya Amani nchini Lesotho katika ziara nchini humo tarehe 08 – 11 Februari, 2023.
Ziara ya Kamati hiyo ya Uangalizi ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika Kinshasha, DRC mwezi Agosti 2022 ambapo walilielekeza Baraza hilo la Wazee la SADC kufuatilia kwa karibu jitihada za usuluhishi wa migogoro inayoendelea kwa muda mrefu katika Falme za Lesotho na Eswatini.
Rais Mstaafu Kikwete ameongozana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius,
Paramasivum Vyapoory, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wazee
amepata wasaa wa kukutana na Mtukufu Motlotlehi Letsie III, Mfalme wa Lesotho, viongozi wakuu wa Serikali ya Lesotho pamoja na wadau wengine muhimu katika mgogoro huo.
Kamati pia imepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lesotho ambaye ndiye Mkuu wa Serikali, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Haki, Sheria na Masuala ya Bunge, Spika wa Bunge, Makamu Rais wa Seneti, Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko, Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani vilivyo Bungeni, Vyama vya Siasa vilivyo nje ya Bunge, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Askofu Mkuu wa Baraza la Kanisa la
Kikristu nchini Lesotho pamoja na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza, AfrikaKusini na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa.
Katika mikutano yote iliyofanyika, Kamati hiyo imesikiliza kwa kina maoni ya wadau hao wote kuhusu namna bora zaidi ya kuweza kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imeshafanyika katika kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro uliopo nchini humo. Kamati hiyo inaripoti kwa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) ambaye kwa sasa ni Hage Geingob,Rais wa Namibia.
OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWANOA MAAFISA WA SERIKALI MPAKANI
KANISA LA TAG LATIMIZA MIAKA 50
Mchungaji Taitas Kamani wa kanisa la TAG wila ya Ilala amesema kanisa hili lilianza mwaka 1973 hivyo wanajivunia mafanikio mbalimbali ikiwemo kuhudumia gereza la watoto.
Habari kamili na Ally Thabith
Saturday, 11 February 2023
UONGOZI WA BODABODA NA WAMACHINGA WAKABIDHI TAARIFA NZITO KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Uendesha bodaboda na bajaji ndug. Saidi amemueleza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, ziara walioenda nchini Rwanda imekuwa ni nzuri kwani wamejifunza namna ya udhibiti ajali ya bodaboda namna ya kuzingatia sheria barabarani nae mwenye wa machinga Namoto Yusuph Yusuph amesema elimu walioipata kwenye nchi ya Rwanda watawapa wamachinga mkoa wa Dar es Salaam ili vipato vyao vikue na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewataka viongozi wa machinga, bodaboda na bajaji waanze kutoa elimu kupitia makongamano.
Habari Kamili na Ally Thabith
Thursday, 9 February 2023
CUFF YALIA NA WALIOWEKA FEDHA NCHINI CHINA
(CUF- Chama Cha Wananchi)
Office of the National Chairman
P.O. BOX 10979 Dar es Salaam,
Tanzania
E-mail:
lipumba@yahoo.com
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI, 08 FEBRUARI 2023
SAKATA
LA FEDHA ZA PLEA BARGAINING ZILIZOKUSANYWA NA AFISI YA MWENDESHA MASHTAKA (DPP) NA UCHUNGUZI WA KILE
KILITOCHOKEA MPAKA BAADHI YA FEDHA HIZO KUTOJULIKANA ZILIPO
Sambamba na
uzinduzi wa Tume hiyo, Chama cha Wanaanchi-CUF tunafahamu juu ya uwepo wa
uchunguzi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni50 unaofanywa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG. Fedha hizizilipatikana kutokana na
utaifishwaji wa mali za Watanzania waliotuhumiwa kwa makosa ya jinai mbalimbali
na kupelekea makubaliano na serikali kupitia ofisi ya DPP yaani “Plea
Bargaining” ambao utahusisha kuhojiwa
kwa watu mbali mbali waliohusika katika jambo hilo.
Ndugu wanahabari,
kama mtakumbuka “Plea bargaining” ililetwa na mabadiliko ya sheria ya mwenendo
wa makosa ya jinai yaliyofanyika mwaka 2019 na kuendeshwa na ofisi ya Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP) kwa kuingia makubaliano na Watuhumiwa wa makosa ya jinai
ambao wengi wao hawakuwa wamepewa dhamana kutokana na makosa yao kutokuwa na
dhamana. Hata hivyo sheria hii ilitekelezwa na DPP hata kabla ya Mhe. Jaji Mkuu
kutunga kanuni za namna bora ya kutekeleza utaratibu wa “Plea bargaining” ambao
ungeainisha mambo muhimu kama akaunti ipi ambayo fedha hizi zipelekwe na kuweka
wazi namna ya matumizi ya fedha hizi.Jambo la kusikitisha zaidi, sehemu ya
fedha hizi zilipokelewa na DPP mwenyewe kwa njia ya fedha taslimu kinyume cha
sheria za nchi na zingine kuwekwa katika akaunti nchini Chinakama alivyoeleza
Mhe. Rais.
Ndugu wanahabari, Sisi
CUF-Chama Cha Wananchi tunaamini kwamba, kazi ya kuchnuguzana kutazama nini
kimetokea na nini kiliharibu ofisi hii ya DPP na kupelekeasehemu ya fedha hizo
za umma kutojulikana zilikowekwa haitoweza kufanikiwa kutekelezwa kwa uhuru na
TUME hii iliyoundwa na Mhe. Rais iwapo aliyekuwa Mkurugenzi wa Ofisi hiyo
kipindi cha Plea Bargaining; Jaji Biswalo bado anashikilia nafasi ya juu katika
moja ya ofisi ya utoaji haki, yaani Mahakama Kuu.
Na kama alivyosema
Mheshimiwa Rais kuwa kubadilisha Mkurugenzi wa ofisi hizi peke yake hakutotosha kumaliza mizizi inayopelekea kujitokeza
kwa mapungufu haya ya kiofisi, Sisi CUF -Chama Cha Wananchi tunaamini ili
kuhakikisha ofisi hizi zinabadilika kabisa na kutekeleza majukumu yake kwa
Muktadha wa Misingi ya Kikatiba, Demokrasia,
Haki sawa kwa wote na Utawala bora kwa mujibu wa sheria, basi hata wale
watumishi waliokuwa wakimsaidia Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kipindi hicho cha
“Plea Bargaining” wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi huru wa TUME hiyo na uchunguzi
wake utakuwa wenye tija na kufuata Utawala wa Sheria pamoja na kurejesha imani
ya Watanzania katika ofisi husika.
Tume pia ichunguze
na kubainisha kama kuna viongozi na taasisi nyingine zilizohusika katika sakata
hili.
Pamoja na uchunguzi
wa fedha zilizopokelewa taslimu na zilizowekwa kwenye akaunti za benki, pia
Tume ichunguze mali zisizohamishika zilizowekwa kama dhamana kwa wale
walioshindwa kulipa fedha taslimu, kama bado ziko mikononi mwa Serikali au
zimerejeshwa kinyemela.
Na mwisho, wale
watakaobainika wamehusika katika sakata hili ama la upotevu wa fedha au
matumizi mabaya ya ofisi husika basi wachukuliwe hatua za kisheria ili kuzuia
matukio kama haya kujirudia tena.
Tuna matumaini Tume
itafanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu, bila woga wala upendeleo na tunaitakia
utekelezaji mwema wa majukumu yake.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF - Taifa
Habari kamili na Ally Thabith
JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KIMETANGAZA UKAGUZI WA MAGARI
Lengo ni kudhibiti ajali pia amesema vyombo vya moto vitakavyo kaguliwa vitabandikwa stika mbele ya kioo cha gari ambako magari makubwa yatatozwa shilingi elfu saba, magari madogo Tsh 5000/= Bajaji na Pikipiki watatonzwa Ths 2000/= ametoa wito wakuwa vikosi vya usalama barabarani kutenga maeneo kwaajili ya ukaguzi wa vyombo hivi vya moto pia amewataka wenye vyombo vya moto kupeleka vyombo vyao vikaguliwe kwani ifikapo tarehe 11/03/2023 ndio mwisho wa ukaguzi hivyo sheria ya kukamata itatumika.
Habari picha na Ally Thabit
Saturday, 4 February 2023
PJM TANZANIA YAJA NA KIPODOZI KABAMBE
Mkurugenzi wa Kampuni ya PJM TANZANIA amesema kutokana na tatizo la Chunusi na matatizo ya ngozi wameamuwa kuja bidhaa kabambe yenye ubora na raisi kupatikana Kwa beinafuu bidhaa hii inaitwa BLUE VALLEY .
Mkurugenzi Piusi Morris amewataka watu wote kuchangamkia bidhaa yao BLUE VALLEY ili ngozi zao ziwe nyororo.
Nae Kwa upande wake Zai wa Kijiwe Nongwa ambae ni barozi wa bidhaa ya BLUE VALLEY amewataka watu watumie bidhaa hii kwani ngozi zao zitanawia.
Habari picha na Ally Thabiti
WAZIRI MCHENGERWA KUKUZA SEKTA YA SANAA
Waziri wa Sanaa, Michezo na Utamaduni amewaakikishia watanzania kuwa sekta ya Sanaa Michezo na Utamaduni zitakuwa Kwa kiwango kikubwa kwani Wizara Yake inatekeleza maagizo na maelekezo ya RÃ is Samia suluhu Hassan ambako Kwa sasas wizara imetoa mikopo ya Fedha isiyo na riba kwenye sekta mbalimbali za Sanaa.
Pia Wizara inakuja na vazi la taifa na mdundo wa taifa ,Waziri Mchengerwa ametoa Rai Kwa jamii kutowaficha na kuwafungia ndani watu wenye maitaji maalum wakiwemo wenye ulemavu wa Aina zote kwani wanauwezo makubwa na Wizara inawaunga mkono.
Mfano Wizara ya Sanaa Michezo na Utamaduni kupitia serikali ya Tanzania imempamkopo usio na riba msanii mwenye ulemavu CHIBAKISMATI milioni 10 Fedha ya kitanzania.
Habari picha na Ally Thabiti
MENEJA WA CHIBAKISMATI AJIVUNIA
Jilbert Rema ni Meneja wa CHIBAKISMATI amesema yangu aanze kumsimamia msanii wake wameweza kupata mafanikio makubwa.
MSANII ALI KIBA AKIPONGEZA WIZARA YA SANAA ,MICHEZO NA UTAMADUNI
Ali Kiba amesema Wizara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni imefanya Jambo zuri na Jena Kwa kuwapa mikopo isiyo na riba wasabi kwani itasaidia Kwa kiasi kikubwa kufanya kazi zao Kwa ufanisi na ajira zitaongezeka nchini Tanzania.
NMB BANK YAJIDHATITI KUWAKWAMUWA WAENDESHA BODABODA NA WAMACHINGA
Kiongozi wa NMB BANK amesema Lengo la kuwapeleka nchini Rwanda Wamachinga,waendesha Bodaboda na Bajaji ili waweze kuongeza wigo wa masomo nje ya nchi kama anavyoonekana Pichani akiwa na tiketi ya ndege .
Uku akiambatana na Mkuu wa mkoa wa DSM Amosi Makala ameahidi kuwa NMB bank itaendelea kuwatafutia fursa ya masomo Wamachinga, waendesha Bodaboda na Bajaji ndani ya nchi na nje ya nchi.
Habari picha na Ally Thabiti
PICHANI MWENYEKITI WA MACHINGA AKIAGANA NA UONGOZI WA MKOA WA DSM NA VIONGOZI WA NMB
Habari na Ally Thabiti
MKUU WA MKOA AWAPA BARAKA VIONGOZI WA MACHINGA NA BODABODA ZIARA YA RWANDA
Mkuu wa Mkoa wa DSM Amosi Makala amewataka viongozi wa Bodaboda ,Bajaji na Wamachinga wayatumie vizuri mafunzo wanayoenda kuyapata nchini Rwanda.
WAMACHINGA WAIPONGEZA NMB BANK
Mwenyekiti wa Machinga Mikoa wa DSM Namoto Yusufu Namoto ameipongeza na kuishikuru bank ya NMB Kwa kuwapeleka nchini Rwanda kwaajili ya mafunzo hivyo elimu watakayoipata watakuja kuwafundisha wengine.
Pia ametoa ofu Mkuu wa mkoa wa DSM Amosi Makala kuwa Wamachinga awatamuangusha na watachangamkia fursa nchini Rwanda.
Habari picha na Ally Thabiti
JUKWAA LA WAARIRI LAIPONGEZA UNITED NATIONS TANZANIA
Ndugu Barile ameumba umoja wa mataifa kutoa elimu Kwa Waariri na Wanahabari katika kuelekea uchaguzi wa wenyeviti wa serikali za mtaa mwaka 2024 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 .
Lengo wanahabari wakitanzania waandike habari sahihi za uchaguzi .
Habari picha na Ally Thabiti
U.N. YATETA NA WAARIRI WA VYOMBO VYA HABARI
Muwakilishi Mkaazi wa United Nations Tanzania amekutana wa waariri wa vyombo vya habari pamoja na wanahabari Lengo ni kuwaeleza nguzo 4 za Mipango ya U.N.kwani amesema nguzo. hizi za maendeleo ili zikamilike zinaitaji ushirikiano wa vyombo vya habari nchinitanzania.
Thursday, 2 February 2023
WAZIRI ASHATU KIJAJI AWATAKA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRI KWENYE BIASHARA
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt Ashatu Kijaji anawataka watu wenye maitaji maalum watumie mikopo ya 2% inayotolewa kwenyehalmashauri ili wazitumie kufanya Biashara,
Wizara Yake inahudumia makundi tote
Habari picha na Ally Thabiti
DR GODWILL G WANGA EXECUTIVE SECRETARY WAFANYABIASHARA WACHANGAMKIE FURSA
Prime Minister's Office Dr Godwill G Wanga Executive Secretary amesema wafanyabiashara, wawekezaji na wenyeviwanda wachangamkie fursa za kiuchumi ilikukuza patio la Tanzania, amewataka ofu washiriki wa mkutano kuwa changamoto walizowasilisha watafanyia kazi.
Habari picha na Ally Thabiti
WAZIRI ANJERA KAIRUKI ALEJESHA TUMAINI KWA WALIMU
Waziri wa Tamisemi Anjera Kairuki amewaakikishia Walimu kelo na changamoto zao zote ikiwemo kupandishwa madaraja na makazi zitatatuliwa na pia Kwa Walimu wenye maitaji maalum changamoto zao zitapatiwa ufumbuzi.
GODWIN GONDWE AIMIZA UADILIFU NA UAJIBIKAJI
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amewataka watumishi na watendaji Wilaya ya Kinondoni wawe waadilifu na wawajibikaji pia washirikiane kwenye utendaji kazi.
Habari picha na Victoria stanslaus
MENEJA TARURA KINONDONI AELEZA MIKAKATI
Meneja Tarura Kinondoni amesema Tarura Wilaya ya Kinondoni inatatuwa kelo za barabara kwa Rami na changarawe, pia tarura wanashirikiana na Tra na Idara zingine kwenye ujenzi wa barabara.
TAASISI YA JAKAYA KIKWETE YA MOYO YAFANYA KAMBI YA SIKU MBILI
WAZIRI WA VIWANDA ,BIASHARA NA UWEKEZAJI AKUTANA NA WADAU IN
Waziri Dr Ashatu Kijaji amesema Lengo la wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kukutana na Wadau wake kuweza kujadili changamoto walizonazo wafanya Biashara, wawekezaji,wenye kampuni na viwanda. Pia kufanya mabolesho ya Sera,Sheria na kanuni ili vipato vyawafanyabiashara na wananchi vikuwe.
Habari na Ally Thabiti
MSTAIKI MEA WA JIJI LA DSM APONGEZA UZINDUZI WA DUKA LA VIATU
Omary Kumbiramoto Mstaiki Mea wa Jiji la Dsm amepongeza uzinduzi wa Duka la Viatu liitwalo SPARX lililopo kata ya mchafukoge kwani Duka ililitasaidia watukupata ajira na Biashara zao zinauzwa Kwa bei nafuu.
Habari picha na Ally Thabiti
HAMAD MUSA SALUM AVUTIA WATU KUNUNUA BIDHAA ZAO
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sparx Hamad Musa Salum amesema watu wajitokeze kununua viatu vya Aina mbalimbali kwani nibei nafuu na imara.
DOKTA AIMIZA JAMII KUPIM SELIMUNDU
Dkt anaeusika na Maswala ya Selimundu amekitaka jamii kupima jenetiki zao ili kugunduwa selimundu.
Habari na Ally Thabiti
MSANII CHIBA KISMATI ATOA NENO KUUSU SELIMUNDU
Martini (Chiba Kismati) amesema Jamii iwapeleke shule watoto wenye selimundu kwani wanauwezo mkubwa mfano yeye ni msanii na mkurugenzi wa wenye taasisi Yake.
Habari na Ally Thabiti