Wednesday, 3 April 2024

DAWASA YAELEZA MAFANIKIO YA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA


Katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameweza kwa kiasi kikubwa kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kumtua mama ndoo kichwani kwa mafanikio makubwa na haya yanathibitishwa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maji Dar es Salaam Kiula Kingu amesema tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ameweza kukamilisha miradi midogo na mikubwa ya maji ambako bwawa la kidunda lenye thamani ya Bilioni 345 mradi huu umesainiwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambako bwawa hili litaweza kutoa maji kwa wingi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Pia kupitia Bwawa hili zitapatikana megawati 20 za umeme na kilometa 70 za barabara kwenda Ngerengere na uwepo wa Daraja Kubwa ambako itasaidia kukua kwa utarii, kilimo, upatikanaji wa samaki. Mradi wa Bilioni 72 ambao maji haya yatawafikia watu elfu 35, mradi wa maji mto Wami ambao gharama yake ni Bilioni 82, alafu mradi wa maji taka wa mbezi bichi wenye ukubwa wa kilometa 100.

Pia Rais Samia aliweza kutoa mashine za kuchimba visima saba kigamboni ambako imesaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji Ilala, Temeke na Kinondoni mkurugenzi mkuu wa Dawasa amesema Rais Samia amesaidia kuimalisha mifumo ya tehama ambako imesaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ukusanyaji wa mpato na kuweka kamati za usimamizi wa maji kwenye mitaa na kuwezesha kupatikana kwa ajila kwa vijana wapatao elfu 680. Amesema haya makao makuu ya Dawasa Ubungo jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment