Wednesday, 3 April 2024

SHEIKH NURDEEN KISHKI KUGHALAMIA NDOA ZA VIJANA MIA MOJA

Mkurugenzi wa Taasisi ya  Taasisi ya Al- Hikma Foundation na Mwenyekiti wa Mashindano ya kuhifadhi Quruan Sheikh Nurdeen Kishki amesema atagharamia ndoa zipatazo mia moja kuanzia utoaji wa Pesa ya Mahali, Pesa ya Ukumbi pamoja na pesa ya vyakula kwa vigezo kumi kwa muoaji awe:-

1. Awe Muislamu, 2. Awe Mkazi wa Dar es Salaam, 3. Mawalii wawe wamekubali, 4. Awe na Kazi, 5. Awe Mtanzania, 6. Awe na Akiri Timamu, 7. Awe amechumbia, 8. Ajaze Fomu, n.k.  

Amesema haya Jijini Dar es Salaam.

Habari na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment