Monday, 29 April 2024

TAASISI YA TUME YA NGUVU ZA ATOMU (TAEC) YABAINISHA MAFANIKIO CHINI YA RAIS DKT SAMIA

 


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomu (TAEC) Professor Razaro Busagala amesema kipindi cha miaka mitatu kwenye uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wameweza kujenga maabara sita miaka ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Zanzaibar, 

Ambako kiasi cha shilingi Bilioni 28.11 zimeweza kutumika kwenye ujenzi wa maabara hizo lengo la kujenga maabara hizi ni kuwezasha usalama katika sekta ya kilimo, kwenye matumizi ya pembe jeo na viwatirifu, sekta ya afya ambako kuweza matumizi sahihi na yenye ubora kwenye vifaa vya MRI, CT-Scan ambako zimewawezesha watoa huduma watoe huduma kwa usalama kwao na kwa wapokeaji huduma hizi na sekta ya uchimbaji madini.

Ambako taasisi yao imeweza kufanikiwa kwa kiasia kikubwa katika uwangalizi na usimamizi wa matumizi ya Nguvu za Atomu haya kwao ni mafanikio makubwa sana, Profesor Razaro Busagala amesema kipindi cha miaka mitatu cha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kiwango chao cha ukusanyaji wa fedha kimeongezeka ambako wamepata kiasi cha Bilioni 10.9, ukilinganisha na miaka ya nyuma walikuwa wanakusanya Bilioni 8.3 pia amewatoa hofu Watanzania na wasio Watanzania kuwa Tanzania kwenye nguvu za Atomu angani na ardhini ni salama, 

Swala la utowaji wa elimu kwa matumizi ya Nguvu ya Atomu wanatoa kwa kiasi kikubwa huku wakiwa na mipango mikakati kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu, amesema haya jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa chuo cha Utarii wakati akizungumzia mafanikio ya taasisi yao kwa miaka mitatu chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa na wanahabari mapoja na wahariri wa vyombo vya habari.

Habari Picha na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment