Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Justina Mashiba amewataka watendaji wa kata,mtaa,tarafa na wilaya kutokuwa kikwazo katika ujenzi wa mradi wa minara kwani kwani mfuko wa mawasiliano sawa kwa wote wanajenga minara 758 Tanzania ambako mpaka sasa washajenga minara 98 imekamilika na kuwashwa.
Kiasi cha bilioni68 zimeshatolewa kwenye mradi huu changamoto kubwa wanayokutana nayo kunyimwa vibali vya ujenzi, vibali vya mipango miji na ubovu wa miundombinu ya barabara. Ametoa rai kwa madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kutoa ushirikiano katika ujenzi wa minara.
Amesema haya kwenye semina na uzinduzi wa kampeni za ujenzi wa minara 758 jijini dar es salaam habari na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment