Monday, 20 September 2021

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AMUUNGA MKONO RAISI

 Merry Masanja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema katika kumuunga mkono raisi Samia Suluhu Hassan kwenye kuitangaza Utalii wa Tanzania Wizara imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo  kuboresha Mali kale,kutunzamisitu,kuingia mikataba na wasanii kwaajili ya kuutangaza vivutio vyetu na kuandaa machapisho mbalimbali pamoja na mabango.

Pia Naibu Waziri amesema kutakuwepo na makongamano na mijadala mbalbali ya kujadili namna ya kuutangaza Utalii wetu. Amewataka Wanahabari na wasanii na wadau wengine kuunga mkono juhudi hizi.

Pia Amewapongeza TFS Kwa kulinda na kutunza misty yetu. Mfano msitu wa KAZI Mzumbwe na mingineyo.

Habari na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment