Sunday, 30 June 2024

RAIS DR KIKWETE AWAPONGEZA WAANDAAJI WA MSOGA MARATHON


 Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya nne 4 Dr Kikwete anawapongoza waandaaji wa mbio  za Msoga Marathon  kwani ubunifu huu ni mzuri na unatija kubwa kwenye sekta ya Afya ambako fedha zilizopatikana zitawezesha kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo kwa kinamama wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua Na kununua  vifaa vya kuwawezesha watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa kutimia .

Rais Dr Kikwete anawatia moyo waandaaji na kuwataka kutokata tamaa na mbio hizi za Msoga Marathon  ziwe endelevu ma zifanyike kila mwaka ''amempongeza mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete na wenzake kuamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Msoga  Marathon. 

Ametoa wito kwa watu wote wawe namoyo wa kuwasaidia watu wenye uhitaji amesema haya wilayani Chalinze kata ya Msoga kijiji cha Msoga  mkoani pwani  kwenye mbio za Msoga Marathon. 

Habari picha na Ally Thabit 

TOYOTA YAJA NA BIDHAA YA KIBABE MSOGA MARATHON


 Jamal Chembera Meneja Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania LTD amewapongeza waandaaji wa Mbio za Msoga  Marathon kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia kuokoa na kunusuru vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa .Jamal Chembera amesema kampuni ya Toyota inamuunga mkono rais Dr Samia  katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ndio maana kampuni ya Toyota wameamuwa kuja na magari ambayo yanatumia nishati ya umeme .

Ivyo amewataka watanzania na wasio watanzania kununua magari kutoka Toyota  kwani bei ni mafuu,ayachafui mazingira  na ukiitaji unapata kwa muda mfupi .ametoa wito watu wasiogope teknolojia na badala yake waitumie teknolojia kama Toyota walivyoleta magari ya kisasa yanayotumia nishati ya umeme.

Habari picha na Ally Thabit 

ADERA IZENGO AFARIJIKA KUWEPO KWA MSOGA MARATHON


 Mwananchi wa Wilaya ya Chalinze Kata ya Msoga kijiji cha Msoga Mkoa wa Pwani Adera Izengo amesema msoga marathon itawakomboa wanawake wakati wa kujifungua  na itanusuru vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa aijafika .

ametoa rai kwa waandaji wa msoga marathon mbio hizi ziwezinafanyika kila mwaka kwani licha ya kupatikana kwa fedha kwaajili ya ujenzi na kuboresha  hospitali ya Chalinze pamoja na ununuzi wa vifaatiba pia mbio zinasaidia watu kufanya mazoezi ya mwili amemshukuru mhe mbunge na naibu waziri Riziwani Kikwete pamoja na waandaji wa msoga marathon  bila kuwasaau washiriki wote amesema haya wilaya ya  Chalinze  kata ya Msoga kijiji cha Msoga mkoani Pwani.

Habari picha na Ally Thabit 

MBUNGE WA CHALINZE ANUSULU VIFO VYA MAMA NA MTOTO


 Riziwani Kikwete Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri amesema wameamuwa kuleta Msoga Marathon Lengo kupata fedha kwaajili ya kununua vifaa vya kuwaifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya kutimiza miezi tisa (NJITI) .

amewashukuru watu,makampuni,taasisi, viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa kiserikali na wadau mbalimbali kwa kushiriki kwenye Msoga Marathon na kutoa michango yao mbalimbali . Kwani yeye mbunge wa Chalinze ameahidi fedha zilizopatikana zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Na amesisitiza kuwa Msoga Marathon itafanyika kila mwaka amesema haya mkoani Pwani wilaya ya Chalinze kata ya Msoga kijiji cha Msoga  kwenye mbio za Msoga Marathon .

Habari picha na Ally Thabit 

Wednesday, 26 June 2024

RAIS KIKWETE KUNOGESHA MSOGA MARATHON

 Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 wa Tanzania Dr Kikwete amepongeza waandaaji wa Msoga Marathon kwani mbio hizi zinampango wa kukusanya kiasi cha fedha milioni Mia tatu therasini ambako zitaenda kutumika kwenye kununua vifaa kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda na ujenzi wa vyumba vya kujifungulia mamawajawazito haya ni malengo mazuri ndio maana yeye anaunga mkono mbio za msoga marathon kushiriki kwenye mbio hizi na kutoa pesa na anatoa wito kwa taaasisi, makampuni,viwanda na watu binaus kushiriki na kuchangia zoezi hili amesema haya wakati akihojiwa na wasafi TV na redio.

Habari na Ally Thabit 

WAFANYA BIASHARA WAPEWA MATUMAINI

 Mwenyekiti  wa Wafanyabiashara  Martini Mbwana anawataka wafanyabiashara kufungua maduka yao kwani changamoto walizoolozesha kamati ya waziri mkuu baadhi washazifanyia kazi na vikao vinaendelea kati ya kamati ya waziri mkuu na Wafanyabiashara lengo wafanya biashara wasitishe kufunga maduka yao.

Mpaka sasa mikoa ambayo wafanyabiashara wamefunga maduka yao .Arusha,Mbeya,Mwanza,Tanga,Mtwara na dar es salaam.  Mwenyekiti wa wafanyabiashara  Martini Mbwana  amesema hii inaleta athari kwa uchumi wa tanzania na uchumi wa mtu mmojammoja ivyo anatoa rai kwa wafanyabiashara  kufungua maduka yao kwani hata mkuu wa mkoa wa dar es salaam CHALAMILA ameimiza hekima na busara itumike na si kufunga maduka kwani kitendo cha kufunga maduka ni kukiuka maagizo na maelekezo ya waziri mkuu Amesema haya jijini 

Habari na Ally Thabit 

Tuesday, 25 June 2024

PROF LADSLAUS MNYENE ATOASIRI NZITO ELIMU KIDIGITALI


 Mkurugenzi wa  Idara ya Sayansi na Teknolojia Wizara ya Elimu Prof Ladslaus Mnyane  amesema Utoaji elimu kwanjia ya kidigitali kuanzia elimu ya Awali ,msingi ,secondary na vyuo vikuu itasidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufundishwa masomo kwa muda mfupi wakiwa wengi,walimu watafundisha wanafunzi kwa uchache wao,itapunguza gharama kwa serikali kwa kutoajili walimu wengi.

Katika mabadiliko ya kiteknolojia duniani tanzania tukiwafundisha wanafunzi kwa njia za kidigitali itawawezesha wanafunzi baada ya kumaliza shule na vyuo vikuu watakuwa wameshabobea katika matumizi ya kidigitali . Hivyo ufanisi utaongezeka kwa kiasi kikubwa katika utendaji kazi kwenye sekta mbalimbali mfano kwenye sekta ya madini,sekita ya kilimo,sekta za maji na sekta zinginezo.

Prof Ladslaus Mnyane amesema lengo la kutoa elimu kwa njia ya kidigitali kuwezesha watanzania kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ya sasa na ya baadae,pia wanatarajia serikali na watu binaus kutekeleza mpango huu kwa vitendo  ifikapo mwezi7/2025  .Swala la kujumuisha na kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu ili wapate elimu kwa nia ya kidigitali ni jambo muhimu na linatija kwa tanzania amesema haya jijini dar es salaam kwenye mjadala wa kupokea maoni kwa wadau wa elimu  kwa namna gani ya kukamilisha mpango wa kutoa elimu kwa njia ya kidigitali.

Habari picha na Ally Thabit 

ROJERS FUNGO WA TARSIWAKUTANA NA WAANDISI WA BARABARA

 Meneja wa taasisi ya TARSI  Rojers Fungo Taasisi yao imeamuwa kufanya semina ya siku tano5 na Waandisi wa barabara pamoja na Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu  na watu wa serikalini lengo kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kudhibiti ajali za barabarani . Semina hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho ya seranq maboresho yakutumia teknolojia za kisasa katika utengenezaji wa barabara.

Rojers Fungo ametoa wito kwa washiriki wa semina hii wazingatie mafunzo na watendee kazi watakayoyapata kwenye semina .

Habari na Ally Thabit 

Monday, 24 June 2024

KATIBU WA MAY SALA AJA NA MUAROBAINI WA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA

 Amadi Sefu Katibu wa May Sala Mbio za Pole ili watu waepuke kupata magonjwa yasiyoambukiza ni vyema wakajiunga na vikundi vya mbio za pole .pia vikundi vya pole vinajenga umoja,mshikamano,kudumisha amani na kuchochea ukuaji wa uchumi amesema haya kwenye viwanja vya barafu jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

WATU WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU

 Mratibu wa Damu Salama Wilaya ya Kinondoni anawataka watu wawewanachangia damu mara kwa mara kwani damuinasaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto amesema haya kwenye viwanja vya barafu kaika bonanza lililoandaliwa na kikundi cha barafu wilaya ya kinondoni .

Kwenye bonanza ili watu wamechangia uniti 22 za damu .

Habari na Ally Thabit 

MWANDISI MAHAMUDU ABAINISHA CHANGAMOTO ZA BARABARA

 Mwandisi Mahamudu amesema Katika Barabara za tanzania zinakabiliwa ba changamoto zifuatazo ,Mabadiliko ya tabia ya nchi kwani barabara nyingi za tanzania zimepata athari kubwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, sera za nchi na uhaba wa fedha. Amesema haya na waandisi wa barabara jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

CHAMA AWAVULUGA WANACHAMA WA SIMBA

 Mchezaji wa Kulipwa Kutoka Zambia Chama amewavuluga na kuwachanganya Mabosi,wanachama,wapenzi na viongozi wa Simba baada ya kufanya maamuzi ya kujiunga na timu ya Yanga.

Habari na Ally Thabit 

Sunday, 23 June 2024

 MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ,AWAONYA NA KUWATADHALISHA WAFANYA BIASHARA

ALBART CHARAMILA , amewataka wafanya biashara wa Kariakoo na Wafanyabiashara kwa Ujumla waache mara moja mpango wao wakutaka kugoma kufungua Maduka kwani kufanya hivyo ni kukiyuka sheria , kanuni , na Taratibu za Nchi kwani madai waliyoyatoa mbele ya Waziri mkuu ,yamefanyiwa kazi kupitia wizara ya fedha , wizara ya viwanda na Biashara na Taasisi zingine za Serekali . swala la kodi ya VAT na Service Review , inafanyiwa kazi kupitia wabunge kila mtumishi wa Serekali anamadai ya serekali kama wao wafanyabiashara lakini hawajachukua maamuzi ya Mgomo .

Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewataka wafanya biashara kuwasilisha serekalini fedha za kodi wanazokusanya kwa wezao amewataka wafanya biashara kutokubali kutumika na wana Siasa ili wagome , na badala yake waendelee kufanya biashara zao ,amewatoa hofu wafanya Biashara wote ,

Soko lililoungua la Kariakoo lilojengwa na Rais Dr. Samia suluhu Hassani  kwa kiasi cha fedha Bilioni 28, tena fedha za kodi Watanzania , litafunguliwa karibuni na Rais Dr Samia na kila mmoja atapata kizimba au Duka la kuuza Bidhaa zake katika soko hilo.

kikubwa mtu afuate sheria na Taaratibu za kuingia katika Soko hilo ametoa wito kwa wana Dar es salaam kutoshabikia wa kushadadia Mgomo wa wafanya biashara na waache ,kusasmbaza Jumbe za Mgomo

Amesema haya jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari,


 WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO MATOKEO YA SENSA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mwl , Kassimu Majaliwa , amezitaka ASASI ZA KIRAI , Watafiti ,Jumuhia za Kimataifa , Wakuu wa Mikoa ,Wakurungezi , Wakuu wa Wilaya  , Katibu tawala na watumishi wa Serekali watumie Takwimu za Sensa zilizofanyika mwaka 2022 wanapoitaji kufanya mipango yao kimaendeleo .

Wizara ya Fedha ya Zanzibar na Tanzania bara bajent zao walizopanga wametumia Takwimu za Sensa , naye kwa upende wake Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar , AHMED SELEMAN ABDULLA amewashukuru wafanyakazi katika ofisi ya Rais ya Takwimu kwa kufanya sensa ya Mwaka 2022 kwa Digitar zaidi . amemuakikishia waziri mkuu wa Tanzania kuwa serekali ya zanzibar itatumia matokeo ya sensa kufanya mipango yao ,huku waziri wa muungano , Dr SELEMAN JAFO ,amesema Sensa ya mwaka 2022 ilikuwa na mafanikio kwa kuwa ilizingatia muungano wa Tanzania .

Amesema haya wakati wa uzinduzi wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, ya kimografia ,kijamii ,kiuchumi  na kimazingira jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa wa mikutano wa kimataifa .

Habari Picha , Ally Thabiti




Saturday, 22 June 2024

KISIEL WAMBURA AIPONGEZA TENMET


 Kisiel Wambura  Mwanachama wa TENMET wanaipongeza na Kuishukuru TenMet kwa ushirikiano na michango wanayoitoa katika kuendeleza harakati za kuwakomboa watoto kwenye sekta ya elimu. Kisiel Wambura wanapaza sauti kwa jamii ya kuimiza watoto wenye ulemavu kupelekwa mashuleni kwaajili ya kupata elimu pia wanafanya uchechemuzi kwa serikali ili itengeneze miundombinu rafiki na wezeshi mashuleni ili watoto wenye ulemavu  wasome kwa uhuru na kujiamini amesema haya jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Friday, 21 June 2024

BANK YA NBC NA TRC WAINGIA MAKUBALIANO


 Kama Inavyoonekana Picha Mkurugenzi  wa Trc Masanja Kadogosa akitiliana saini na kiongozi wa Bank ya Nbc kwaajili ya mashilikiano ya kuwasafirisha wanariadha Nbc kuelekea Dodoma. 

Habari picha na Ally Thabit 

NBC KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO KWA KUSHIRIKIANA NA TRC


 Kiongozi wa Bank ya Nbc wameingia Makubaliano na Shirika la reli tanzanzania (TRC) lengo ni kuwasafirisha wanarihadha na washiriki wote wa mbio za Nbc Marathon zitakazo fanyika jijini Dodoma tarehe 28 julai 2024 ambakoa fedha zitakazopatikana kupitia mbio hizi zitatumika kutoa Chanjo ya kansa ya shingo ya mlango wa kizazi kwa wanawake na pesa zingine zitapelekwa kwenye taasisi ya Mkapa ambako pesa hizi zitatumika kuwasomesha wakunga lengo wapate ujuzi mzuri wa kuwazalisha wakina mama kiutaalam ambako itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua amesema haya jijini dar es salaam kwenye kituo cha tren ya umeme (SGR)

Habari picha na Ally Thabit 

MKURUGENZI WA TRC AELEZA TIJA ZA SAFARI YA RAIS DR SAMIA

 

Masanja Kadogosa Mkurugenzi  wa Trc amesema tiara za rais Dr Samia zina umuhimu na faida kubwa kwa taifa letu la tanzania kwani ziara hizi zinasaidia kwa kiwango kikubwa kukuwa kwa uchumi wa tanzania,kupatikana kwa teknolojia mpya za kisasa kwenye nyanja mbalimbali ambako teknolojia hizi zinaraisisha utendaji kazi ,tiara zinadumisha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya tanzania na mataifa mengine,inakuza dipromasia, inawezesha kupatikana kwa maarifa mapya na utaalam mbalimbali.

Mkurugenzi  wa Trc Masanja Kadogosa ameishukuru serikali ya tanzania kwa kuweza kumchagua kuwa Mkurugenzi  wa Trc kwani ameweza kuifufua reli  2019 kwa kushirikiana na wenzake na ameweza kuusimamia mradi wa SGR kwani reli inamkumbusha 1994 wakati akiwa kidato cha 5 moshi  yeye na wenzake walivyokosa usafiri wa tren wakati wa likizo ya kurudi majumbani mwao ndio maana Mkurugenzi wa Trc Masanja Kadogosa anaipongeza na kuishukuru serikali kwa kuwekeza kwenye reli. Amesema haya kwenye kituo cha SGR jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Thursday, 20 June 2024

RAIS DR SAMIA KUNOGESHA TAMASHA LA UTAMADUNI SONGEA


 Mratibu wa Tamasha la Utamaduni na Balozi  wa Utalii Kutoka kwa Kampuni ya DRUM BEATCARNIVAL (TZ) LIMITED  kwa kushirikiana  na Wizara ya Utamaduni na Michezo .Lydia amesema rais Dr Samia atakuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la utamaduni litakalo fanyika mkoani Ruvuma wilaya ya Songea eneo la majimaji tarehe 20/7/2024 Tamasha litaanza na kumalizika tarehe 27/7/2014.

Lengo la tamasha hilikukuza utamaduni wetu,utalii , mila na desturi. Katika tamasha hili kutakuwa na mbio za kilometa20,kilometa 5,kilometa 10,mbio za magari na bayskeli .Mratibu Ridia amesema huu ni mwaka wa tatu wa tamashaili na ushiliki umekuwa mkubwa pia Tamasha hili litakuwa linafanyika kila mkoa.

Katika Tamasha hili la utamaduni rais Dr Samia  akifungua Tamasha hili kutakuwepo na makongamano mbalimbali amesema haya kijiji cha makumbusho jijini dar es salaam
Habari picha na Ally Thabit .

Tuesday, 18 June 2024

KAMISHINA WA FEDHA AWAPA MAAGIZO MAZITO CRDB

 Chares  Mwamwaja ameitaka Crdb bank Kupitia kampuni yao ya bima watoe elimu ya fedha na bima  kwa jamii nchi nzima hususani kwa watu wa vijijini pia waongeze ushilikiano kwa kampuni zingine za bima  na waongeze ubunifu kwenye huduma zao za fedha na bima bila kusaau kampuni ya bima crdb itoe huduma zao kwenye nchi jirani mfano Kenya ,Uganda,Kongo,Burundi na nchi zingine pia izingatie miongozo,sera,kanuni na sheria ya tanzania amesema haya kwenye uzinduzi wa kampuni ya bima Crdb.

Habari na Ally Thabit 

CRDB YAZINDUA KAMPUNI YA BIMA

 Mkurugenzi  Mkuu  wa Bank ya CRDB Abdli Majidi Msekela ameamuwa kuja kampuni tanzu ya bima lengo kuokoa maisha ya watanzania na kulinda Mali zao ,ameaidi kushilikiana na kampuni mbalimbali nchini lengo kutoa huduma bora na zenye ufanisi . Pia wanamipango kampuni ya bima kufika nje ya nchi amesema haya jijini Dar es salaam  kwenye uzinduzi wa kampuni ya bima CRDB.

Habari na Ally Thabit 

Saturday, 15 June 2024

WAFANYABIASHARA WAJAWA NA MATUMAINI NA RAIS DR SAMIA


 Mwenyekiti  wa Umoja wa Wafanyabiashara amesema licha ya changamoto wanazopitia ikiwemo mizigo yao kuzuiliwa na tra na kukamatwa na jeshi la polisi mara kwa mara kwao imekuwa ni kilio kikubwa lakini kupitia kikao chao chini ya mkuu wa wilaya ya Ilala wanaamini kelo na chanagamoto walizompatia zitafanyiwa kazi na kutatuliwa na rais Dr Samia kwani awana imani na matumaini na waziri mkuu Kassim Majaliwa kwakuwa aliowaaidi eneo la mnazi mmoja alijatekelezwa hata moja ivyo awataki kumuona wala kusikia maneno yake.

Habari picha na Ally Thabit 

PWANI YAWAFITA MACHOZI WATU WENYE UALBINO


 Kahimu Katibu Tawara wa Mkoa wa Pwani Mkoa wa pwani watu wenye ualbno wanawezeshwa kikamilifu katika shughuri mbalimbali za kiuchumi wa kupewa mikopo,masoko ya kibiashara lengo wajikwamuwe kiuchumi na ili wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mkoa wa pwani swala la ulinzi na usalama kwa watu wenye ualbino wanalifanyia kazi kikamilifu ndio maana amna matukio ya kukatwa wala kuuliwa kwa mtu mwenye ualbino na kamwe aitotokea amesema haya kwenye kongamano la watu wenye ualbino  lililofanyika mkoa wa pwani wilaya ya kibaha.

Habari picha na Ally Thabit 

KILIO CHA WAFANYA BIASHARA CHAPOKELEWA


 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo anawataka Tra kutowasumbua wafanya biashara wa kariakoo na jeshi la polisi waache kuwakamata wafanyabiashara na kutowabambikia kesi pia anawaakikishia wafanyabiashara kuwa changamoto walizo nazo anamfikishia mkuu wa mkoa wa dar es salaam, waziri mkuu,makamu wa rais na rais mwenyewe ivyo anawataka wafanyabiashara kutogoma na wala wasifunge maduka .

Habari picha na Ally Thabit 

MWENYEKITI WA TGNP APAZA SAUTI BAJETI KUU YA SERIKALI

 Mama Gema Mwenyekiti  na Mwanaharakati wa Tgnp anasikitika kwa kiwango kikubwa kwa bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa na waziri wa fedha Dr Mwigulu Mchemba aijazingatia wala kuwekwa mambo ya kijinsia wala amna msamaa wa kodi kwenye taulo za kike. Nivyema Wabunge na serikali wawe wanaweka kipaumbele kwenye maswala ya kijinsia, Mwenyekiti  wa bodi wa Tgnp amesikitika kwa kiwango kikubwa utoaji wa maoni kuhusu dira mpya ya maendeleo  ya miaka 50 ijayo watu wenye ulemavu awajapewa mazingira rafiki na wezeshi namna ya kutoa michango yao ya maoni . 

Ivyo ni Vyema Serikali Kuweka Mazingira  ambayo watu wenye ulemavu  watashiriki katika kutoa maoni yao na bajeti kuu ya serikali awajawazingatia watu wenye ulemavu  ,ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wakae pamoja ili wapaze sauti zao kwa serikali kwa lengo la kuwekewa mazingira  rafiki na wezeshi katika kutoa maoni yao katika kutoa maoni yao kwenye dira mpya ya taifa ya miaka 50 ijayo.amesema haya makao makuu ya Tgnp mabibo jijini Dar es salaam  kwenye ufatiliaji wa usomwaji wa bajeti kuu ya serikali.

Habari na Ally Thabit 


Wednesday, 12 June 2024

MAGNETIC Y SWAI APAZA SAUTI DHIDI YA WATU WENYE UALBINO

 

Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Watu Wote Sawa(WAWOSA)  iyopo Dodoma Magnetic Y Swai anaitaka serikali kufanya mabadiliko ya sera,sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo dhidi ya watu wanaofupisha maisha ya watu wenye ualbino Nawanaokata viungo vya watu wenye ualbino  lengo watu wenye ualbino waishi kwa amani amesema haya mkoani pwani wilaya ya kibaha kwenye kongamano la kuusu uelewa kuusu watu wenye ualbno. 

Habari picha  na Ally Thabit 

MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO ASIKITISHWA NA VITENDO VYA UKATILI KWA WATU WENYE UALBINO

 Kapole Makamu Mwenyekiti  wa Chama cha Watu wenye Ualbino (TAS) tangu mwaka 2006 mpaka Leo 2024 vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino vimezidi kushika kasi na kupelekea watu wenye ualbino kukosa amanita nchini tanzania  amesema haya kongamano la uwelewa kuusu ualbino mkoani pwani wilayani kibaha.

Habari picha na Ally Thabit 

IFIKE MWISHO UONEVU KWA WATU WENYE UALBINO

 Mwenyekiti  wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Taifa (TAS) Godfrey Moler anaitaka serikali kukomesha mala moja uonevu,ukatwaji wa viungo na mauaji kwa watu wenye ualbino kwa kuwakamata watu wanaotekeleza vitendo hivi. Huku akiipongeza serikali kwa kazi na jitihada wanazozitoa amesema haya mkoani Pwani wilaya ya kibaha kwenye kongamano la watu wenye ualbno taifa 

Habari picha na Ally Thabit 

SHIVYAWATA YALAANI UKATILI DHIDI YA WATU WENYE UALBINO

 Katibu Mkuu wa Shivyawata Lubago amesema sheria kali iwekwe kwa wale ambao wanaowakata viungo na kuwauwa watu wenye albino pia amewataka watu wenye ulemavu  washiliki kutoa maoni kwenye dira mpya ya maendeleo ya  taifa  amesema haya kwenye kongamano la uelewa kuusu watu wenye ualbino mkoa wa pwani wilaya ya kibaha.

Habari na Ally Thabit 

Tuesday, 11 June 2024

TGNP WAITAKA SERIKALI KUTENGA BAJETI YENYE MLENGO WA KIJINSIA

WILFRED KULWA Afisa mtafiti na mchambuzi wa maswala ya kiuchumi na jinsia TGNP amesema serikali itenge majeti yenye mlengo wa kijinsia kwenye wizara zote ili kuondoa ombwe kwenye maswala ya kijinsia  pia TGNP inaofu kuwa bajeti ya mwaka huu kiasi kikubwa cha fedha kitaelekezwa kwenye maswala ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao hivyo wanaitaka serikali fedha zielekezwe katika kutoa elimu kwa wanawake ili wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uwongozi wa wenyekiti wa serikali za Mitaa, Ubunge, Udiwani na Urais ili wawe na fursa ya kufanya maamuzi makubwa vilevile bajeti hii pesa nyingi zitaelekeza kwenye maandalizi ya dira mpya ya maendeleo ya Taifa ya miaka 50 ijayo.

TGNP yaitaka serikali ihusishe makundi maalumu katika utowaji wa maoni ya dira mpya ijayo kwani dira tuliyonayo aijazingatia makundi maalumu na mlengo wa kijinsia Wilfred Kulwa ameipongeza serikali kwenye wizara ya afya kwa kuweza kununua Ambulance kwani zitaokoa maisha ya mama na mtoto kipindi wanavyokwenda hospitali kujifungua swala la kuongeza muda wa mapunziko wakati anapojifungua mtumishi wa serikali ni jambo zuri na serikali kutenga fedha kwaajili ya bima za afya kwa wote ni jambo zuri.

Kwa upande wa wizara ya elimu serikali ifanye maboresho kwenye sera ya elimu kwenye upande wa matundu ya vyoo kwani sera iliyopo aioneshi mlengo na maitaji ya kijinsia kwenye matundu ya vyoo ambapo kuna ombwe kubwa kwa wanafunzi wa kike kupata idadi chache kwa matundu ya choo ikilinganisha na wanafunzi wa kiume, swala ya elimu ya amali ni muhimu ila serikali itenge fedha nyingi kwa ajili ya mafunzo kwa walimu ili kuwepo na mlengo na maitaji ya kijinsia kati ya mwalimu na mwanafunzi, huku TGNP wakiipongeza serikali kwa kuweza kuongeza fedha ya mikopo kwan elimu ya juu.

Bwana Wilfred Kulwa amesema wizara ya kilimo iyakikishe mladi wa BBT iweke mgawanyo wa kijinsia katika utoaji wa mbegu yatilifu na mikopo ya kilimo iwafikie wanawake, ametoa wito kwa serikali kuhakikisha mikopo inayokopwa na serikali iwe ya masharti nafuu na isiwe na vikwazo vigumu ili isituletee matatizo kama mikopo ya miaka ya nyuma japokuwa deni la taifa ni imilivu.

Amesema haya makao makuu ya TGNP Mabibo jiji Dar es Salaam nilipofanyanae maojiano.


Habari Picha na Ally Thabiti

Sunday, 9 June 2024

TGNP YAMGUSA KITIRA MKUMBO


 Waziri wa Mipango na Uwekezaji  Prof Kitira Mkumbo amesema tgnp inafanya kazi kubwa ya kupinga ukatili wa kijinsia na kutaka mgawanyo wa rasilimali pamoja na kutokomeza mira na destuli potofu. Waziri Kitira Mkumbo ameiakikishia tgnp na watanzania kuwa dira mpya ya maendeleo  ya miaka 50 ijayo itaweka ,itazingatia na kusimamia maswala haya yote muhimu bila kusaau haki ya kuishi,utawarabora ,misingi ya utu na mengineyo amesema haya chuo kikuu mlimani kwenye kongamano la dira mpya ya maendeleo  miaka 50 ijayo nilipofanya nae maojiano.

Habari picha na Ally Thabit 

CUF YATOA MAAZIMIO MAZITO


 Mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi Cuf Prof Haluna Lipumba kupitia baraza kuu la uongozi la  taifa kwenye chama cha Cuf wanaitaka serikali  kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi wa serikali ya mtaa na uchaguzi mkuu kama walivyokubaliana kwenye vikao vya meridhiano,kuwepo na mabadiliko ya katiba kwenye kipengere cha mgombea binausi,wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili wapate haki ya kuchagua na kuchaguliwa . Amewataka viongozi wavyama vya siasa waache rugha na vitendo vya kuvunja na kuugawa muungano wetu,pia amewataka vijana wa chama cha cuf kuanzisha uamsho wa jino kwa jino kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na kuelekea uchaguzi mkuu.

 Cuf wanaitaka serikali kubolesha mfuko wa mahafa na itoe tasmine ya matatizo yaliotokea kwenye bwawa la mwalimu nyerere vilevile kuangalia namna ya kuweza kupunguza fedha za deni la taifa kwani limekuwa kubwa ambako zaidi ya tilioni 70 tanzania inadaiwa .amesema haya makao makuu ya chama cha cuf jijini daer es salaam  eneo la buguruni.

Habari picha na Ally Thabit 

NURSE MBOBEZI WA MAGONJWA YA SARATANI NA MATIBABU YA TIBA SHUFAA AMPONGEZA RAIS DR SAMIA


 Anastasia Giles Mitema katika huduma ya tiba shufaa inasaidia wagonjwa kwa kiasi kikubwa katika Hospitali ya Oshenroad Rais Dr Samia amewezesha kwa kiasi kikubwa kwenye hospitali hii kwa kutoa fedha pamoja na vifaa tiba .

Habari picha na Ally Thabit 

KATIBU AAHIDI USHIRIKISHWAJI WATU WENYE ULEMAVU DIRA MPYA YA MAENDELEO MIAKA 50


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji Tausi ameahidi kushirikisha kundi la watu wenye Ulemavu wa aina zote kwa kuweka mazingira wezeshi kwao.  lengo watoe mchango wa dira mpya ya maendeleo miaka50 ijayo.

Habari picha na Ally Thabit 

TGNP ELIMU WANAYOITOA IZINGATIWE KUELEKEA DIRA MPYA YA MAENDELEO YA 20250




 Zito Kabwe anaitaka Wizara ya Mipango na Uwekezaji watumie  maswala ambayo Tgnp wanayopigania ili yawepo kwenye jamii ikiwemo Mgawanyo wenye usawa wa rasilimali za nchi,Mgawanyo wa kazi wenye usawa kwa wanaume na wanawake ,haki ya kumiliki ardhi I've yenye usawa kati ya wanaume na wanawake kwani wanawake awanafursa kumuliki ardhi nchini tanzania ivyo kupitia dira hii mpya ya maendeleo ya miaka 50 haya yakiwekwa maswara ya usawa wa kijinsia yatapiga hatuwa kwa kiasi kikubwa ,amesema haya chuo kikuu cha mlimani kwenye kongamano ya dira mpya ya maendeleo nilipofanya nae maojiano. 

Habari picha na Ally Thabit 

WAFANYA BIASHARA WAMUONYA NA KUMTAADHARISHA KAMISHINA MKUU WA TRA


 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wafanyabiashara Peter Mbilinyi anamtaka kamishina mkuu wa tra tanzania aache kuwakumbatia wanasiasa mfano kuna mwanasiasa amegawa majiko ya gesi kwa wafanya biashara ambao awalipi kodi kariakoo pia amewataka viongozi wa Halmashauri ya Ilala waache kuwatumia wafanyabiashara ambao awalipi kodi.

Peter Mbilinyi amewataka wafanya biashara wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano utakao fanyika ukumbi wa Anatogo tarehe 13/6/2024 lengo kujadili mambo waliokubaliana na waziri mkuu na kupitia changamoto zilizokuwa zinawakabili wafanya biashara kipindi cha mgomo.

Ameitaka serikali kuwasajili wafanya biashara elfu 20000 waliopo kariakoo ili waweze kulipa kodi, vilevile serikali ikusanye kodi bandarini ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara. Umoja wa wafanyabiashara kariakoo unawafanyabiashara elfu 30000 ambao wamesajiliwa .

Habari picha na Ally Thabit 

Thursday, 6 June 2024

CHAMA CHA WAFANYAKAZI CHAMPONGEZA RAIS SAMIA


 Naibu Katibu Mkuu wa Shilikisho la vyama vya wafanyakazi Saidi amempongeza rais Dr Samia  kwa kuboresha maslai ya wafanyakazi nchini tanzania mfano malipo ya fedha za wafanyakazi vyeti feki,malipo  ya malimbikizo ya madeni ya wafanya kazi ,Ongezeko la misheara kwa wafanyakazi mwaka jana ,Ongezeko la ajira ,kupandishwa kwa maharaja kwa wafanyakazi, malekebisho ya kikokotoo kwa wastafu .

Kipindi cha miaka mitatu rais samia amekuza ushilikiano na mausiano kati ya wafanya kazi na serikali amesema nilipofanya nae maojohano makao makuu jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA AWAPA NENO WAHITIMU WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA

 Dr Philp Mpango Makamu wa rais wa Tanzania amewataka wanafunzi waliohitimu kwenye chuo cha Utumishi  wa Umma wazingatie waliofundishwa kwenye utendaji wao wa kazi pia wawe Wazalendo na watangulize maslai ya taifa mbele huku akiwataka wawe watu wenye uweredi,uadilifu,wazingatie maadili na wawe na hofu ya mungu katika utumishi wao.

Makamu wa rais ameupongeza uongozi wa chuo cha utumishi  wa umma kwa mafunzo na elimu bora wanayotoa kwenye chuo Chao na namna wana vyowafundisha wanafunzi hawa nidhamu,maadili,uzalendo ,utendaji wa haki,kuepuka rushed na kuwana hofu ya mungo. Amesema kwenye maafari ya wahitimu wa chuo cha Utumishi  wa Umma kwenye ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es. 

Habari na Ally Thabit 

LATRA CCC YAWAFIKIA WATU WENYE ULEMAVU


 Daud Goodluck Daudi Executive Secretary amesema elimu inayotolewa na Latra ccc dar es salaam inazingatia kwa kiasi kikubwa makundi ya watu wenye ulemavu  mbalimbali mfano kuna vipeperushi vya maandishi ya nukta nundu kwaajili ya watu wasio ona pia kwenye usafili wa mabasi ya mwendo kasi kwenye  mabasi kuna viti vya watu wenye ulemavu   wanawake wajawazito na wazee .

pia kwenye vituo vya mwendo kasi miundombinu ni rafiki na wezeshi kwa makundi yote hata watoa huduma wake wana uwezo wa kuwahudumia watu wenye ulemavu na makundi mengine. LATRA CCC dar es salaam inatoa elimu kwa madereva bodaboda,bajaji na daradara ili kuepukana na ajali .

Amekipongeza chuo cha NIT,CBE kwa mafunzo wanayoyatoa ya udereva kwa madereva pia ameipongeza Hospitali ya taifa  muhimbili kwa kuingia makubaliano na chuo cha taifa cha usafilishaji NIT kwani ushirikiano  wao utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguwa kwa ajali nchini .

Habari picha na Ally Thabit 

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WAAHIDI MAZITO

Loy Mangura Mwanafunzi aliyehitimu Chuo cha Utumishi wa Umma amesema kwaniaba ya wanafunzi wenzake elimu walioipata kutoka chuoni kwao wataitumia vizuri kwaajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla .Pia watazingatia utendaji wa kazi wenye maadili ,uzarendo,uwaminifu na uchapakazi hodari ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapa fursa mbalimbali watoto wa kike ikiwemo fursa ya elimu,ajira kwa wanawake ili waweze kujikwamuwa kiuchumi .amesema haya jijini dar es salaam kwenye maafari ya wanafunzi wa chuo cha utumishi wa umma.

Habari picha na Ally Thabit 
 

Wednesday, 5 June 2024

TGNP YAPONGEZWA NA KAMISHNA WA UHAMIAJI TANZANIA


 Dr. Anna Makakala Kamishna Jenerari wa Uhamiaji Nchini Tanzania ameipongeza na kuishukulu TGNP kwa kazi kubwa wa uchechemuzi katika jamii kwani wanawake wengi kupitia TGNP wameweza kujikwamua kiuchumi kwa kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara na uongozi ndiyo maana jeshi la uhamiaji nchini Tanzania linawaunga mkono wanawake wanapokuwa wamekwama mipakani wanapopeleka biashara zao nchi za jirani.

Kamishna wa Uhamiaji wamewatia moyo TGNP kwa kazi yao mzuri wanayoifanya hivyo amewataka wanawake nchini kutokata tamaa na kubweteka na badala yake wachangamkie fursa mbalimbali ikiwemo kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024 na uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2025 lengo waweze kushika nafasi kubwa za maamuzi ili waweze kutatua changamoto zinazo wakabiri kwani wanawake wanauwezo mkubwa wa kuongoza mfano Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassani ambae ni mchapa kazi mzuri na ameweza kuifungua Tanzania kimataifa na kukuza Diplomasia kiuchumi ametoa wito kwa jamii na wanasiasa kuacha mila na desturi potofu na kandamizi zidi ya wanawake na kuondoa mfumo dume kwenye vyama vya siasa na katika jamii pindi wanawake wanapogombea nafasi za uwongozi na wawepe ruhusa kwa kugombea kwenye uwongozi, amesema haya jijimi Dar es Salaam nilipofanyanae maojiano.

Habari picha na Ally Thabiti 

LATRA YATOA VYETI KWA MADEREVA 1518


Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa Latra Habibu Suluhu lengo la kuwapa vyeti madereva wa mabasi na maroli ili waweze kutambulika Tanzania na nje ya Tanzania wanapokuwa wanafanya shughuli zao za usafirishaji kwa mwaka jana walitoa mafunzo kwa madereva 999 ambako kwa mwaka huu idadi imeongezeka jumla ya madereva waliopewa mafunzo 3000 na waliohitimu ni 1518 ambako jumla idadi yao kwa mwaka jana na mwaka huu ni 2517.

Pia mkurugenzi mkuu mtendaji wa Latra amesema madereva wanafundishwa kutambua watu wenye ulemavu pamoja na kuheshimu arama zao amesema haya jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji vyeti vya madereva 1518.

Habari Picha na Ally Thabiti. 

 

SCHAOLASTICA PEMBE MRATIBU WA TAASISI TANZANIA COALITION AGAINST CHILD LABOUR APIGA VITA UTEKWAJI NA UKATWAJI WA VIUNGO VYA WATU WENYE ULEMAVU


Scholastica Pembe Mratibu wa Taasisi Tanzania Coalition Against Child Labour kuchukua hatua kali zidi ya vitendo viovu na vibaya wanavyofanyiwa watu wenye Ualbino pia amelitaka jeshi la polisi nchini Tanzania kuwatafuta na kuwakamata wale wote waliomteka mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novati mwenye miaka miwili na nusu wa mkoani Kagera Tanzania.

Pia Jeshi la Polisi lifanye jitihada za makusudi za kumtafuta mpaka wampate mtoto mwenye Ualbino mtoto huyu Asimwe Novati. Scholastica Pembe Mratibu wa Taasisi Tanzania Coalition Against Child Labour ametoa wito kwa jamii wahache mila na desturi potofo na kandamizi zidi ya watu wenye Ualbino pia ametoa rai kwa waganga wa kienyeji kuacha ramli chonganishi.

Habari Picha na Victoria Stanslaus.

EXECUTIVE DIRECTOR CLEMENCE MWOMBEKI WA TAASISI YA DOOR OF HOPE TO WOMEN AND YOUTH TANZANIA (DHWYT) ABAINISHA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA AJIRA KWA WATOTO


 Executive Director Clemence Mwombeki wa Taasisi ya Door of Hope to Women and Youth Tanzania (DHWYT) amesema lengo la kukutana kwao kufanya maboresho ya sera, sheria, kanuni na taratibu za ajira zidi ya watoto kwani watoto wengi wameajiliwa kwenye sekta binafsi na kupelekea kukosa haki zao za kimsingi ikiwemo elimu.

Richa ya serikali kuingia mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa lakini bado wimbi la ajira za watoto zimekuwa kubwa sana kwenye sekta mbalimbali, migodini, kwenye kilimo, masokoni, viwandani na maeneo mengineyo hata hivyo wanaharakati na wadau wanaopinga ajira za watoto wameweza kundi la watoto wenye ulemavu pamoja na wazazi na walezi wenye ulemavu ili nao waondokane na mazira ya ajira kwa watoto.

 Executive Director Clemence Mwombeki wa Taasisi ya Door of Hope to Women and Youth Tanzania (DHWYT) ameraani vikali na kukemea vitendo vya utekwaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino ameitaka serikali kuwatafuta na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika kumteka mtoto mwenye Ualbino miaka miwili na nusu Asimwe Novati wa mkoani Kagera Tanzania pia serikali kupitia vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na jeshi la polisi lifanye jitihada za makusudi za kumtafuta mtoto huyu mwenye Ualbino Asimwe Novati. Amesema haya Jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabiti.

CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO MKOA WA DAR ES SALAAM KUONANA NA RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Mkoa wa Dar es Salaam Gabriel Aluga amesikitishwa vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye Ualbino na amelaani vikali kutekwa kwa mtoto mwenye Ualbino mwenye miaka miwili na nusu ASIMWE NOVAT wa mkoani Kagera Tanzania.

Hivyo kwa pamoja watu wenye Ualbino wanaomba kuonana na Rais Kdt Samia Suluhu Hasani ili wafikishe kilio chao  na mateso wanayopa watu wenye Ualbino, mwenyekiti amemtaka spika wa bunge la Tanzania pamoja na wabunge kupitia bunge linaloendelea hivi sasa watoe tamko la kuraani na kukemea utekwaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino pia mwenye amesema tarehe 12/06/2024 wilaya kibaha mkoani Pwani kutakuwa na kongamano kubwa la watu wenye Ualbino.

Habari Picha na Ally Thabiti

 

CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO TANZANIA (TAS) CHA KEMEA VIKALI UTEKWAJI WA WATU WENYE UALBINO

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Taifa Godfrey Molel ameitaka serikali kuwakamata na kuwachukulia hatua kari watu walio mteka mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka miwili na nusu anaejulikana kwa jina la Asimwe Novat mkoani Kagera wilia ya Karagwe ambae mpaka sasa mtoto huyo ajulikani alipo.

Hivyo chama cha watu wenye ualbino wanavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha mtoto huyu anapatikana akiwa hai huku chama hiki kikimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Kamilius Wambura waende wakaweke kambi ili wawasake watu waliomteka mtoto Asimwe Novat, hata hivyo chama hiki kinamuomba Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atoe tamko la kukomesha na kuraani vitendo vya mauaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino kwani watu wenye Ualbino wanahaki ya kuishi kama watu wengine mesema haya makao makuu ya chama cha watu wenye Ualbino Taifa jijini Dar es Salaam walivyokutana na wana habari.



Habari picha na Ally Thabiti