Thursday, 23 May 2024

WAZIRI WA AFYA ABAINISHA MBINU ZA HEDHI SALAMA

 Ummi Mwalimu Waziri wa Afya amesema ili kuwepo na hedhi salama nchini tanzania ni vyema wadau na serikali kujenga miundombinu rafiki na wezeshi kwenye mashule kwaajili ya wasichana waliopo mashuleni pamoja na kwenye masoko na maofisini lengo wanawake wanapofikia kipindi cha hedhi waweze kujistili huku wakiendelea na shughuri zao za kila siku.

Ametoa wito kwa jamii kuacha mira na destuli potofu pindi mwanamke anapofika kipindi cha hedhi.

Habari na Ally Thabit 

WIZARA YA UVUVI YAGUSWA NA WATU WENYE ULEMAVU


 Mkurugenzi wa  Uvuvi Prof  Mohammed Shekh Kutoka Wizara ya Uvuvi na Mifugo amesema katika wavuvi wadogo ambao mkutano wa kimataifa utafanyika tarehe 5/6/2024 jijini dar es  salaam ni muhimu sana kwani utasaidia wavuvi hawa kupata fursa mbalimbali ,Swala la kuwashirikisha na kuwafikia watu wenye ulemavu kwenye sekta ya uvuvi ni muhimu na lina tija kubwa hivyo wizara ya uvuvi na mifugo wamelibeba na watalifanyia kazi amesema haya jijini dar es salaam  nilipofanya nae mahojiano.

Habari picha na Ally Thabit 

WAZIRI WA UVUVI KUWATAFUTIA WAVUVI WADOGO MASOKO YA KIMATAIFA


 Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega amesema tarehe 5 /6/2024 kutakuwa na mkutano mkubwa wa kimataifa utakao fanyika Dar es salaam  lengo la mkutano huu kutatuwa changamoto walizonazo wavuvi wadogo na kujifunza mbinu za kisasa za kuvua pamoja na matumizi ya teknolojia .

Kwa tanzania wavuvi wadogo asilimia 95% na wameweza kujiajili na kuajili wengine zaidi ya ajira laki mbili therathini na sita elfu na fedha wanazochangia kwa mwaka tilioni 3.4 na kwa fedha za kigeni bilioni tano na tisa, Waziri wa uvuvi na  mifugo Abdallah Ulega  amemshukuru na kumpongeza rais Dr Samia  kwa kukuza na kuimarisha dipromasia ya uchumi ndio maana tanzania ikapewa nafasi ya kuandaa mkutano wa wavuvi wadogo kwa bara  la Afrika.

Mkutano huu utachochea wavuvi wadogo wa tanzania kupata masoko ya kuuza bidhaa zao kimataifa,pia itachochea kuwepo na mabadiriko ya sera na mihongozo kwa wavuvi wadogo watanzania na Afrika kwa ujumla  .pia tanzania itapata fursa ya kuwashawishi watu kuja kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi. Amesema haya wakati wa kuzungumza na wanahabari jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Wednesday, 22 May 2024

HER INITIATIVE YAWAKOMBOA WANAWAKE KIUCHUMI


Daniel Robert Head and Communication Officer amesema wameweza kuwakomboa na kuwakwamua wasichana kiuchumi kupitia Digital Platform mfano Panda Chart, Ongea App mpaka sasa Wanawake, Wasichana na Mabinti wapatao 5270 kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Lindi na Pwani wametafutia masoko lakini pia wameweza kuwatengenezea Platform pindi wanapotafuta kazi ikitokea wanatakiwa kutoa rushwa ya ngono watoe taarifa, amsema haya kwenye wiki ya bunifu iliyoandaliwa na COSTECH jiji Dar es Salaam ukumbiwa JNICC.

Habari Picha na Ally Thabiti.  

TAI YAWAKOMBOA WASICHANA


HAIKA MBOYA Human Resource and Administration amesema fanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa elimu ya afya ya uzazi wanawake na wasichana lengo waweze kukabiliana na chanamoto mbalimbali katika makuzi yao na wajuwe namna ya kuweza kujitunza kipindi cha mabadiliko ya kimwili inavyofika kila mwezi.

Ameitaka jamii kukaa karibu na mabinti zao wanapofikia kipindi cha ukuwaji wa kimwili wanamradi wa OKY pia elimu hii ya afya ya uzazi wanatoa mashuleni na mikoa waliyifikia Dar es Salaam pamoja na Arusha kwenye jamii ya wafugaji wa kimasai Haika Mboya amesema pia wamewafikia watu wenye ulemavu wa aina zote amesema haya jiji Dar es Salaam kwenye ukumbi wa JNICC katika wiki ya ubunifu iliyoandaliwa na COSTECH.

Habari Picha na Ally Thabiti 

BARAZA LA ULINZI NA USALAMA LA AFRIKA KUKUTANA TANZANIA MAY 25


Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na kati January Makamba amesema tarehe 25/05/2024 chombo cha baraza la ulinzi na usalama kwa Afrika lenye wanachama nchi kumi na tano 15 watakutana nchini Tanzania jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC lengo la kukutana kwa baraza hili ni kujadiri migogoro iliyopo kwenye nchi za Afrika.

Na nafasi za wanawake katika uwongozi na namna ya kujikwamua kiuchumi na kufanya maazimisho ya baraza hili la ulinzi na usalama la Afrika ambako lilianzishwa tarehe 25/05/2004 kwasasa limetimiza mika 20 katika mkutano wa baraza hili la ulinzi na usalama Rais Dr Samia Suluhu Hassan atakuwa mwenyekiti wa mkutano huu hii yote inatokana na Tanzania kuwa kitovu cha amani Afrika na Duniani kote.

Pia Tanzania imekuwa ni nchi ya kuongonza harakati za kupigania uhuru kwa nchi za Afrika na kuwa suluhishi wa migogoro kwenye bara la Afrika tangu enzi za Hayati Rias Nyerere, Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete na Rais Magufuri na sasa Rais Dkt Samia.

Waziri wa Mambo nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kati amesema mkutano wa baraza la ulinzi na usalama wa Afrika utauzuliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa amesema haya kwenye ofisi ya wizara ya mambo ya nje zilizopo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

Habari Picha na Ally Thabiti

Tuesday, 21 May 2024

UN WOMEN BUNIFU ZAO ZATATUWA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE


 Michael Jerry Pogramme Analyst-Women's Economic Empowerment amesema bunifu wanazozifanya zinatatuwa kwa kiasi kikubwa changamoto wanazokutana nazo wajasilia Mali wanawake na wasichana. lengo kubwa ni kuwainuwa kiuchumi wajasiliamali wanawake na wasichana  ambako UN WOMEN imewafikia wanawake Mia moja 100 tanzania bara na Zanzibar kwa kuwapa mafunzo namna ya kutumia teknolojia ya mitandao ili waweze kujinasua katika umasikini .

Michael Jerry amesema kundi la watu wenye ulemavu kupitia bunifu zao awajaliacha nyuma kwani UN WOMEN  wamebuni njia ya sauti kwaajili ya kuwafikia watu wasiiona amesema haya kwenye wiki ya bunifu yalioandaliwa na COSTECH jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

WABUNIFU WAUNGA MKONO NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 

Winifrida Anyambi Robert Engineer  kutoka TIRDO amesema wamefanya bunifu ya matumizi ya nishati safi mbalimbali katika kuunga mkono juhudi na jitihada za rais Dr Samia kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia wameweza kubuni mkaa safi wa kupikia ambao hauaribu mazingira na auna madhara ya kiafya kwa watumiaji .
Pia wamebuni majiko ambayo yanaubora katika matumizi ya kupikia .

Winifrida Anyambi amesema katika mradi wao wameweza kuwafikia wanawake na wanaume ,vijana na wasichana katika shughuri zao za ujasilia Mali kwenye mikoa ya Geita,Pwani,Mwanza,Morogoro na Dar es salaam  amesema haya kwenye wiki ya bunifu ilioandaliwa na COSTECH jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

WATU WENYE ULEMAVU HAWAJAACHWA KWENYE BUNIFU


 Katibu Mkuu  Prof Carolyne  Nembo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia amesema katika maswala ya bunifu watu wenye ulemavu  wa aina zote wamejuishwa na kushirikishwa kikamilifu katika maswala ya bunifu ambako wizara ya Elimu inatoa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu mashuleni kuanzia Elimu ya hawali,msingi,secondary na vyuo vikuu na vya kati.Mfano kwawasio Ona wanapewa mashine za kuandikia maandishi ya nukta nundu ,kompyuta na kwa watu wenye uono hafifu na wenye uharibino wameandaliwa vitabu vyenye maandishi makubwa.

Pia serikali imeandaa wali wakufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum haya yote yanafanywa lengo watu wenye ulemavu waweze kushiriki kikamilifu kwenye bunifu na  wajue kutumia teknolojia za kisasa. Amesema haya kwenye week ya bunifu ilioandaliwa na COSTECH.

Habari na Ally Thabit 

Monday, 20 May 2024

MKURUGENZI WA NIMR AWATOA OFU WATANZANIA


 Prof Saidi Abudi Mkurugenzi  Mkuu wa NIMR amesema watajitahidi tafiti zao ziweze kutatuwa matatizo yanayowasibu watanzania,pia watajitahidi kuja na chanjo za kuzuia maambukizi ya magonjwa ya binadamu.

Habari picha na Ally Thabit 

WAZIRI WA AFYA ATOA MAAGIZO MAZITO

 Waziri wa Afya Ummi Mwalimu ameitaka taasisi  ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR wafanye tafiti zenye kutatuwa changamoto kwa muda mfupi, pia tafiti wanazozifanya zije na chanjo za kuzuia magonjwa hili serikali isitumie pesa nyingi kwaajili ya kutibu,amehaidi kutoa ushirikiano na kutoa pesa nyingi kwa tafiti za NIMR  .

Ambako kwa sasa kwenye bajeti ya serikali imetenga bilioni 3.5 fedha hizi ili zitumike kwenye tafiti za NIMR. 

Habari na Ally Thabit 

EQUITY BANK KUYAFIKIA MAKUNDI YOTE


 Mkurugenzi  Mkuu wa Equity  Bank Isabera Maganga ameaidi kuwa dirisha la mikopo lililozinduliwa leo kwaajili ya kutoa huduma za kifedha kwenye Equity bank litawahudumia wanawake wote wa vijijini,mijini,wajasiliamali wadogo,wakati na wakubwa pia fundi la wenye ulemavu wanawake watapata huduma za mikopo kikubwa wawe na sifa za kukopesheka.

Isabera Maganga ametoa wito kwa watu wote waitumie bank ya Equity kwani ni salama na inatoa mikopo ambayo aina masharti magumu na riba yake ni kiwango cha chini, ametoa rai kwa wanawake kutumia dirisha la Equity  bank lililozinduliwa leo kwani litawasaidia katika kujikwamuwa kiuchumi.

Habari picha na Ally Thabit 

GSI YAIPONGEZA EQUITY BANK

 Mkurugenzi wa GSI Fatma Kange amesema uzinduzi wa  dilisha maalum kwaajili ya kuwahudumia wanawake kwenye bank ya Equity litafunguwa fursa mbalimbali kwa wanawake .dilisha hili litafanya wanawake kutengeneza bidhaa bora.

Habari na Ally Thabit 

EQUITY BANK YAWAFIKIA WANAWAKE

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi maalum Dr Dorothy Ngwajima  ameipongeza Equity bank kwa kuzinduwa dirisha maalum kwakuwahudumia wanawake ambako itasaidia wanawake kupata mikopo ya masharti nafuu amewataka wanawake kuitumia bank ya Equity ili wajikwamuwe kiuchumi.


Habari picha na Ally Thabit 

Saturday, 18 May 2024

KATIBU MKUU WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA AIMIZA WATANZANIA KUFANYA MAZOEZI


 Philip Bai Katibu Mkuu Kamati ya Olimpiki  tanzania amewataka watanzania kushiriki kwenye mbio mbalimbali kwani zina umuhimu katika miili yao, amewataka waandaaji wa mbio za riadha kuwashirikisha watu wenye ulemavu.

Habari  picha na Ally Thabit  

MKUU WA SHULE YA SENT JOSEPH AIMIZA MAADIRI KWA WANAFUNZI

 Sister Tiodora amewapongeza Wanafunzi waliomaliza  Kidato cha sita Shule ya Sekondary Sent Joseph amewataka kuendeleza nidhamu na elimu walioipata wakaitumie vizuri katika jamii. Pia amewataka wazazi na walezi wawapeleke shule watoto wa kike kwani wote wana haki sawa.

Sister Tiodora ametoa wito kwa jamii kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu na badala yake wawapeleke shule na kuwapa fursa mbalimbali.

Habari na Ally Thabit 

MBIO ZA MSOGA HALF MARATHON KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO


 Mratibu wa Mbio za Msoga Nelson Mrashana amesema mbio hizi zitafanyika tarehe 29/6/2024 wilaya ya Charinze eneo la Msoga  ,Lengo la mbio hizi kukusanya kiasi cha milioni Mia moja  ambako fedha hizi zitapelekwa kwenye hospital Msoga ili kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifunguwa hususani watoto ambao wanazaliwa kabla ya wakati (Njiti).

Pesa hizi zitasaidia kununua vifaa tiba mfano kangaroo . Nelson Mrashan amewataka watu binausi,taasisi,mashirika kushiriki kwenye mbio hizi ambako gharama za fomu elfu 35000 ambako fedha hizi unalipa kupitia lipa namba ya tigo 15840234 .

Habari picha na Ally Thabit 

Thursday, 16 May 2024

MATAPELI WA MTANDAONI WATIWA MBALONI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam  Jumanne Mulilo amesema wamewakamata watu 27 jijini dar es salaam ambao wamekuwa wakifanya utapeli kwa kutumia raini za simu za mkononi  ,matapeli hawa walikuwa wanatuma jumbe kwenye simu tofautitofauti ili watumiwe pesa .

Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa kutoa taarifa ambazo zimepelekea kukamatwa kwa matapeli hawa ,kamanda Mulilo amesema mpaka sasa jumla ya matapeli wanaotumia simu za mkononi kwaajili ya kutapeli watu wameshakamatwa 85 amesema haaya wakati akizungumza na wanahabari makao makuu ya Jeshi la Polisi kanda maalum jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

Wednesday, 15 May 2024

DR LUCAS MAGANGA MTAFITI NIMR MBEYA AELEZA CHANJO KUMI 10 ZA UKIMWI


 Taasisi ya NIMR  Mkoa wa Mbeya inafanya tafiti kwenye magonjwa mbalimbali mfano marelia,ukimwi ,  Kifua kikuu ,kansa na magonjwa mengineyo Dr  Lucas Maganga mtafiti taasisi ya utafiti NIMR  Mbeya ameitaka jamii kuwa na uvumilivu kwa watu wanaofanya tafiti kwani tafiti autoi majibu ya hapo kwa hapo.

Ameitaka jamii watafiti wanapoenda kufanya tafiti zao wawape ushilikiano wa kutosha kwani utafiti unaitaji ushiliki mkubwa wa jamii , taasisi ya NIMR  Mbeya inafanya kazi ya utafiti kanda ya kusini pamoja na mkoa wa mbeya kwa ujumla ambako mwaka1990 taasisi hii ilikuwa na mashilikiano na wabia kutoka ujerumani na marekani lakini ilipofika mwaka 2008 taasisi  hii ya utafiti Mbeya ilichukuwa na taasisi ya utafiti NIMR  ambako kwa sasa inatambulika taasisi ya utafiti  NIMR  Mbeya.

Dr Lucas Maganga amesema taasisi ya NIMR  Mbeya imefanya tafiti za chanjo 10 za UKIMWI  lengo kupata tiba na namna ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI  kupitia chanjo hizi walizofanyia tafiti taasisi ya NIMR  Mbeya inajumla ya wataalam 170

Kupitia Tafiti zao Wana Mipango na Mikakati ya kufikia makundi yote kwa sasa watu wenye uziwi wana mtaalam mmoja ambaye anatumia Lugha ya Alama, taasisi hii inasaidia serikali katika kufanya mabadiliko  ya kisera kwenye sekta ya afya.

Habari picha na Ally Thabit 

KAMATI YA BUNGE INAYOSIMAMIA MASWALA YA UKIMWI,AFYA NA MAZINGIRA YATEMBELEA TAASISI YA UTAFITI IFAKARA INSTITUTE


 Mbunge wa Jimbo la Ndanda na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Ukimwi,Afya na Mazingira Devidi Mwambe akimwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hii kama amavyoonekana pichani akipata maelezo kutoka kwa mtafiti wa taasisi ya IFAKARA INSTITUTE  Kama wanavyoonekana pichani wakiwa kwenye banda. Ambako mtafiti huyu akimwelezea namna taasisi ya IFAKARA ilivyogundua inside ya kukabiliana na mbu lengo ni kutokomeza marelia nchini.

Habari picha na Ally Thabit .


TAASISI YA IFAKARA YAIMIZA USHIRIKIANO KWA WANANCHI


 Alex Limwagu Mtafiti wa Taasisi ya Ifakara amesema kongamano  la kisayansi  la 32  litasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mabadiliko ya kiutafiti nchini tanzania kwani watafiti wengi kutoka nchi mbalimbali wataeleza mbinu na njia wanazozitumia katika kufanya tafiti zao pamoja na teknolojia za kisasa za kufanyia tafiti.

 Ameipongeza na kuishukuru NIMR  kwa kuweka kongamano ili kwani litajenga mausiano mazuri na watafiti hapa nchini na nje ya nchi na kukuza ushirikiano wa kitafiti.

Ametoa wito kwa jamii kutoa ushilikiano pindi watafiti wanaitaji taarifa kwaajili ya utafiti pamoja na maeneo ya kufanyia tafiti mfano bila utafiti wa kuuwa mbu kwa kutumia dawa using fanyika mpaka Leo mazalia ya mbu yangekuwa  mengi na kusingekuwa na tafiti ya kutibu marelia watu wengi wangekufa kwaajili ya marelia. 

Amesema haya kwenye kongamano la 32 la watafiti wa sayansi lililoandaliwa na NIMR  kwenye ukumbi wa mwalimu nyerere  jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

KAMATI YA UKIMWI AFYA MAZINGIRA YA BUNGE YAPONGEZA TAFITI ZA NIMR


 Mbunge wa Mkoa wa Lindi Devidi Mwambe ambae amemwakilisha Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ukimwi na afya mazingira amesema tafiti zinazofanywa na NIMR  zinafaida kubwa Sana ,kwani tafiti hizi zinatatuwa changamoto katika jamii na zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha na kuandaa sera kwenye sekta ya afya.

Mbunge Mwambe ameipongeza NIMR  kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufanya tafiti zenye tija na mafanikio makubwa ikiwemo namna ya kukabiliana na HIV na magonjwa mengine . Swala la tafiti kuwekwa kwenye maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasioona ni muhimu pia matumizi ya Lugha za alama kwa wenye uziwi ni vyema yazingatiwe.

Amesema haya kwenye kongamano la 32 la utafiti wa  kisayansi  uliofanyika ukumbi wa mwalimu nyerere  jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

TCRA YAKUTANA NA WADAU WA HABARI

 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tcra Mwandisi Kisaka amesema lengo la kukutana na wadau wa habari ni kuweza kujadili changamoto wanazokutana nazo ili serikali iweze kufanyia kazi.

Habari na Ally 

Tuesday, 14 May 2024

NAIBU WAZIRI MKUU AIPONGEZA NATIONAL INSTITUTE FOR MEDICAL RESEACH (NIMR)


 Dr Doto Mashaka Biteko amesema tafiti zinazofanywa na  National Institute  for Medical Reseach (NIMR) zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta mbalimbali nchini tanzania Pia tafiti hizi zinawezesha serikali kufanya maamuzi sahihi kupitia tafiti zao na kupelekea kupatikana maendeleo kwa haraka na kwa kasi nchini tanzania .

Naibu Waziri Mkuu Dr Doto Mashaka Biteko amesema serikali itaendelea kutoa fedha nyingi kwenye National  Institute for  Medical Reseach (NIMR) wafanye tafiti zao za sayansi  kwa kisasa kupitia teknolojia mpya kwani tafiti zao zimeboresha huduma za kiafya nchini na kupelekea kuwepo na madiliko ya sera za afya.

Pia serikali itaendelea kuboresha miundombinu kwenye mahabarata wanazofanyia tafiti na kuongeza wafanyakazi kwenye taasisi  pamoja na kuboresha maslai yao.amesema haya kwenye kongamano la 32 lililojuisha watafiti wa kisayansi  kutoka mataifa mbalimbali duniani ambako linafanyika jijini dar es salaam  ukumbi wa mwalimu nyerere. 

Habari picha na Ally 


MKURUGENZI WA NIMR AHAIDI MAZITO KWENYE KONGAMANO LA 32 LA TAFITI ZA KISAYANSI


 Prof Saidi Abudi Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Tafiti Tanzania NIMR  amesema kongamano ili la 32 lililowakutanisha watafiti wa kisayansi kutoka nchi mbalimbali duuniani litasaidia kutatua changamoto mbalimbali za tafiti pamoja na kuwawezesha watumishi wa NIMR  wanaofanya tafiti kupata mbinu mpya za tafiti na kujifunza teknolojia za kisasa za kufanyia tafiti .

Kongamano ili litasaidia kufanya maboresho ya sera za utafiti tanzania, Prof Saidi Abudi amemshukuru na kumpongeza rais Dr Samia  kwa kutoa fedha nyingi kwenye taasisi ya NIMR  ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya uwekezaji kwenye vituo 7 vya utafiti ikiwemo  Mbeya,Mwanza,Amani,Dar es salaam  upande wa muhimbili na mabibo,Morogoro na Pwani uko kote tafiti zinafanyika kwenye marelia,Tibii na magonjwa mengineyo.

Amesema haya kwenye kongamano la32 la kisayansi jijini dar es salaam ukumbi wa mwalimu nyerere 

Habari picha na Ally Thabit .

DR KAPOLOGWE ABAINISHA UMUHIMU WA UTAFITI


 Dr Kapologwe Kutoka NIMR amesema Tafiti zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto zilizopo kwenye Jamii mfano sekta ya Elimu ,kilimo na sekta zinginezo Kupitia taasisi ya NIMR  sekta ya afya imeweza kukuwa kwa kiasi kikubwa mpaka kupelekea kuwepo na huduma bora za afya haya yote yamefanywa na taasisi ya NIMR. 

Dr Kapologwe amesema tafiti zinazofanywa na NIMR  ni jumuishi kwa makurdi yote amesema haya kwenye kongamano la 32 la tafiti za kisayansi jijini Dsm  ukumbi wa mwalimu nyerere.

Habari picha na Ally Thabit 

DR ERIZABETI SHAYO AELEZEA TUZO ALIOIPATA

 

Mtafiti kutoka Taasisi ya NIMR Tanzania amesema Tuzo alioipata leo nikwaajili ya tafiti anazozifanya zilivyoweza kusaidia mabadiliko kwenye sekta ya Afya ambako imepelekea mpaka kuwepo na mabadiliko makubwa ya kisera ambako apoawali kwenyesekta ya afya kuna sera zilikuwa zinakwamisha upatikanaji wa huduma bora za afya tanzania.

Pia ameandika Majarida ambayo yalizungumzia matatizo yaliopo kwenye sekta ya afya na kutoa mapendekezo na mabolesho ya sekta afya ,ambako serikali kupitia taasisi ya NIMR imefanyia kazi na kuleta mabadiliko kwenye sekta ya afya .

Dr Erizabeti Shayo ameweza kuwatia moyo wasichana na wanawake kushiliki kwenye maswala ya tafiti na kupenda masomo ya sayansi .ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwasomesha watoto wa kike kwani wanauwezo mkubwa wa kufanya  kama rais Dr Samia. Amewataka kutenga muda wakuwa na familia pamoja na malezi pia washiliki katika shughuri mbalimbali  za kiuchumi.

Swala la tafiti kuwafikia watu wenye makundi maalum ni muhimu na lina tija amesema haya kwenye kongamano la 32 la kisayansi lililoandaliwa na taasisi ya utafiti tanzania NIMR jijini dar es salaam  ukumbi wa mwalimu nyerere.

Habari picha na Ally Thabit 

Monday, 13 May 2024

ESTA MAMBALI ABAINISHA MIKAKATI YA WIZARA YA AFYA


Esta Mambali wa Wizara ya Afya amesema katika kukabiliana na maswala ya afya na mazingira wizara ya afya inatekeleza kwa vitendo jitihada na juhudi za rais Dr Samia  kwa kufanya miradi mbalimbali ya kuondoa ualibifu wa mazingira kwa kuimiza wananchi matumizi ya nishati safi ya kupikia ambako wizara ya afya imeandaa machapisho mbalimbali pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi na watumishi wa wizara ya afya  namna ya kuzingatia utunzaji wa mazingira ambko itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na mabadiliko ya nchi.

Mfano wanawaimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na waachane na matumizi ya kuni na mkaa amesema haya kwenye semina  iliowakutaanisha mabibiafya na mabwanaafya ukumbi wa mwalimu nyerere  jijini dar es salaam  .

Huku Esta Mambali akisisitiza kuwa elimu wanazozitoa wanafikia makurdi yote wakiwemo watu waishiopembezoni na makurdi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu wa aina zote.

Habari picha na Ally 

CUF KUSIMAMISHA WAGOMBEA WANAWAKE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof Hibrahim Haruna Lipumba amesema uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unafanyika mwaka huu 2024 chama cha cuf kitasimamisha kwa wingi wanawake ili wagombee nafasi  za wenyekiti na ujumbe Tanzania nzima kwani wanawake wanauwezo mkubwa wa kuongoza pia amesema watawaunga mkono na kuondoa vikwazo vilivyokuwavinafanya wanawake washing we kugombea  huku akiwataka wanawake wajitokeze kwa wingi katika kuchagua na kuchaguliwa kwenye uchaguzi huu.

Mwenyekiti Lipumba amesema elimu wanayoitoa TGNP ya watu kuachana na mira na desturi potofu dhidi ya wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ni mzuri na ni vema vyama vote vya siasa kuunga mkono juhudi na jitihada hizi zinazofanywa na TGNP kwa kuondoa vikwazo kandamizi na mira desturi potofu zinazokuwa kikwazo kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi.

Ametoa wito kwa wanaume nchini kuwachana na mifumo dume badala ÿke wawape ruksa wanawake kugombea nafasi za uongozi amesema haya kwenye kongamano la miaka 60 ya muungano lililoandaliwa na shirika la utangazaji TBC maktaba ya taifa chuo kikuu mlimani nilipofanya nae maojiano.

Habari picha na Ally Thabit 

TCCIA WAIPONGEZA TANTRADE


 Mkurugenzi  wa Tccia Oska Kisanga amesema tantrade imewasaidia kwa kiasi kikubwa kupeleka biashara zao nchini Korea Kusini  baada ya kuingia makubaliano na nchi hiya ambako mwanzoni ilikuwa vigumu watanzania kupeleka biashara zao nchini Korea Kusini.

Habari picha na Ally Thabit 

TANTRADE YATEKELEZA KWA VITENDO DHAMIRA YA DR SAMIA


 Mkurugenzi wa Tantrade Latifa M Khamis amesema  wameingia makubaliano na nchi ya Korea Kusini lengo wafanyabiashara watanzania waweze kupeleka biashara zao kwa uhuru ambako itasaidia kwa kiasi kikubwa  kukua kwa biashara za watanzania .

Makubaliano haya yamefungua milango ya Wakorea Kusini kuja kuwekeza Tanzania. Bi Latifa M Khamis amesema tantrade inatekeleza haya kwa vitendo kwaajili ya kumuunga mkono rais Dr Samia falsafa ya kukuza diplomatic ya uchumi ambako kwenye maonyesho ya sabasaba ya mwaka huu kutakuwa na siku ya bidhaa za Korea amesema jijini dar es salaam  alipokutana na  wakorea.

Habari picha na 

RAIS DR SAMIA KUONGOZA MKUTANO NCHINI UFARANSA


 Waziri wa Mambo Ya Nje na Ushilikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema rais Dr Samia anaenda nchini  Ufaransa kwaajili ya kuongoza mkutano wa kujadili matumizi ya nishati safi ya kupikia ambako rais Dr Samia yeye ndio Mwenyekiti Mwenza wa maswala ya nishati safi ya kupikia .

Mkutano huu utaudhuliwa na mataifa mbalimbali kutoka duniani kote lengo kuu la mkutano ni kujadili sera,sheria,kanuni na taratibu zinazokwaimisha na kuludisha nyuma mipango ya nishati safi ya kupikia kwa nchi za Afrika ,pili kubolesha na kulekebisha sera,sheria,kanuni na taratibu zilizopo sasa na tatu kuzitaka nchi zilizoendelea na makampuni makubwa kutoa fedha na ahadi mbalimbali ambazo zitasaidia katika kuarakisha matumizi ya nishatisafi ya kupikia.

Waziri January Makamba amesema Tanzania imepata nafasi kubwa ya kushiriki mkutano huukwa sababu rais Dr Samia amekuwa kinara na ameweka mikakati mizuri na mikubwa katika kupigania matumizi ya nishati safi ya kupikia  Mkutano huu utafanyika tarehe 14 /5/2024 amesema haya jijini dar es salaam kwenye office ya mambo ya nnje.

Habari picha na Ally Thabit 


Thursday, 9 May 2024

MKURUGENZI WA MILKI BUNIFU ABAINISHA MIKAKATI YA KUWAFIKIA WATU WENYE


 Loy Mhando Mkurugenzi wa Milki bunifu  Brela amesema kupitia mkataba wa marakeshi inayozungumzia maswala ya kujumuisha watu wenye ulemavu namna ya kupata taarifa kwaupande wao brela kupitia milki bunifu  kwenye shughuri mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu na wataweza kuwafikia watu wenye ulemavu wa aina zote .

Kwa wenye uziwi watatumia wataalamu wa rugha za alama ili na wao waweze kupata taarifa na kufaidika na milki bunifu,kwa wasioona brela inamikakati yakuweza kuweka maandishi ya nukta nundu ili na wao waweze kupata taarifa mbalimbali na kushiliki kikamilifu kwenye milki bunifu kwa ngazi zote.

Amesema haya jijini dar es salaam  kwenye maazimisho ya siku  milki bunifu ambako kila mwaka ufanyika tarehe 26/4 Duncan kote.

Habari picha na Ally Thabit 

RAIS DR SAMIA APIGA MALUFUKU MATUMIZI YA MKAA

 Rais Dr Samia amezitaka taasisi zote za kiserikali ifikapo mwezi wa nane 8/2024  taasisi ziachane na matumizi ya mkaa na kuni wakati wa kupika kwani matumizi haya ya mkaa canaletto athali kubwa ya kiafya na mazingira kwa ukataji wa miti.

Pia serikali iko kwenye mango wa kushusha bei ya gesi za kupikia ili kila mtanzania aweze kutumia nishati safi katika kupika chakula. Nae kwa upande wake Spika wa bunge la tanzania dokta Tulia Akison amesema nishati safi ya kupikia inasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kukuza wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

piainawaepusha wanawake na vijana kuepukana na vitendo vya ukatili wakati wanapoenda kukata kuni mfano kubakwa na vitendo vya uzalilishaji.

Kwa upande wake waziri mkuu amewataka wakuu wa wilaya,wakurugenzi, wakuu wa mikoa na watendaji wote kusimamia na kuwaimiza wananchi wote wazingatie matumizi ya nishati safi ya kupikia .

Nae waziri wa nishati Dr Doto Biteku ameahidi kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, pia ataenda kuwasimamia watendaji wote kutotumia kuni na mkaa kwenye taasisi zao na wakuu wa wilaya ,wakuu wa mikoa attendance kuwasimamia .

Waziri wa nishati amesema ifikapo mwaka 2034 watanzania zaidi ya asilimia 80%waweze kutumia nishati safi ya kupikia haya ndio malengo ya serikali waliojiwekea.

Habari picha na Ally Thabit 


BRELA YAWAESHIMISHA WABUNIFU

 

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Brela Godfrey Nyaiza amesema brela wanafanya kazi kubwa ya kutangaza na kutafuta masoko kazi za wabunifu lengo wabunifu waweze kujikwamuwa kiuchumi na waweze kujiajili na waweze kujiajili wenyewe, ndio maana kwenye maazimisho ya wiki milki bunifu brela impinging makubaliano na chuo kikuu Mzumbe,chuo kikuu TIA, Kosota,chuo kikuu Mlimani na taasisi ya viwatilifu lengo wabunifu wafikiwe kwa uraisi na  wapewembinu mbalimbali za kazi zao.
Amesema haya jijini Dar es salaam  kwenyeaazimisho ya wiki ya milki bunifu ambako kila mwaka uazimishwa kila ifikapo tarehe26 mwezi wa 4 .

Habari picha na Ally Thabit 

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA MABANDA YA WAWUNIFU


 Naibu waziri wa wizara ya michezo ,Sanaa na utamaduni Amisi Mwijuma amewapongeza na kuwatia moyo wabunifu nchini Tanzania na kuwaaidi kuwa kupitia brela kazi zao za ubunifu zitakuwa na mafanikio na kuwanyanyua kiuchumi.

Amesema haya baada ya kuwatembelea moja ya wabunifu jijini Dsm alipokabiziwa kazi anazozifanya mbunifu huyu.

Habari picha cha Ally thabiti

WANAWAKE WAJANE WAPONGEZA UCHECHEMUZI WA TGNP

 

Katibu wa Wajane  Kata ya Kibonde Maji Adija Abdallah amewapongeza TGNP kwa kazi wanayoifanya ya uchechemuzi  kwa kuamasisha watu kuachana na mila na desturi potofu zidi ya wanawake wanapoitaji kugombea nafasi za uongozi.

Ivyo amewataka wanawake nchini Tanzania kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi za serikali ya mitaa takao fanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu takao fanyika mwakani kwenye udiwani,ubunge na uris.

 ametoa wito kwa wanawake wajane kuunga mkono  juhudi na  jitiada zinazofanywa na tgnp za kuwataka wanawake kushiliki kwenye chaguzi na amewataka wamaume kuondoa mawazo Uganda za kutoa nafasi kwa wanawake kugombea amesema haya jijini Dsm viwanja vya sabasaba kwenye wiki ya wanawake wajane nilipofanya nae maojiano.

Habari na Ally Thabit 

BRELA YAAZIMISHA WIKI YA UBUNIFU

Katika Maazimisho ya Wiki Bunifu Brela imefunguwa fursa kwa taasisi mbalimbali lengo kukuza bunifu na kuzilinda  kama inavyoonekana kwenye picha  taasisi zikitiliana saini kwenye hati ya makubaliano kwaajili ya kushilikiana  kwenye nyanja mbalimbali 

 Habari picha na Ally  Thabiti.

TIA YAIPONGEZA BRELA


 Mkuu wa Chuo cha TIA Prof Paranju amesema hati ya makubaliano waliosaini na Brela itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza bunifu,kupatikana kwa masoko ya kitaifa na kimataifa na Brela inasajili wajasilia Mali wa chuo cha TIA kwa Mwanza,Mbeya,dar es salaam, zanzibar na kwenye matawi ya TIA .

Prof Paranju amesema wafanyakazi wa tia pamoja na wanafunzi 28153 watanufaika na makuvaliano haya jijinini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

LIBERTY SPARKS WAITAKA SERIKALI KUBOLESHA SERA YA BIASHARA


 Mkurugenzi Mkuu wa Liberty Sparks Evance amesema ni vyema serikali kuweza kufanya mabadiliko ya sera na sheria  kwani itasaidia kukuza biashara.

Habari na Ally Thabit 

KANISA LA TAG LAJA NA MUAROBAINI WA MMOMONYOKO WA MAADILI


 Mchungaji Drt. Barbaras  Weston Mtokambali Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God. Amesema kanisa la Tag katika kukabiliana na maswala ya mmomonyoko wa maadili nchini Tanzania  wamewekeza vijana kwa kiwango kikubwa kwa kuwapa elimu mbalimbali za kumjuwa mungo na makatazo mbalimbali ambako kuànzia shule za awali,msingi,secondary na vyuo vyikuu kanisa la Tag linatoa mafunzo kwa wanafunzi wote wa shule za seeikali na binausi.

Ambako kanisa la Tag three 14/7/2024 kwenye uwanja wa uhuru jijini dsm wataazimisha miaka 85 tanguy kuanzishwa kanisa la Tag, pia kutakuwa na makongamano mbalimbali yatakayojumuisha vijana ,viongozi wa dini na viongozi kutifa mbalimbali na viongozi wa serikali.
Habari picha na Ally Thabit 

HAKI ELIMU YATOA MAPENDEKEZO YA BAJETI


 Makumba Mwenezi Meneja Idara ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera haki Elimu amesema kwenye makadlio ya bajeti Elimu iliowasilishwa bungeni na Waziri wa elimu Prof Adofu Mkenda kiasi cha tilioni 1.9 bad akijafikia viwango vya kimataifa kwa kila nchi iwezekufikia asilimia20% lakini kwa Tanzania makadilio ya bajeti iliowasilishwa bungeni aijafikiwa haha kidogo.

Swala la mikopo ya elimu ya juu si rafiki kwa vyuo vya Ufundi na vyuo vya kati  kwani wanafunzi wa vyuo hivi awana sifa za kukopesheka na hata wanafunzi wa vyuo vya juu wasio somea masomo ya sayansi nao awana sifa za  kukopesheka.

Taasisi ya haki Elimu inaitaka serikali kuweka mifumo ya mikopo ya elimu rafiki kwa wanafunzi wote ,pia waondoe vikwazo na masharti magumu ya mikopo kwa wanafunzi wote.

Swala la mafunzo ya Amali ni vema serikali mafunzo haya yangeanza kuanzia kidato cha kwanza hadi 4 kwa shule zote za secondary za serikali na binausi, pia walimu wa mafunzo haya wawe na ujuzi wa kutosha

Elimu jumuishi bajeti yake sio rafiki.

Habari picha na Ally Thabit 

Tuesday, 7 May 2024

COOK FUND YAONGEZA UWELEWA WA MATUMIZI YA NISHATI SAFI


 Dr Peter amesema biashara ya hewa ukaa ni muhimu Sana kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambako watu wataachana kupika kupitia kuni na mkaa kwa kiwango kikubwa.

Watanzania walio wengi wanapika kwa kutumia kuni na mkaa ndio maana taasisi  ya Cookfund wamesajili miradi ipatayo42 ya hewa ukaa na wamewezesha wataalamu 80 kwenye sekta 4 kwaajili ya kuwapa mafunzo ya matumizi ya hewa ukaa mpaka sasa washatoa semina6 za kuwajengea uwezo wataalam mbalimbali .

Lengo kubwa watu waingie kwenye biashara ya hewa ukaa ili kuzinusulu na kuziokoa ekta 48.14 milioni za misitu nchini Tanzania zisialibiwe kwa kukatwa.

Pia taasisi yao inatoa mafunzo kwa wakulima namna ya kutumia nishati safi ya kupikia ili wailing na kuitunza misitu yao na waingie kwenye biashara ya hews ukaa ambako itawasaidia kujiinua kiuchumi.

Habari picha na Ally Thabit 

WATANZANIA WAIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA YA HEWA UKAA


 Manual W Muro senior Finance Specialist  Cookfund Programme Meneger amesema biashara ya hewa ukaa inafaida kubwa ni vyema watanzania wajitokeze kwa wingi katika kuwekeza kwenye biashara hii ya hewa ukaa.

Kwani kwa Tanzania inafursa kubwa ya kufanya biashara hii kwakuwa kuna hekta za misitu zaidi ya milioni40  pia biashara hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuifadhi na kulinda misitu yet kwani wananchi wataacha matumizi ya kuni na mkaa katika kupika.  

Imanue W Muro amesema ni vyema serikali na sekta binausi waweke dira ya pamoja ili kufanikisha biashara ya hewa ukaa ,pia serikali ifanye mabolesho ya sera ,kanuni na sheria ya biashara ya hewa ukaa lengo kuwavutia watu wengi kuwekeza kwenye  biashara hii ya hewa ukaa.

Ambako sheria iliopo sasa ilianzishwa mwaka 2022  ,amesema haya jijini dar es salaam kwenye mkutano wa wadau wa hewa ya ukaa UNIDO,COOKFUND FOOD AND AGRICUITURE OF ORGANIZATION OF THE UNITED NATIONS NA UNCDF

 

Habari picha na  Ally thabit