Tuesday, 14 May 2024

MKURUGENZI WA NIMR AHAIDI MAZITO KWENYE KONGAMANO LA 32 LA TAFITI ZA KISAYANSI


 Prof Saidi Abudi Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Tafiti Tanzania NIMR  amesema kongamano ili la 32 lililowakutanisha watafiti wa kisayansi kutoka nchi mbalimbali duuniani litasaidia kutatua changamoto mbalimbali za tafiti pamoja na kuwawezesha watumishi wa NIMR  wanaofanya tafiti kupata mbinu mpya za tafiti na kujifunza teknolojia za kisasa za kufanyia tafiti .

Kongamano ili litasaidia kufanya maboresho ya sera za utafiti tanzania, Prof Saidi Abudi amemshukuru na kumpongeza rais Dr Samia  kwa kutoa fedha nyingi kwenye taasisi ya NIMR  ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya uwekezaji kwenye vituo 7 vya utafiti ikiwemo  Mbeya,Mwanza,Amani,Dar es salaam  upande wa muhimbili na mabibo,Morogoro na Pwani uko kote tafiti zinafanyika kwenye marelia,Tibii na magonjwa mengineyo.

Amesema haya kwenye kongamano la32 la kisayansi jijini dar es salaam ukumbi wa mwalimu nyerere 

Habari picha na Ally Thabit .

No comments:

Post a Comment