Thursday, 9 May 2024

RAIS DR SAMIA APIGA MALUFUKU MATUMIZI YA MKAA

 Rais Dr Samia amezitaka taasisi zote za kiserikali ifikapo mwezi wa nane 8/2024  taasisi ziachane na matumizi ya mkaa na kuni wakati wa kupika kwani matumizi haya ya mkaa canaletto athali kubwa ya kiafya na mazingira kwa ukataji wa miti.

Pia serikali iko kwenye mango wa kushusha bei ya gesi za kupikia ili kila mtanzania aweze kutumia nishati safi katika kupika chakula. Nae kwa upande wake Spika wa bunge la tanzania dokta Tulia Akison amesema nishati safi ya kupikia inasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kukuza wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

piainawaepusha wanawake na vijana kuepukana na vitendo vya ukatili wakati wanapoenda kukata kuni mfano kubakwa na vitendo vya uzalilishaji.

Kwa upande wake waziri mkuu amewataka wakuu wa wilaya,wakurugenzi, wakuu wa mikoa na watendaji wote kusimamia na kuwaimiza wananchi wote wazingatie matumizi ya nishati safi ya kupikia .

Nae waziri wa nishati Dr Doto Biteku ameahidi kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, pia ataenda kuwasimamia watendaji wote kutotumia kuni na mkaa kwenye taasisi zao na wakuu wa wilaya ,wakuu wa mikoa attendance kuwasimamia .

Waziri wa nishati amesema ifikapo mwaka 2034 watanzania zaidi ya asilimia 80%waweze kutumia nishati safi ya kupikia haya ndio malengo ya serikali waliojiwekea.

Habari picha na Ally Thabit 


No comments:

Post a Comment