Alex Limwagu Mtafiti wa Taasisi ya Ifakara amesema kongamano la kisayansi la 32 litasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mabadiliko ya kiutafiti nchini tanzania kwani watafiti wengi kutoka nchi mbalimbali wataeleza mbinu na njia wanazozitumia katika kufanya tafiti zao pamoja na teknolojia za kisasa za kufanyia tafiti.
Ameipongeza na kuishukuru NIMR kwa kuweka kongamano ili kwani litajenga mausiano mazuri na watafiti hapa nchini na nje ya nchi na kukuza ushirikiano wa kitafiti.
Ametoa wito kwa jamii kutoa ushilikiano pindi watafiti wanaitaji taarifa kwaajili ya utafiti pamoja na maeneo ya kufanyia tafiti mfano bila utafiti wa kuuwa mbu kwa kutumia dawa using fanyika mpaka Leo mazalia ya mbu yangekuwa mengi na kusingekuwa na tafiti ya kutibu marelia watu wengi wangekufa kwaajili ya marelia.
Amesema haya kwenye kongamano la 32 la watafiti wa sayansi lililoandaliwa na NIMR kwenye ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment