Mbunge wa Mkoa wa Lindi Devidi Mwambe ambae amemwakilisha Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ukimwi na afya mazingira amesema tafiti zinazofanywa na NIMR zinafaida kubwa Sana ,kwani tafiti hizi zinatatuwa changamoto katika jamii na zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha na kuandaa sera kwenye sekta ya afya.
Mbunge Mwambe ameipongeza NIMR kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufanya tafiti zenye tija na mafanikio makubwa ikiwemo namna ya kukabiliana na HIV na magonjwa mengine . Swala la tafiti kuwekwa kwenye maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasioona ni muhimu pia matumizi ya Lugha za alama kwa wenye uziwi ni vyema yazingatiwe.
Amesema haya kwenye kongamano la 32 la utafiti wa kisayansi uliofanyika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment