Monday, 13 May 2024

CUF KUSIMAMISHA WAGOMBEA WANAWAKE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof Hibrahim Haruna Lipumba amesema uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unafanyika mwaka huu 2024 chama cha cuf kitasimamisha kwa wingi wanawake ili wagombee nafasi  za wenyekiti na ujumbe Tanzania nzima kwani wanawake wanauwezo mkubwa wa kuongoza pia amesema watawaunga mkono na kuondoa vikwazo vilivyokuwavinafanya wanawake washing we kugombea  huku akiwataka wanawake wajitokeze kwa wingi katika kuchagua na kuchaguliwa kwenye uchaguzi huu.

Mwenyekiti Lipumba amesema elimu wanayoitoa TGNP ya watu kuachana na mira na desturi potofu dhidi ya wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ni mzuri na ni vema vyama vote vya siasa kuunga mkono juhudi na jitihada hizi zinazofanywa na TGNP kwa kuondoa vikwazo kandamizi na mira desturi potofu zinazokuwa kikwazo kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi.

Ametoa wito kwa wanaume nchini kuwachana na mifumo dume badala ÿke wawape ruksa wanawake kugombea nafasi za uongozi amesema haya kwenye kongamano la miaka 60 ya muungano lililoandaliwa na shirika la utangazaji TBC maktaba ya taifa chuo kikuu mlimani nilipofanya nae maojiano.

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment