Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega amesema tarehe 5 /6/2024 kutakuwa na mkutano mkubwa wa kimataifa utakao fanyika Dar es salaam lengo la mkutano huu kutatuwa changamoto walizonazo wavuvi wadogo na kujifunza mbinu za kisasa za kuvua pamoja na matumizi ya teknolojia .
Kwa tanzania wavuvi wadogo asilimia 95% na wameweza kujiajili na kuajili wengine zaidi ya ajira laki mbili therathini na sita elfu na fedha wanazochangia kwa mwaka tilioni 3.4 na kwa fedha za kigeni bilioni tano na tisa, Waziri wa uvuvi na mifugo Abdallah Ulega amemshukuru na kumpongeza rais Dr Samia kwa kukuza na kuimarisha dipromasia ya uchumi ndio maana tanzania ikapewa nafasi ya kuandaa mkutano wa wavuvi wadogo kwa bara la Afrika.
Mkutano huu utachochea wavuvi wadogo wa tanzania kupata masoko ya kuuza bidhaa zao kimataifa,pia itachochea kuwepo na mabadiriko ya sera na mihongozo kwa wavuvi wadogo watanzania na Afrika kwa ujumla .pia tanzania itapata fursa ya kuwashawishi watu kuja kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi. Amesema haya wakati wa kuzungumza na wanahabari jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment