Tuesday, 21 May 2024

WATU WENYE ULEMAVU HAWAJAACHWA KWENYE BUNIFU


 Katibu Mkuu  Prof Carolyne  Nembo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia amesema katika maswala ya bunifu watu wenye ulemavu  wa aina zote wamejuishwa na kushirikishwa kikamilifu katika maswala ya bunifu ambako wizara ya Elimu inatoa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu mashuleni kuanzia Elimu ya hawali,msingi,secondary na vyuo vikuu na vya kati.Mfano kwawasio Ona wanapewa mashine za kuandikia maandishi ya nukta nundu ,kompyuta na kwa watu wenye uono hafifu na wenye uharibino wameandaliwa vitabu vyenye maandishi makubwa.

Pia serikali imeandaa wali wakufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum haya yote yanafanywa lengo watu wenye ulemavu waweze kushiriki kikamilifu kwenye bunifu na  wajue kutumia teknolojia za kisasa. Amesema haya kwenye week ya bunifu ilioandaliwa na COSTECH.

Habari na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment