Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na kati January Makamba amesema tarehe 25/05/2024 chombo cha baraza la ulinzi na usalama kwa Afrika lenye wanachama nchi kumi na tano 15 watakutana nchini Tanzania jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC lengo la kukutana kwa baraza hili ni kujadiri migogoro iliyopo kwenye nchi za Afrika.
Na nafasi za wanawake katika uwongozi na namna ya kujikwamua kiuchumi na kufanya maazimisho ya baraza hili la ulinzi na usalama la Afrika ambako lilianzishwa tarehe 25/05/2004 kwasasa limetimiza mika 20 katika mkutano wa baraza hili la ulinzi na usalama Rais Dr Samia Suluhu Hassan atakuwa mwenyekiti wa mkutano huu hii yote inatokana na Tanzania kuwa kitovu cha amani Afrika na Duniani kote.
Pia Tanzania imekuwa ni nchi ya kuongonza harakati za kupigania uhuru kwa nchi za Afrika na kuwa suluhishi wa migogoro kwenye bara la Afrika tangu enzi za Hayati Rias Nyerere, Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete na Rais Magufuri na sasa Rais Dkt Samia.
Waziri wa Mambo nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kati amesema mkutano wa baraza la ulinzi na usalama wa Afrika utauzuliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa amesema haya kwenye ofisi ya wizara ya mambo ya nje zilizopo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.
Habari Picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment