Thursday, 16 May 2024

MATAPELI WA MTANDAONI WATIWA MBALONI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam  Jumanne Mulilo amesema wamewakamata watu 27 jijini dar es salaam ambao wamekuwa wakifanya utapeli kwa kutumia raini za simu za mkononi  ,matapeli hawa walikuwa wanatuma jumbe kwenye simu tofautitofauti ili watumiwe pesa .

Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa kutoa taarifa ambazo zimepelekea kukamatwa kwa matapeli hawa ,kamanda Mulilo amesema mpaka sasa jumla ya matapeli wanaotumia simu za mkononi kwaajili ya kutapeli watu wameshakamatwa 85 amesema haaya wakati akizungumza na wanahabari makao makuu ya Jeshi la Polisi kanda maalum jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment